Kundi la wezi wenye silaha mbali mbali usiku wa kuamkia leo wamevamia Ofisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -Usharika wa Kimara -Korogwe na kuiba mali nyingi na fedha taslim kwa kuwafunga na kuwakatakata mapanga walinzi wa Chui Security Company .Baadhi ya samani zilizoibiwa ni pamoja na Computer zote ,TV Sets,PA systems nk.Wezi hao walitumia gas kuvunja sefu ya kuweka fedha pamoja na milango ya magrill kuingia ofisini.Tukiwa kwenye sehemu ya tukio askari wa doria walikuja baada ya kuitwa tangu alfaajiri saaa kumi hadi saa moja kasoro.
Tuanatoa pole kwa Washarika wa Kimara na Mchungaji wao Rev.Wilbrod Mastahi
Mungu huwa haibiwi watakiona cha Moto
Sijui kama kwenye Biblia kuna maandiko ya kuwaombea wawe ndondocha kama wenzetu wanavyowasomea albadri ili wapate kichaa, wenye ufahamu na hilo tuelezeeni tuwaombee waehuke, lakini sijawhi sikia hilo kwenye biblia
Tusiwaombee wawe ndondocha, itakuwa bora tukiwaombea kwanza watambue kuwa ni dhambi, pia waache hiyo dhambi si kanisani tuu, bali mahali popote wasiibe tena. Pia wamfahamu Bwana Yesu kuwa ni mwokozi wao, ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni na pia kupitia wao na watu wengine waokoke
poleni sana washirikakundi la wezi wenye silaha mbali mbali usiku wa kuamkia leo wamevamia ofisi za kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania -usharika wa kimara -korogwe na kuiba mali nyingi na fedha taslim kwa kuwafunga na kuwakatakata mapanga walinzi wa chui security company .baadhi ya samani zilizoibiwa ni pamoja na computer zote ,tv sets,pa systems nk.wezi hao walitumia gas kuvunja sefu ya kuweka fedha pamoja na milango ya magrill kuingia ofisini hapo.tukiwa kwenye sehemu ya tukio askari wa doria walifika baada ya kuitwa tangu alfaajiri saaa kumi hadi saa moja kasoro.
Tuanatoa pole kwa washarika wa kimara na mchungaji wao rev.wilbrod mastahi