Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,285
- 33,881
Malcom,Kumbe Thomas Marealle alianza kufahamiana na Kwame kabla ya wakina Nyerere.
Imepitwa leo tunataka ibadilishweIko poa sana
Fidel...Imepitwa leo tunataka ibadilishwe
Smart...Ahsante kwa kumbukumbu...
Ni kweli Marealle alienda UN kudai uhuru kabla ya Nyerere?Malcom,
Abdul Sykes alifahamiana na Kenyatta 1950 kabla ya Nyerere.
Ally Sykes alifahamiana na Kenneth Kaunda 1953 kabla ya Nyerere.
Abbas Sykes amesoma darasa moja King's College, Budo na Kabaka Edward Mutesa aliyekuja kuwa Rais wa kwanza wa Uganda.
Hizi zote ni historia za kusisimua sana.
Nimezieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
MALCOM LUMUMBA kauliza ''Kumbe Thomas Marealle alianza kufahamiana na Kwame kabla ya wakina Nyerere''Malcom,
Abdul Sykes alifahamiana na Kenyatta 1950 kabla ya Nyerere.
Ally Sykes alifahamiana na Kenneth Kaunda 1953 kabla ya Nyerere.
Abbas Sykes amesoma darasa moja King's College, Budo na Kabaka Edward Mutesa aliyekuja kuwa Rais wa kwanza wa Uganda.
Hizi zote ni historia za kusisimua sana.
Nimezieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Nguruvi3,MALCOM LUMUMBA kauliza ''Kumbe Thomas Marealle alianza kufahamiana na Kwame kabla ya wakina Nyerere''
Hapa subject ni Nyerere and Marealle. Hayo mengine yanakujaje?
Laki...Ni kweli Marealle alienda UN kudai uhuru kabla ya Nyerere?
Sawa hakuna shida katika hiloHaya mengine yamekuja kwa muktadha huu huu wa muulizaji kushangaa kuwa Chief Thomas Marealle alimjua kwanza Nkrumah kabla Nkrumah hajafahamiana na Nyerere.
Familia ya Sykes ukimaanisha. Sidhani kama Nyerere alitakiwa kujua kila mtu.Nikaona si vibaya nikawaeleza viongozi wengi ambao walijuana na wapigania uhuru wengine mapema sana.
Hapana, ni katika kuweka sawa maandishi. Hoja hapo ni kumzodoa Nyerere na hili hukuanza leo. Ulichotaka ni kuumbia umma Familia pendwa ilikuwa juu sana dhidi ya mvaa kaptula Julius.Hukupendezewa mimi kuongeza taarifa hii ya Kenyatta, Kaunda na Kabaka ambayo naamini si wengi wanaijua?
Hapana hujaniudhi kabisa Mohamed, umekirihisha kwa sarcasm, innuendos etcIkiwa nimekuudhi kwa kuandika haya basi niwie radhi ndugu yangu.
Shukraani mno mkuu,but muda mwingine ni vema to let it go, unatoa mada nzuri tu na sisi wasomaji/wachangiaji tunatakiwa tuisome ili kuielewa sio kuuliza maswali!,unakuta mchangiaji bila hata kujaribu kuisoma mada ili aielewe, tayari ameshakimbilia kuuliza swali ambalo nalo linaonyesha ni jinsi gani alivyo, it's time now historia ya nchi yetu na Africa hapa iandikwe kwa ukweli(facts)sio politics, kuna mengi kuhusu hasa nini kilitokea hapa nchini, pale Angola (Mr.Savimbi alikua mzalendo au msaliti?),Zimbabwe je wapiganaji wa uhuru walipigana clean war or walifanya war crimes?even SA kuna mengi watu hawajui ukweli wake, tusiwalaumu foreigners wanapotuandikia historia wakati sisi wenyewe tuna uchoyo wa ukweli.Nguruvi3,
Haya mengine yamekuja kwa muktadha huu huu wa muulizaji kushangaa kuwa Chief Thomas Marealle alimjua kwanza Nkrumah kabla Nkrumah hajafahamiana na Nyerere.
Nikaona si vibaya nikawaeleza viongozi wengi ambao walijuana na wapigania uhuru wengine mapema sana.
Hukupendezewa mimi kuongeza taarifa hii ya Kenyatta, Kaunda na Kabaka ambayo naamini si wengi wanaijua?
Ikiwa nimekuudhi kwa kuandika haya basi niwie radhi ndugu yangu.
Nguruvi3,Sawa hakuna shida katika hilo
Familia ya Sykes ukimaanisha. Sidhani kama Nyerere alitakiwa kujua kila mtu.
Hapana, ni katika kuweka sawa maandishi. Hoja hapo ni kumzodoa Nyerere na hili hukuanza leo. Ulichotaka ni kuumbia umma Familia pendwa ilikuwa juu sana dhidi ya mvaa kaptula Julius.
Hapana hujaniudhi kabisa Mohamed, umekirihisha kwa sarcasm, innuendos etc
Kuna nyakati nakuonea huruma sana jinsi Nyerere anavyoitesa nafsi yako
Huwa najiuliza, hate dhidi ya Nyerere inakujenga au kukusaidia nini ?
Kitu kimoja hutaweza kukifuta katika historia, Nyerere ni Rais wa kwanza wa Tanganyika huru
Mohamed uwe na kumbu kumbu!Hayo maneno mengine unayosema ''kuzodoa,'' ''kaptula,'' mimi sijapata kuyasema popote.
Siwezi kuwa mjinga na kukosa adabu kwa kiasi hicho.
Hakuna tatizo kuandika historia ya wazee wako !Unionee huruma mimi kwa kuandika historia ya TANU ambayo ndiyo historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
Nateseka kuona jinsi jina la Nyerere linavyokutesa! kwakweli inanitesa, ni kwanini uteseke hivyo wakati unajua historia haiandikwi inajidhihiri.Nadhani unaeteseka ni wewe si mimi.Kitu kama kinakutesa unakiacha.
Hapa kuna tatizo, historia ya Wazee wako haina shida.Wewe ndiyo uaneteseka kwa kuwa unaumia kila ukisoma historia ya kweli ya Nyerere na TANU na ndiyo maana kila ukiona nimeandika utakuja.
Ukasema walikataa baadhi ya mambo uliyowashauri wakaandika yao!Waadishi wa ''Nyerere Biography,'' walinihoji kuhusu Nyerere na wakanisifia kuwa katika watu wanaoifahamu historia ya Nyerere mimi ni mmoja wapo na hawakuishia hapo wakasifia Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu bora - ya Salim Ahmed Salim, Brig. Hashim Mbita na yangu.
Haya yameandikwa katika kitabu hiki cha Mwalimu Nyerere.
Basi kama unakubali hilo hakuna tatizoKuniambia kuwa siwezi kumfuta Julius Nyerere hili wala sihitaji wewe unifahamishe ni jambo liko wazi kabisa.
https://www.facebook.com/Mohamed uwe na kumbu kumbu!
Hakuna tatizo kuandika historia ya wazee wako !
Nateseka kuona jinsi jina la Nyerere linavyokutesa! kwakweli inanitesa, ni kwanini uteseke hivyo wakati unajua historia haiandikwi inajidhihiri.
Ile ya Rais wa Tanganyika imeshajidhihiri sijui kama itafutika. Ni Nyerere
Hapa kuna tatizo, historia ya Wazee wako haina shida.
Historia ya kweli kuna shida , ukweli kwa mujibu wako na mujibu wako hauwezi kuwa ukweli kwa kila mtu.
Hapa nateseka kidogo hasa unapowachanganyia vijana mchele na mapumba halafu kuwaambia ndio ukweli, hapana. Ukiawaambi ni ukweli wa wazee wako hakuna shida. Wazee wako si Tanganyika.
Ninaposema pumba usikirihike nina maana fyongo kama ile ya Abdul kutohutubia popote nje ya Mwembe Togwa lakini anatakiwa akuzwe kama Rais wa Tanganyika! na historia ya Familia iwe ya Tanganyika! lahaula sheikh! tusitiri , tunajitahidi kukusitiri
Ukasema walikataa baadhi ya mambo uliyowashauri wakaandika yao!
Basi kama unakubali hilo hakuna tatizo
Marealle alienda kudai Uhuru wa Wachagga, hakuwa na Chama.Laki...
Hili sina ujuzi nalo.
Wewe umesikia wapi?
Ufahamu wangu mimi kuhusu Tanganyika kufanya mawasiliano na UNO kwa kusudi la kudai uhuru nimesoma katika Nyaraza za Sykes (Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951).
Earle Seaton aliishauri TAA Political Subcommittee kuanza mazungumzo na UNO kuhusu hali ya Tanganyika kama nchi chini ya udhamini wake.
Baada ya kuundwa kwa TANU ndiyo Mwalimu Nyerere akaenda UNO February, 1955 kama msemji wa TANU chama cha kupigania uhuru wa Tanganyika.
Sasa Marealle atakwenda UNO kuwakilisha chama kipi?
Laki...Marealle alienda kudai Uhuru wa Wachagga, hakuwa na Chama.
Mzee,https://www.facebook.com/
Nguruvi,
Mimi sikejeli wala kukebehi.
Nakueleza historia ya TANU kama ukweli wake ulivyokuwa.
Na nimenyanyua kalamu baada ya kuona hizo historia zilizoandikwa zimepotoshwa.
Nani alikuwa anaijua historia ya African Association, TAA hadi kuundwa kwa TANU kwa kiwango nilichoeleza mimi?
Kadi ya TANU No. 1 Territorial President Julius Kambarage Nyerere, kadi No. 2 Ally Kleist Sykes, kadi No. 3 Abdulwahid Kleist Sykes, kadi No. 4 Waziri Dossa Aziz, kadi No. 5 Denis Phombeah (Mnyasa) Kadi No. 6 Dome Okochi Budohi (Mkenya).
Nani alikuwa anaijua historia hii?
Katika hao wanachama wa TANU sita ambae sikupata kuwajua ni wawili - Nyerere na Phombeah.
Hawa nimewasoma katika Nyaraka za Sykes.
Lakini hao wote sita nimeeleza historia zao katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kitabu hiki kimevunja rekodi tunakwenda toleo la tano Kiswahili na Kiingereza.
Kwa nini kitabu hiki kimependwa kiasi hiki?
Sababu ni kuwa hii ndiyo historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nikejeli na "Mwembe Togwa," na maneno yote upendayo mimi sirejeshi kejeli narejesha maneno ya kweli katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa ushahidi wa picha na nyaraka.
Ndiyo maana hapa nimeingia na jina langu halisi.
Wewe unaweza ukatukana, ukakejeli na kukebehi.
Anakujua nani?
Mimi niko hapa kwa picha na sauti.
Hakuna asiyenifahamu.
Mimi nimebeba dhima ya elimu yangu na heshima ya walimu wangu na heshima ya mama yangu aliyenifunza adabu.
Sithubutu kukurejeshea ufedhuli.