Kivuko cha busisi ni jipu jingine

Kivuko cha busisi ni jipu jingine

desmond JJ

Member
Joined
Jul 6, 2012
Posts
56
Reaction score
28
Nimekuwa nikitumia KIVUKO hiki kwa muda mrefu tu, gharama za kuvuka ni shilingi 400 za kitanzania kwa mtu mzima, (sitozungumzia watoto na wanafunzi Kwakuwa jipu lenyewe lipo hapa kwene gharama za kuvuka kwa watu wazima) KIVUKO /VIVUKO vya eneo hili yaani Mv. Misungwi, na Mv. Sengerema vinafanya kazi kuanzia asubuhi mpaka saa Sita usiku na uwezo wa kubeba watu zaidi ya miatatu kwa kila KIVUKO /PANTON, shida iko kwa akina ZAKAYO yaaani watoza ushuru pale kwene vibanda
Siku zote za uuzaji wao wa ticket huwa hawana shilingi 100 ya chenji kwa wanaotoa shilingi miatano (500/=).
ukiangalia pale mezani zimejaa shilingi miambili (200/=) na miatano (500/=), lakini ajabu yake hata ukitoa shilingi elfu moja bado hutapewa shilingi 600/= yako katika maana ya zile Mia mbili 3,utapewa miatano na kuambiwa hatuna shilingi Mia
Watu wanaovuka hapo kwa siku kwenda na kurudi (kutoka sengerema, geita, chato, bukoba nk ...... Kwenda Mwanza, shinyanga, na maeneo mengine Au kinyume chake) ni takribani 2000 au zaidi, sasa tutoe labda watoto na wanafunzi 300, kisha tutoe watu wengine 200 ambao wanaweza pata chenji yao kwa bahati mbaya/nzuri nao wasiwe kwene mahesabu, tufanyie kazi wasafiri 1500 ambao wanaacha tshs 100 kila siku ambayo ukizidisha kwa 1500 unapata tshs 150,000/= kila siku ambazo zinabaki kwa akina Zakayo hawa ambayo ni kama milioni 4 unusu kwa mwezi, ukiendelea zaidi utapata majibu ni kiasi gani kwa mwaka watoza ushuru hawa wanakusanya, hiyo ni moja sitazungumzia magari na deals za hapa na pale.
Kinachotatiza zaidi kutoka kwa hawa akina Zakayo ukidai chenji ambayo ni halali yako wanakuwa wakali mno, na ukiomba heri kwamba una shilingi miatatu hata kama aliepita kaacha Mia yake pale unaambiwa gharama ni mianne zaidi ya hapo hakuna maelezo ya punguzo.
Sasa hizi fedha za masalia zinakusanyiwa mfuko gani?... Kwangu hili nalo ni jipu linalosubiri kutumbuliwa
 
Back
Top Bottom