Kiwango cha madawa ya kulevya mtaani kimeshuka

Kiwango cha madawa ya kulevya mtaani kimeshuka

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema kuwa kutokana na juhudi kubwa wanazozifanya kwa kushirikiana na jamii, wameweza kupambana na uuzwaji wa dawa za kulevya nchini, na kwa sasa kiwango cha dawa hizo mtaani kimeshuka.

“Kiwango cha dawa za kulevya mtaani kimeshuka kwa kiwango kikubwa sana. Leo hii nikikwambia, ‘Nenda katafute heroine au cocaine,’ huwezi kuipata kirahisi kama ilivyokuwa mwanzo, ambapo ukienda Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni Mapipa au Mkwajuni unakuta mtu anauza yupo wazi kabisa,” amesema Kamishna Jenerali Lyimo.

Lyimo alikuwa akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo Agosti 14, 2025, kufuatia kukamatwa kwa shehena kubwa ya dawa mpya ya kulevya aina ya Mitragyna speciosa, ikiwa katika mifuko 756 na uzito wa kilogramu 18,485.6 (takriban tani 18.5), ambayo ilikuwa ikiingizwa nchini kama mbolea.
 
Aretas lyimo anapambana sana kongole kwake wakati mwingine anaingia yeye mwenyewe site
 
Back
Top Bottom