Mkuu, umefikiria jambo la maana sana mkuu.
lakini unajua viwanda vya caste iron na fabrication ya iron vilikuwa vingapi Tanzania?
mimi najua viwili tu, kimoja ni Moshi machine tools, na kingine kilikuwa Ulanga.
ilikuwa kazi ya Nyerere..............mzee wangu alikuwa anachongesha spare za lorry lake hapo, spare za mandolini alikuwa anachongesha hapo pia.
wahuni wamekiua kiwanda ili wafanye biashara za spare za machines including magari kuwa ghali, na kuanzisha biashara ya used spare parts..............UHUNI mtupu!!!
ukiachilia mbali economic value ya kiwanda tajwa kwa wilaya ya Hai, uwepo wake ungelikuwa na economic vlue kubwa sana kwa nchi hii.......spare zote za mitambo na magari zingeweza kutengenezwa hapo.......at least karibia zote.
sasa hivi watu wananunua tyre rod end ya used..........si kifo hiki.
Watu wangelijua ni kwa nini CCM haitakiwi kuwepo.......hata as a political party, nchi hii ingeendelea sana.