Kizaazaa baada ya Housegirl kupekuliwa na kukutwa na uchawi na mwajiri wake

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
House girl huyo amabaye inaonekana alikuwa ni rafiki wa aliyekuwa akimfanyia kazi alikuta mkoba wake umepekuliwa na kukosa vifurushi ambavyo alipewa na mganga havipo kwenye mkoba wake

Baada ya hapo ndipo akamsubiria mwajiri wake aje na kuanza kumvaa kuwa amepekuwa mkoba wake na kumuibia, Mwajiri naye akamgeuka na kumuuliza nimekuibia kitu gani?

Housegirl akakosa cha kusema kwa kuwa zilikuwa ni dawa za kienyeji na mabishano yakaendelea huku mwajiri akikataa kumlipa fedha za kazi aliyofanya na kumrudisha kwao

Dawa za kienyeji sio uchawi
Kutumia dawa za mitishamba na kuwa na uchawi ni vitu viwili tofauti.Kuna dhana kuwa mtu anayetumia dawa za kienyeji basi huyo ni mchawi.

Mimi nina mwaka wa 20 sasa sijawahi kutibu mchafuko wa tumbo,kichomi na kichwa(kipanda uso) kwa dawa za kisasa.Lakini mimi sio mchawi,ila ninajua sana dawa za kienyeji ambazo wakati wa udogo bibi yangu mzaa Mama alikuwa akionionyesha na mimi kukariri miti na kuandika matumizi yake ktk note book.

Kuna jirani yangu alikuwa anatokwa na damu puani mara kwa mara,siku nikajikaza na kumuuliza kama anaweza kutumia dawa za kienyeji ili aone kama zitamsaidia...Nilimpa miiba ya Karunguyeye na akachoma kwa kuvuta ule moshi,akapyenga bongobonge la damu lilioganda,na toka siku hiyo anasikia tu nini maana ya kutokwa damu.

Wakati namtinu nilienda na "First Aid Kit" yangu ya kienyeji,imejaa miiba ya nungunungu,nyoya la mkia wa mbuni,ngozingozi ya Fungofungo kwa watoto wasiopata usingizi na dawa kibao za majani mwitu niliyoyakausha kwa ajili ya blood clotting nk.

Jamaa alipoona hiyo Kit akajua mimi Sangoma,nikamwambia si sangoma,hizo ni dawa tu mbadala za huduma ya kwanza ya majanga kama kutokwa damu baada ya kujikata,kuumwa na nge au nyoka,kuumwa na tandu au kuondoa uvimbe baada ya kutembelewa na dudu washa.Mpaka kesho jamaa huwa ananiita "MWANDULAMI"

Kwa hiyo nyie wadada wa mjini mnaowaza kuwa Dawa za mitishamba ni uchawi,ondoeni hiyo dhana...Kuna vijiji havina Duka la Dawa Baridi wala Famasia,huko ni mwendo wa dawa asili na mitishamba.
 
You have spoken it all Comrade!
 
Hawa watu hawana watetezi kwahiyo wakikutana na hawa wanaojifanya wa mjini ilhali wao hutenda kwa kujificha ni hatari.
Dawa si tatizo, waache kuwadhalilisha hawa watu. Kwanini asimpe dawa zake waachane kwa salama.
Pesa zikiingia, dhuluma hutawala. Huu ni upuuzi wa hali ya juu.
Huyu Dada anayaita maji ya maiti, how on earth would she know that. Na yeye ni mshirikina tu.
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Umezuka mtindo wa kuwasakama wasichana wa kazi kwa uchawi. Watu wanasahau, ukifanya hivyo kwa mwenzako nawe litarudi tu. Kuna haja ya kupuuza mambo haya ya kijinga. Hapo akiulizwa, amewahi kudhurika, jibu hana.
 
Ila alikuwa ameshikwa na kigugumizi inaonyesha alikuwa na lengo baya
 
Hawana confidence hawa na yupo ugenini. Huenda kigugumizi ni cha kupekuliwa. Ni tabia mbaya kukurupuka na kudhalilisha watu.
 
House girl huyo amabaye inaonekana alikuwa ni rafiki wa aliyekuwa akimfanyia kazi alikuta mkoba wake umepekuliwa na kukosa vifurushi ambavyo alipewa na mganga havipo kwenye mkoba wake
Baada ya hapo ndipo akamsubiria mwajiri wake aje na kuanza kumvaa kuwa amepekuwa mkoba wake na kumuibia,
Mwajiri naye akamgeuka na kumuuliza nimekuibia kitu gani? Housegirl akakosa cha kusema kwa kuwa zilikuwa ni dawa za kienyeji na mabishano yakaendelea huku mwajiri akikataa kumlipa fedha za kazi aliyofanya na kumrudisha kwao

beki Tatu anakoroma noma....kaingiliwa anga zake bila kutegemea.

Ila kwani angekutwa na vidonge vya majira ama dawa za pharmacy mama mwenye nyumba Angelika pia?
 
Hawa watu hawana watetezi kwahiyo wakikutana na hawa wanaojifanya wa mjini ilhali wao hutenda kwa kujificha ni hatari.
Dawa si tatizo, waache kuwadhalilisha hawa watu. Kwanini asimpe dawa zake waachane kwa salama.
Pesa zikiingia, dhuluma hutawala. Huu ni upuuzi wa hali ya juu.
Huyu Dada anayaita maji ya maiti, how on earth would she know that. Na yeye ni mshirikina tu.
Tena ukutane na wamjini wale wa maombi na makanisa ya kisasa. Utajuta
 
beki Tatu anakoroma noma....kaingiliwa anga zake bila kutegemea.

Ila kwani angekutwa na vidonge vya majira ama dawa za pharmacy mama mwenye nyumba Angelika pia?
Hakuna cha anga hapo. Huyo Dada wa kazi ni mtu mzima na inawezekana na yeye amewahi kusikia suala la wafanyakazi wa ndani kuambiwa wachawi. Hivi akifumwa na uchawi anaweza kuwa na ujasiri wa kuudai? Uchawi ni makorokoro au mwili wa muhusika? Walianza vikongwe, wakafuata walemavu wa ngozi na sasa wanawanyemelea hao kina dada
 
Hii clip ni tata...
Wote wawili mfanyakazi na mwajiri wamepinda...
Kwa mazungumzo yao na mabishano yao tu si watu wenye ustaharabu...sijawai kuwa na mfanyakazi wa kunijibu ngebe...
Na sijawai kuongea na mfanyakazi kwa kebehi kiasi hicho...yani ni kama huyu mwajiri alikuwa anataka ugomvi wa ngumi...maana sijaona sababu ya yeye kuendelea kum-provoke huyu mama (sijui dada maana sauti imekomaa)

Mimi msichana tukishindwana nampa nauli anaenda kwao...kuna maana gani kuendelea kurumbana na mtu ambaye umeshaamua kuwa anaondoka????huyu mama hata mumewe atakuwa na shida...ni typical ya wanawake wanaoongea bila summary...amerefusha discussion bila sababu...kuna kitu alikuwa anatafuta kwa huyu mfanyakazi kinguvu...MKONG'OTO...

Hayo mengine ya uchawi, sijui dawa za kienyeji so far hayana proof hivyo siwezi ku judge...inaweza kuwa uchawi au dawa tu kwani huwezi lazimisha mtu mzima akwambie anaumwa nini...ugonjwa ni siri ya mtu....

Ila hata mimi sipendi madawa nisoyajua nyumbani kwangu sababu dunia imeharibika sana these days...ingawa naamini sana mitishamba...
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Umezuka mtindo wa kuwasakama wasichana wa kazi kwa uchawi. Watu wanasahau, ukifanya hivyo kwa mwenzako nawe litarudi tu. Kuna haja ya kupuuza mambo haya ya kijinga. Hapo akiulizwa, amewahi kudhurika, jibu hana.
HayajakukutA mkuu tema matee
 
HayajakukutA mkuu tema matee
Hayajakukuta ndio chaka la kuruhusu tuhuma zisizo na uthibitisho. Can you judge anything from that clip? Kwa kuwa yamekukuta basi ni lazima yawe sahihi. Hawa watu ni wanyonge mno. Wapo ugenini na hakuna utetezi. They are very vulnerable. Wanalipwa kidogo na kila udhaifu wa nyumba huelekezwa kwao.
 
Hii clip ni tata...
Wote wawili mfanyakazi na mwajiri wamepinda...
Kwa mazungumzo yao na mabishano yao tu si watu wenye ustaharabu...sijawai kuwa na mfanyakazi wa kunijibu ngebe...
Na sijawai kuongea na mfanyakazi kwa kebehi kiasi hicho...yani ni kama huyu mwajiri alikuwa anataka ugomvi wa ngumi...maana sijaona sababu ya yeye kuendelea kum-provoke huyu mama (sijui dada maana sauti imekomaa)

Mimi msichana tukishindwana nampa nauli anaenda kwao...kuna maana gani kuendelea kurumbana na mtu ambaye umeshaamua kuwa anaondoka????huyu mama hata mumewe atakuwa na shida...ni typical ya wanawake wanaoongea bila summary...amerefusha discussion bila sababu...kuna kitu alikuwa anatafuta kwa huyu mfanyakazi kinguvu...MKONG'OTO...

Hayo mengine ya uchawi, sijui dawa za kienyeji so far hayana proof hivyo siwezi ku judge...inaweza kuwa uchawi au dawa tu kwani huwezi lazimisha mtu mzima akwambie anaumwa nini...ugonjwa ni siri ya mtu....

Ila hata mimi sipendi madawa nisoyajua nyumbani kwangu sababu dunia imeharibika sana these days...ingawa naamini sana mitishamba...
Wote wagomvi..hakuna mwenye afadhali
 
Dawa za kienyeji sio uchawi
Kutumia dawa za mitishamba na kuwa na uchawi ni vitu viwili tofauti.Kuna dhana kuwa mtu anayetumia dawa za kienyeji basi huyo ni mchawi.

Mimi nina mwaka wa 20 sasa sijawahi kutibu mchafuko wa tumbo,kichomi na kichwa(kipanda uso) kwa dawa za kisasa.Lakini mimi sio mchawi,ila ninajua sana dawa za kienyeji ambazo wakati wa udogo bibi yangu mzaa Mama alikuwa akionionyesha na mimi kukariri miti na kuandika matumizi yake ktk note book.

Kuna jirani yangu alikuwa anatokwa na damu puani mara kwa mara,siku nikajikaza na kumuuliza kama anaweza kutumia dawa za kienyeji ili aone kama zitamsaidia...Nilimpa miiba ya Karunguyeye na akachoma kwa kuvuta ule moshi,akapyenga bongobonge la damu lilioganda,na toka siku hiyo anasikia tu nini maana ya kutokwa damu.

Wakati namtinu nilienda na "First Aid Kit" yangu ya kienyeji,imejaa miiba ya nungunungu,nyoya la mkia wa mbuni,ngozingozi ya Fungofungo kwa watoto wasiopata usingizi na dawa kibao za majani mwitu niliyoyakausha kwa ajili ya blood clotting nk.

Jamaa alipoona hiyo Kit akajua mimi Sangoma,nikamwambia si sangoma,hizo ni dawa tu mbadala za huduma ya kwanza ya majanga kama kutokwa damu baada ya kujikata,kuumwa na nge au nyoka,kuumwa na tandu au kuondoa uvimbe baada ya kutembelewa na dudu washa.Mpaka kesho jamaa huwa ananiita "MWANDULAMI"

Kwa hiyo nyie wadada wa mjini mnaowaza kuwa Dawa za mitishamba ni uchawi,ondoeni hiyo dhana...Kuna vijiji havina Duka la Dawa Baridi wala Famasia,huko ni mwendo wa dawa asili na mitishamba.
Ni kama hujasikiliza vizuri hayo maongezi!
HG aliulizwa before kama anaumwa akajibu haumwi na hakuna dawa yoyote anayotumia! Sasa utasemaje ni dawa za kawaida?
 
Hii clip ni tata...
Wote wawili mfanyakazi na mwajiri wamepinda...
Kwa mazungumzo yao na mabishano yao tu si watu wenye ustaharabu...sijawai kuwa na mfanyakazi wa kunijibu ngebe...
Na sijawai kuongea na mfanyakazi kwa kebehi kiasi hicho...yani ni kama huyu mwajiri alikuwa anataka ugomvi wa ngumi...maana sijaona sababu ya yeye kuendelea kum-provoke huyu mama (sijui dada maana sauti imekomaa)

Mimi msichana tukishindwana nampa nauli anaenda kwao...kuna maana gani kuendelea kurumbana na mtu ambaye umeshaamua kuwa anaondoka????huyu mama hata mumewe atakuwa na shida...ni typical ya wanawake wanaoongea bila summary...amerefusha discussion bila sababu...kuna kitu alikuwa anatafuta kwa huyu mfanyakazi kinguvu...MKONG'OTO...

Hayo mengine ya uchawi, sijui dawa za kienyeji so far hayana proof hivyo siwezi ku judge...inaweza kuwa uchawi au dawa tu kwani huwezi lazimisha mtu mzima akwambie anaumwa nini...ugonjwa ni siri ya mtu....

Ila hata mimi sipendi madawa nisoyajua nyumbani kwangu sababu dunia imeharibika sana these days...ingawa naamini sana mitishamba...
Mwenyewe anakuambia "ana moto"hahaha.

Hao wamekutana pipa na mfuniko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom