MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,882
Mkuu, hili chapisho ulikuwa umewahi kulisoma hapo kabla ??? Mimi ninayo nakala ngumu (Hard Copy) ambayo ilichapishwa mwaka 1973. Soma hicho kitabu, taarifa kuhusu Chief Edward zipo. Tena waandishi wanaenda mbali zaidi kuweka hadi Exchange of Notes ambazo Sultani wa Zanzibar baada ya mkutano wa Berlin analalamika kwa Uingereza na Ujerumani akidai kwamba Aruscha (Arusha) na maeneo mengine ya Uchagani yalikuwa ni mali ya Zanzibar (Under Zanzibar Suzerain), hivyo angehusishwa kwenye ule mkutano.Malcom...
Nimeanza kutafuta hizi taarifa:
Sijapata hiyo taarifa lakini naendelea.
Nimeona na hiyo hapo chini:
Tanzania treaty practice [by] Earle E. Seaton [and] Sosthenes T. Maliti. (Book, 1973) [WorldCat.org]
Get this from a library! Tanzania treaty practice [by] Earle E. Seaton [and] Sosthenes T. Maliti.. [Earle Edward Seaton; Sosthenes T Maliti]www.worldcat.org
Bahati mbaya sijaweza kufungua na kusoma kuhusu Wamasai kudai uhuru wao.
Lakini umenisaidia kwa kueleza kuwa "Chief" Edward alishauriwa na watu kutoka Amerika adai uhuru.
Ndiyo kusema yeye mwenyewe hakuwa na fikra ya kuutaka uhuru wake?
Je aliunda chama cha kuwaunganisha watu wake?
Maswali ni mengi.
Gaddafi alianza vizuri na alipata heshima kubwa Libya, laiti angekubali kukubaliana na mabadiliko ya dunia na kuacha demkrasia ichukue mkondo wake angebaki kuwa baba wa Taifa la Libya na heshima zote.Ongezeo, tumemsoma Kwame, Nelson, Keneth, Ghaddafi, Mugabe, BenBella, Nujoma na wengineo wa nyakati hizi katika contemporary African politics.
Lakini bado kwa sisi wengine tunamuona Nyerere kama aliwazidi wengi ktk uongozi hasa ktk kujenga msingi wa uongozi katika awamu ya kwanza ya uongozi baada ya uhuru.
Mkuu Mohamed,Malcom,
Mimi sina tatizo na taarifa hizi nauliza ili nipate kujua.
Earle Seaton nimemkuta katika Nyaraka za Sykes na mimi naamini ndiye mwandishi wa kwanza kumuhusisha na harakati za uhuru wa Tanganyika watu wakamsoma.
Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utakuta historia yake humo.
Malcom...Mkuu, hili chapisho ulikuwa umewahi kulisoma hapo kabla ??? Mimi ninayo nakala ngumu (Hard Copy) ambayo ilichapishwa mwaka 1973. Soma hicho kitabu, taarifa kuhusu Chief Edward zipo. Tena waandishi wanaenda mbali zaidi kuweka hadi Exchange of Notes ambazo Sultani wa Zanzibar baada ya mkutano wa Berlin analalamika kwa Uingereza na Ujerumani akidai kwamba Aruscha (Arusha) na maeneo mengine ya Uchagani yalikuwa ni mali ya Zanzibar (Under Zanzibar Suzerain), hivyo angehusishwa kwenye ule mkutano.
Mkuu, umeniambia kwa ujasiri kabisa kwamba umesoma maandiko yote kuhusu Tanganyika. Lakini kwanini taarifa muhimu kama hizi kuhusu Tanganyika zikupite ???
Shukrani, nitajitahidi....Malcom...
Kweli nimesoma mengi lakini taarifa hii sikupata kusoma kokote lazima nikwambie ukweli.
Ndiyo maana nikaingia kutafuta hizi taarifa.
Hizi ni taarifa muhimu sana.
Hata John Iliffe ambae ndiye bingwa wa historia ya Tanzania hakuna popote amegusia hata kwa mbali.
Nakushukuru sana.
Ikiwa si taklif kwako nitashukuru kupata screen shots za vipande muhimu hasa hivyo muhimu vya kudai uhuru ingawa sijui ingewezekanaje maana zipi zile article 26 na 27 za Mandate Territory ambazo Seaton alikuwa bingwa na anazijua fika.
Nitakachofaya nitawasiliana na jamaa zangu Zanzibar Archives nione kama kuna lolote kuhusu Sultan katika kadhia hii.
Nitakachopata nitakiweka hapa In Shaa Alah.
Gold...Acha kujirudiarudia kila siku wewe Mzee. Wewe si mzima tushang'amua hilo, una ugonjwa wa akili kila mara kujirudiarudia na stories zako na kutafuta mwanya wowote lengo lako kuu likiwa kusifia Sykes kwa namna yoyote. Unajishushia hadhi na maandiko yako hayana credibility ya kuwa historia sababu una upendeleo wa wazi.
Usharejesha ufidhuli tayari. Hakuna tatizoSithubutu kukurejeshea ufedhuli.
James Comey, unajua hoja nzima hapa ni kutaka kuonyesha jambo kuhusu NyerereMzee,
Nimepata shauku, andiko la Nguruvi linatakiwa kudhibitishwa.
Kwa ufahamo wako, ni kweli kuwa Ally Sykes hakuwai toa hutuba yoyote ya kudai uhuru nje ya Mwembe Togwa au nje ya Dar esam Salaam?
MS,James...
Nguruvi haipendi historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo mimi nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kabla ya mimi kuandika historia hii historia ya TANU na uhuru ilikuwa ikitamtaja Nyerere peke yake.
Hapo ndipo mimi nikaandika historia ya harakati za uhuru kupitia Nyaraka za Sykes.
Ukifanya rejea nyuma utaona niliyoandika.
Yeye anaemkusudia ni Abdul Sykes si Ally Sykes mdogo wake.
Kleist Sykes baba yao hawa ndugu wawili na Abbas Sykes ndiye aliyeasisi African Association mwaka wa 1929 lakini hakuna popote nilipokuta kuwa alikuwa anahutubia mikutano ya hadhara.
Sababu ni kuwa wakati wa African Association hadi TAA viongozi hawakuwa wanaitisha mikutano ya hadhara.
Mikutano ya hadhara ilianza baada ya TANU kuundwa 1954.
Nguruvi tatizo lake ni kuwa nisingeandika historia ya Abdul Sykes anataka tubakie ni ile historia rasmi ya Chuo Cha CCM Kivukoni ambayo Abdul Sykes na wazalendo wengine hawakutajwa ila Julius Nyerere peke yake
Mimi ni mpenzi wa kufuatilia historia na huwa napenda eye witness hasa ktk historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.James Comey, unajua hoja nzima hapa ni kutaka kuonyesha jambo kuhusu Nyerere
Mada ya katiba imekuja mahususi kwasababu tumewahi kujadiliana na Mo na kumwambia aliyeandika katiba ya TANU ni Julius Kambarage Nyerere wa Butiama.
Ukisoma bandiko lake, Mo anasisitiza kuwa katiba imenukuliwa neno kwa neno kutoka Ghana.
Tukubaliane naye kwa hilo, swali linabaki nani alinukuu katiba hiyo? hapa hatakueleza
Kumbuka kuanzia 1929 Mwalimu Cecil Matola na Kleist wakiasisi chama , na hapa Cecil ndiye chair hadi mapinduzi yaliyofuatia ya akina Abdul na hadi Abdul anagaragazwa na Mwalimu Nyerere pale Anatouglo hakuna kitu kilichoitwa katiba, iwe ya page 1 au kunukuu kutoka South Africa
Hapa haina maana Nyerere alianzisha harakati, la hasha, wakati anazaliwa shughuli za siasa zilishaanza. Wakati anakuja Dar alikuwa na taarifa za uwepo wa chama ukizingatia alikuwa kiongozi Makerere , alikuwa kiongozi Tawi la Tabora, alikuwa Msomi wa kweli
Kazi ya Mo ni moja kutafuta kila hiyana kumdunisha, kumzodoa Mwalimu n.k.
Mada hapo juu imekuja mahususi kuonyesha kwamba Nyerere hakuandika katiba
Well, tuonyeshe ya Abdul Sykes ya kunukuu! kutoka popote , iwe nusu ukurasa au mstari mmoja
Nyerere atakuwa Nyerere na ndiye Rais wa Tanganyika.
Tunawashukuru sana sana wazee wetu wakiwemo akina Abdul Sykes kwa kazi zao zilizotufanya tuwe Taifa kama leo. Hata kama Abdul hakuwahi kuwa katibu kata, kazi zake na wenzake ni za kutukuka na ziheshimiwe
Nguruvi...Usharejesha ufidhuli tayari. Hakuna tatizo
Mjibu James Comey hoja yake. Ni wapi na lini AbdulWahid Kleist Sykes Mbuwane aliwahi kuhutubia mkutano wa kuimarisha chama au kudai uhuru nje ya eneo la Mwembe Togwa!
James...MS,
Nashukuru, ninazidi kuelewa utofauti wa Julius Nyerere na viongozi wengine wa TANU. Kiufupi iwe TAA iwe TANU Nyerere ndiye aliipeleka mikoani. Na hii ndiyo hoja ninayoiona ya Nguruvi ambayo anaipia chapuo kuwa kwanini maelezo yako mengi huwa yanatukuza "wazee wako" mara nyingi kuliko wazee wote waliopigania nchi?
James...Mimi ni mpenzi wa kufuatilia historia na huwa napenda eye witness hasa ktk historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Huwa naonaga mambo mengi yanajadiliwa humu wakati watu kama Maria Nyerere na wengine ambao walikuwa karibu na Nyerere wangeweza kuyatolea ufafanuzi.
Bado naamini kuwa Nyerere alikuwa nanuwezo mkubwa wa kuandika katiba ya TANU pasi na kukopi ya CPP. Ama idhibitishwe vinginevyo.
Kwangu naona hoja nyepesi kutoka kwa mzee MS kuamini kuwa hiyo katika ilikopiwa neno kwa neno kwa kuogopa kubatilishwa na Britisham Colonial Government. Kwamba TANU ilikosa utashi kitu ambacho kinaacha maswali mengi kuliko majibu.
Kufariki 1933 haimaanisha Mwalim Cecil hakuwa M/kiti na muasisi 1929Nguruvi...
(Cecil Matola alifariki 1933 nna nafasi yake ikashikwa na Mzee bin Sudi).
Kuntu! Abdul hakuwahi, Nyerere alisambaza TANU kupitia mikutano ya siasa.Abdul Sykes umuhimu wake hauko katika kuhutubia mikutano.
Nafasi ya Mwalim Cecil ipo wapi?Umuhimu wake upo kuwa baba yake Kleist Sykes ndiye aliyekutana na Dr. Kwegyr Aggrey 1924 na Dr. Aggrey akampa wazo la kuunda African Association (AA) 1929.Kleist akaunda AA 1929.
Ili kutenganisha maslahi ya Waislam katika AA akaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Association) 1933 akiwa Secretary na Mzee bin Sudi akiwa Rais.
Wawili hawa walikuwa President na Secretary katika AA.
Hata sijui kwanini Abdul kaingia hapa! Just to make him relevant? OK tukubaliane na hiloAbdul Sykes alipochukua uongozi wa TAA na Dr. Kyaruzi 1950 iliundwa TAA Political Subcommittee na katika wajumbe wa kamati hii alikuwamo Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.
Nyerere hakuingizwa, aliingia kwa kumshinda Abdul na aliingia katika uongozi si katika chamaHii kamati ndiyo ilijenga msingi wa kuunda TANU 1954 baada ya Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi wa TAA baada ya uchaguzi kati yake na Abdul Sykes April 1953.
Not true Mo! sijui kwanini unarudia huu uongo! ni uongo kwasababu Nyerere alikuwa katibu wa Tawi la Tabora na 1948 alihudhuria mkutano wa chama.Hapa ndipo utakapokutana na Julius Nyerere alivyopokelewa na Abdul Sykes 1952.
Hili imefika mwisho! nashukuru tumeelewana na James Comey atakuwa amepata jibu.Historia hii ya Abdul Sykes, nduguze na baba yao na wenzake wa nyakati zile na wazalendo wengine Dar-es-Salaam na majimboni ndiyo muhimu kwangu sio kama Kleist Sykes au mwanae Abdul alikwea jukwaa kufanya mkutano wa hadhara.
Nguruvi...Kufariki 1933 haimaanisha Mwalim Cecil hakuwa M/kiti na muasisi 1929
Kuntu! Abdul hakuwahi, Nyerere alisambaza TANU kupitia mikutano ya siasa.
Nafasi ya Mwalim Cecil ipo wapi?
Hata sijui kwanini Abdul kaingia hapa! Just to make him relevant? OK tukubaliane na hilo
Nyerere hakuingizwa, aliingia kwa kumshinda Abdul na aliingia katika uongozi si katika chama
Nyerere alikuwa katibu wa Tawi Tabora, alihudhuria mkutano wa chama 1948
Not true Mo! sijui kwanini unarudia huu uongo! ni uongo kwasababu Nyerere alikuwa katibu wa Tawi la Tabora na 1948 alihudhuria mkutano wa chama.
Hapo akiwa katibu wa Tawi kubwa nchini alikutana na viongozi wa makao makuu akiwemo Abdul.
Kwamba Abdul alimpokea unataka kuuaminisha umma alimuingiza, alimfundisha siasa n.k.
Ukiacha kuwa Abdul alikuwa 'Townsman'' , kwa elimu na kufunguka katika mambo ya kimataifa hasa akiwa masomoni Edimburgh Nyerere alikuwa mbali sana
Abdul hakuwa na chochote cha kumfunza ukiachilia zile connections tu za mjini na uenyeji.
Ni kwa msingi huo Nyerere alipopata uongozi kitu cha kwanza ni kuandika katiba.
Iwe aliandika au kunukuu si hoja , hoja ni kwamba alitambua chama hakiendeshwi kama Familia na wala hakiendi kama Mtumbwi wa Tanga, chama lazima kiwe na utaratibu.
Uwezo wa Nyerere ulimfanya afike sehemu za nchi kuitangaza TANU kwa mafanikio.
Nyerere alitambua Tanganyika ni zaidi ya kidongo chekundu, Kipata na Mwembe Togwa
Katiba na mikutano ni mambo ambayo AbdulWahid Sykes na Kleist Sykes hawakufanikiwa kuyafanya. Mohamed hili si kosa kila kitu kina wakti wake.
Kosa ni kuficha ukweli kwa kumzodoa Nyerere au kumdunisha kama ulivyoleta mada ya katiba.
Well, aandike, aazime, anukuu afanye chochote ukweli utabaki pale pale ni Nyerere aliyefanya hivyo, si Abdu au Kleist. Ni muhimu ingawa ni ngumu 'kumesa' kwa mashabiki
Abdul na Wazee wengine walifanya kilicholingana na uwezo wao na hakika ulikuwa msingi mkubwa wa siasa za nchi, lakini si wao peke yao.
Mchango wa Mwana wa Butiama hauhitaji parapanda, Julius anatetewa na historia
Hili imefika mwisho! nashukuru tumeelewana na James Comey atakuwa amepata jibu.
Mzee,James...
Nyerere hakuipeleka TAA wala TANU majimboni.
Nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes vipi TAA ilienezwa majimboni toka ilipoundwa 1929 hadi kufikia 1950 ulipokuja mwamko mpya.
Unaijua historia ya Ali Migeyo?
Salum Mpunga?
Msham Awadhi?
Hamisi Heri?
Mama bint Mwalimu?
Bi. Chiku bint Said Kisusa?
Bi. Mwamtoro bint Chuma?
View attachment 2149504
Salum Mpunga
Soma kitabu.
Usichangie kwa dhana.
Hawa wazee wangu mchango wao hauna mfanowe.
Soma historia ya Schneider Abdillah Plantan kwanza katika jeshi la Wajerumani Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914-1918) kisha soma historia yake katika TAA na TANU 1950 - 1961 uhuru ulipopatikana.
Soma kitabu.
Ndiyo maana kitabu hiki haijapata kutokea kinakwenda toleo la tano kuanzia 1998.
Nashukuru, majibu nimepata mengi kuliko nilivyofikiri mwanzo.Kufariki 1933 haimaanisha Mwalim Cecil hakuwa M/kiti na muasisi 1929
Kuntu! Abdul hakuwahi, Nyerere alisambaza TANU kupitia mikutano ya siasa.
Nafasi ya Mwalim Cecil ipo wapi?
Hata sijui kwanini Abdul kaingia hapa! Just to make him relevant? OK tukubaliane na hilo
Nyerere hakuingizwa, aliingia kwa kumshinda Abdul na aliingia katika uongozi si katika chama
Nyerere alikuwa katibu wa Tawi Tabora, alihudhuria mkutano wa chama 1948
Not true Mo! sijui kwanini unarudia huu uongo! ni uongo kwasababu Nyerere alikuwa katibu wa Tawi la Tabora na 1948 alihudhuria mkutano wa chama.
Hapo akiwa katibu wa Tawi kubwa nchini alikutana na viongozi wa makao makuu akiwemo Abdul.
Kwamba Abdul alimpokea unataka kuuaminisha umma alimuingiza, alimfundisha siasa n.k.
Ukiacha kuwa Abdul alikuwa 'Townsman'' , kwa elimu na kufunguka katika mambo ya kimataifa hasa akiwa masomoni Edimburgh Nyerere alikuwa mbali sana
Abdul hakuwa na chochote cha kumfunza ukiachilia zile connections tu za mjini na uenyeji.
Ni kwa msingi huo Nyerere alipopata uongozi kitu cha kwanza ni kuandika katiba.
Iwe aliandika au kunukuu si hoja , hoja ni kwamba alitambua chama hakiendeshwi kama Familia na wala hakiendi kama Mtumbwi wa Tanga, chama lazima kiwe na utaratibu.
Uwezo wa Nyerere ulimfanya afike sehemu za nchi kuitangaza TANU kwa mafanikio.
Nyerere alitambua Tanganyika ni zaidi ya kidongo chekundu, Kipata na Mwembe Togwa
Katiba na mikutano ni mambo ambayo AbdulWahid Sykes na Kleist Sykes hawakufanikiwa kuyafanya. Mohamed hili si kosa kila kitu kina wakti wake.
Kosa ni kuficha ukweli kwa kumzodoa Nyerere au kumdunisha kama ulivyoleta mada ya katiba.
Well, aandike, aazime, anukuu afanye chochote ukweli utabaki pale pale ni Nyerere aliyefanya hivyo, si Abdu au Kleist. Ni muhimu ingawa ni ngumu 'kumesa' kwa mashabiki
Abdul na Wazee wengine walifanya kilicholingana na uwezo wao na hakika ulikuwa msingi mkubwa wa siasa za nchi, lakini si wao peke yao.
Mchango wa Mwana wa Butiama hauhitaji parapanda, Julius anatetewa na historia
Hili imefika mwisho! nashukuru tumeelewana na James Comey atakuwa amepata jibu.
James...Mzee,
Aya ya tatu inaweza upeleka huu mjadala kwingine. Hai swii kuandika maneno kama hayo kwa muandishi makini kama wewe. Hapa mtu anaweza sema unamfananisha Nyerere na wazee wako na ukamuona Nyerere hafiki ktk viwango vya hao wazee wako.
Hapo mjadala utakuwa mwingine.
Kusema Nyerere hakuipeleka TANU majimboni pia kunaweza kujadiliwa.
Huo mwamko unaouzungumzia kuanzia 1952 kwa nini haukutokea kabla ya Nyerere kuwa mwenyekiti TANU?
Sikatai kuwa kuna wazee wa makabila mbalimbali (hata wazee wangu) wameshiriki katika Uhuru wa Tanganyika lakini ukisema "Mfanowe hakuna" hapa panaleta shida.