Kiwanja cha kununua kinatakiwa

Wakuu, kwanza poleni na majukumu ya hapa na pale, lakini ni suala la kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuendelea kuwa nasi katika kazi za hapa na pale.

Naomba kusema yaliyonileta kwa jamvi siku ya leo. Kama heading inavyojieleza kwa uwazi wake, kiwanja kinatakiwa maeneo ya Kibaha, kuanzia Maili Moja mpaka Mlandizi.

Kama kuna mwenye nacho au ndugu yake maeneo ya Kinondoni, Tegeta, Bunju mpaka Bagamoyo nako nakupenda pia.

1. Kiwanja kiwe kimepimwa.
2. Kisiwe na mgogoro wa familia na jamii inayozunguka
3. Kiwe karibu na barabara kuu.
4. Kisiwe katikati ya nyumba kiasi cha kukosa kupata njia ya kupitisha gar nk.
5. Ukubwa kuanzia 20×20 na kuendelea, offer yangu mwisho millioni 5.

Natanguliza zangu shukrani. Mwenye nacho au ndugu anaweza kuni PM.
Mkuu, ebu acha maskhara kwenye mambo ya msingi wallahi...
 
Kama unataka kiwanja maeneo hayo fika RUVU vipo vingi sana maeneo ya RUVU kwenye Soko la samaki vinaanzia 1mil > na umbali wa kutoka Mlandizi hadi Ruvu hauzid 4km
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom