Kiwango cha faini mahakama ya mafisadi chapunguzwa

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
1,808
2,000
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inatarajia kujadili kushusha kiwango cha fedha kinachohusika katika makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kwenye mahakama ya mafisadi ili kukomesha vitendo vya rushwa.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Nimeulizwa sana na waandishi wa habari tangu Julai hadi sasa walitegemea kungekuwa na kesi nyingi lakini kuna kesi moja katika Mahakama ya Mafisadi tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi ndiyo mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua,”amesema.

Aliongeza kwa sasa waliozoea kupora mabilioni wamerudi nyuma ambapo wezi hao wameonekana wakiiba fedha chini ya Sh bilioni moja iliyopo kisheria hivyo wanategemea kujadili sheria hiyo ili iwalenge hata wanaochukua kiasi kidogo.

“Sisi kama serikali tukiona wizi sasa umenza kupungua na kuenea katika viwango vya Sh milioni 400, 500, 700 tumeanza kujadiliana kuangalia uwezekano wa kushusha kiwango cha fedha ili tuweze kukomesha kabisa udokozi, ubadhilifu, wizi wa fedha au mali ya umma,”alisema.

Aidha alifafanua uamuzi wa Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda kutafuta vijana wanaojua sheria ili kusaidia wananchi kabla ya kwenda mahakamani ni mzuri.

Aliongeza kuwa tayari wamepeleka mswada wa msaada wa kisheria ambao utasaidia wananchi hasa wa vijijini na wanawake ambao ndiyo wanaumizwa na desturi zilizopitwa na muda ili kuwasaidia kupata haki na itakuwa na wasaidizi wa kisheria nchi nzima wapatao 4,900.

Makonda alisema wamejadili utoaji na upatikanaji wa haki kwa wakati kwani kuna changamoto ya watu kuwa wengi na kuchelewa kupata haki zao.

Alisema kwa kuona adha hiyo mkoa huo kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya watajenga Mahakama za Mwanzo 20 ili kuongeza kasi za utoaji na upatikanaji wa haki kwa wananchi endapo wanapopelekwa vituo vya polisi.
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
I see!!Mimi nilijua wataanza na Edward Lowassa.Maana wakati wa kampeni tulia,biwa Mahakama hii itaanzishwa ili wote walioiibia nchi kama Braza Eddo walale lupango.

Tukaambiwa huyo Eddo ndio mwizi wa wezi wote na Mahakama hii inamstahili.Lkn sasa wanalalamika kuwa "hakuna kesi?" Eti kwa sbb watu wanaiba hela kidogo kuanzia milioni 200,400 na 500?

Kwa hiyo Uhujumu uchuni ni kuiba kuanzia bilioni 1?ukiiba hata milioni 100 iliyotengwa kujenga Kisima cha Maji cha Wananchi wa kata ya Mwigumbi Shinyanga inakuwa sio uhujumu?kumbe kiwango cha kuiba inabidi sasa tupunguze....Tuibe kidogo kidogo jamani...unaseti dokezo lako la milioni 300 au 995,mnapiga mkwanja mnatulia....maana ili uitwe muhujumu uchumi lazima upige kuanzia B moja na kuendelea.
 
Mavipunda

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
5,980
2,000
Huyu Mwakiyembeni anadhani watu wote ni vifuu kama wapiga kura wake? Kama ile Mahakama ingefanya kazi vyema ingekua mtaji mzuri kwa UPINZANI kushinda uchaguzi ujao.. Takriban washitakiwa wote wangelitoka CCCM. Hata huyo Lowasaa alipiga hela alipokuwa cccm hivyo kama angepandishwa mahakama ya mafisadi angekuwa na kundi kubwa la watuhumiwa wenzake kutoka huko.. Pale walibugi kuanzisha ile kitu kwanza matumizi mabaya ya fedha na pili ilikuwa ni kitanzi cha kuinyonga cccm
 
Mavipunda

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
5,980
2,000
I see!!Mimi nilijua wataanza na Edward Lowassa.Maana wakati wa kampeni tulia,biwa Mahakama hii itaanzishwa ili wote walioiibia nchi kama Braza Eddo walale lupango.

Tukaambiwa huyo Eddo ndio mwizi wa wezi wote na Mahakama hii inamstahili.Lkn sasa wanalalamika kuwa "hakuna kesi?" Eti kwa sbb watu wanaiba hela kidogo kuanzia milioni 200,400 na 500?

Kwa hiyo Uhujumu uchuni ni kuiba kuanzia bilioni 1?ukiiba hata milioni 100 iliyotengwa kujenga Kisima cha Maji cha Wananchi wa kata ya Mwigumbi Shinyanga inakuwa sio uhujumu?kumbe kiwango cha kuiba inabidi sasa tupunguze....Tuibe kidogo kidogo jamani...unaseti dokezo lako la milioni 300 au 995,mnapiga mkwanja mnatulia....maana ili uitwe muhujumu uchumi lazima upige kuanzia B moja na kuendelea.
Mi nazidi kukata tamaa na hii nchi.. Huyu Mwakiyembeni nae alitakiwa apande hapo mahakama ya mafisadi si unakumbuka aliyoyafanya pale Mawasiliano na Uchukuzi afu JP MPiana alikaa mwezi mzima akitafuta mawaziri waadilifu akiwemo huyo...
 
Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,170
2,000
Mi nazidi kukata tamaa na hii nchi.. Huyu Mwakiyembeni nae alitakiwa apande hapo mahakama ya mafisadi si unakumbuka aliyoyafanya pale Mawasiliano na Uchukuzi afu JP MPiana alikaa mwezi mzima akitafuta mawaziri waadilifu akiwemo huyo...
Ndege wafananao...
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,904
2,000
Wakati jirani zetu WAMEPATA CJ/JAJI MKUU MPYA na TAYARI ameweka KITENGO maalumu cha mahakama ya Mafisadi.
Amewaagiza MAJAJI kuwa KESI zote za UFISADI zisikilizwe ndani ya MIEZI 3 tu kisha hukumu itolewe!
Amewaonya kuwa JAJI yeyote ATAKAYETOA VISINGIZIO vya UCHELEWESHWAJI wa kesi ataenda NYUMBANI!
Sisi huku kwetu bado TUNAJIVUTA hatujaona kasi ya kufanya hivyo.
Sijui limeishia wapi na kubaki ni MIJADALA tu.
Mwakyembe atuambie!!
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,266
2,000
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inatarajia kujadili kushusha kiwango cha fedha kinachohusika katika makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kwenye mahakama ya mafisadi ili kukomesha vitendo vya rushwa.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Nimeulizwa sana na waandishi wa habari tangu Julai hadi sasa walitegemea kungekuwa na kesi nyingi lakini kuna kesi moja katika Mahakama ya Mafisadi tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi ndiyo mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua,”amesema.

Aliongeza kwa sasa waliozoea kupora mabilioni wamerudi nyuma ambapo wezi hao wameonekana wakiiba fedha chini ya Sh bilioni moja iliyopo kisheria hivyo wanategemea kujadili sheria hiyo ili iwalenge hata wanaochukua kiasi kidogo.

“Sisi kama serikali tukiona wizi sasa umenza kupungua na kuenea katika viwango vya Sh milioni 400, 500, 700 tumeanza kujadiliana kuangalia uwezekano wa kushusha kiwango cha fedha ili tuweze kukomesha kabisa udokozi, ubadhilifu, wizi wa fedha au mali ya umma,”alisema.

Aidha alifafanua uamuzi wa Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda kutafuta vijana wanaojua sheria ili kusaidia wananchi kabla ya kwenda mahakamani ni mzuri.

Aliongeza kuwa tayari wamepeleka mswada wa msaada wa kisheria ambao utasaidia wananchi hasa wa vijijini na wanawake ambao ndiyo wanaumizwa na desturi zilizopitwa na muda ili kuwasaidia kupata haki na itakuwa na wasaidizi wa kisheria nchi nzima wapatao 4,900.

Makonda alisema wamejadili utoaji na upatikanaji wa haki kwa wakati kwani kuna changamoto ya watu kuwa wengi na kuchelewa kupata haki zao.

Alisema kwa kuona adha hiyo mkoa huo kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya watajenga Mahakama za Mwanzo 20 ili kuongeza kasi za utoaji na upatikanaji wa haki kwa wananchi endapo wanapopelekwa vituo vya polisi.
Sahihisha heading!
 
Bhikalamba

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
814
1,000
Kwani mahakama za kawaida zinaruhusu kuiba kiasi gani bila kushitakiwa!?
A very nice question, unajua mimi nilikuwa namshangaa huyu jamaa Mark-Wembe eti hakuna kesi kwa sababu watu wanaiba kidogo. Kwani hicho kidogo kimeruhusiwa kisheria. Lakini pia vipi wale jamaa wa Kiwira, Tangold, Meremeta, Richmond, Escrow, Deep green, Epa n.k , je hawapaswi kupelekwa Kule mbona kesi zimekuwa adimu wakati madudu yaliyo Kwisha fanyika yapo lukuki. Au ndiyo kuogopa kufukua makaburi kwani harufu yake ni Kali yaweza mdhuru mfukuaji
 
The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,289
2,000
Hii nchi imekaa kifutuhi futuhi tu kwa kila kitu, Elimu, sheria, kilimo, sayansi, mawasiliano, technology, afya yaani hakuna cha afadhali. Tulikosea wapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom