Kiza hutengeneza maumbo?

Mshana we ni mwongo sana vitu hivyo hakuna hata uchawi nayo ni mambo yakusadikika tu.
 
Hata horror movies ukiwa unaangalia unatishika tena unaogopa kwelikweli na huku unajua ile ni muvi tu imeektiwa.fikra inaumba sana ukishindwa kuimudu mfano ikitokea mtu amefariki mtu anakwambia kwa hakika kbs nimemuona marehem kapita hapa au kasimama huku hofu imemjaa.hizo fikra unaziumba mwnyw ilhali kiuhalisia hamna hicho kitu na hakitatokea eti umuone marehem kakusimamia.
 
Na ndio maana kuna watu huwa hawapendi kabisa kuziangalia
 
Duu we jamaa hauna undugu au uhusiano wowote na marehemu Sheikh Yahya Hussein!?
 
Daaa umenikumbusha mbali kidogo uliposema ananyosha mkono anazima taa.
hzo stori bado zpo mkuu.
 
mkuu wewe noma
 
Hahahaha! Mkuu umenikumbusha mbali sana. Iliwahi kutokea nikiwa nasoma Advance. Kuna Jamaa alisimamishwa shule kwa makosa ya kinidhamu. Sasa watu wakawa wanatania kuwa kuna mzimu wake kila siku unazurura hapo shuleni. Sasa siku moja tumetokea darasani usiku kupiga msuli,tumekaa mahali tunajipumzisha huku tunasikiliza redio. Bahati mbaya nikapitiwa na usingizi.

Niliokuwa nimekaa nao wakaenda kutafuta shuka leupe pee,wakaja kunifunika kisha wakawajulisha watu kuwa Leo waje wakamshuhudie mzimu wa Jamaa. Sasa wamejikusanya wakaja wengi,wakaanza kujiuliza eti siyo mzimu. Ile wamesema twendeni tukamfumue,mm nikakurupuka kwa wenge la ajabu .......hahahaha! Watu wote walikimbia mpaka wale waliokuwa wamecheza mchezo. Na mm nilipoona wanakimbia,nikawafata mbio nikijua kuna noma. Bado shuka limenishikilia tu. Shule nzima walitoka mbio wanakimbia. Majamaa na wenyewe hawakuwa na uwezo tena wa kujitutumua. Watu tulicheka Sana siku hyo.
 
 
Mimi kwenye mawingu hasa jioni, naweza angalia juu nikaona wingu limetengeneza picha kama ya mnyama au mtu au jengo,

Hiyo imekaaje bwana Mshana maana mmmmh!
 
Mimi kwenye mawingu hasa jioni, naweza angalia juu nikaona wingu limetengeneza picha kama ya mnyama au mtu au jengo,

Hiyo imekaaje bwana Mshana maana mmmmh!
Kuna cases chache ni kweli lakini nyingi ni mind tricks na hizo picha hutengenezwa kwenye medulla zikarushwa machoni kisha hayo mawingu ni kama projector
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…