Kivuko cha Bagamoyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kivuko cha Bagamoyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Jan 4, 2012.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Magufuli pamoja na kuboronga na kauli zake tata ila hili la kununua kivuko kipya cha kutoka Bagamoyo kuja ferry nimelipenda. Litapunguza foleni kwa wakazi wa Bagamoyo na Mbezi.
  Swali ni lini kitanunuliwa? na ufisadi uliojaa kwa magamba??
   
 2. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kama kaboronga kweli basi huo utakuwa mradi usio na tija. Hayo sio maendeleo kwani kuna ardhi kubwa ya kujenga highway. Mbona vivuko vinahitajika kwa kiu kubwa sehemu nyingi nchini. Siielewi hii serikali yetu na utafiti wao. Badala kuweka bandari Bagamoyo boti za Zanzibar zi dock huko wakaweka highway na pia njia za reli hadi Dar wao wanawaza tofauti. Pumba hizi anataka kumfurahisha bosi wake.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  kaka hizi huitwa immediate solutions sioni ubaya wa kuwa na kivuko toka Bagamoyo mpaka Kivukoni au Kigamboni ni njia mbadala na inaweza kuwa ya haraka zaidi hata kushinda uwepo wa barabara pana
   
 4. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa nini gharama zake walipie wakazi wa kigamboni ambao hawatakitumia? 'si awapandishie bei za mabasi na daladala wanaosafiri kati ya dar na bagamoyo!!!! hii inadhihirisha kuwa hata hilo wazo ni la kukurupuka na kutapatapa tu, the last kicks of a dying horse. haliko kwenye ilani ya magamba 2010 wala kwenye mipango ya miundo mbinu ya jiji la dar au bagamoyo. Inaonyesha pia magamba walivyoishiwa uwezo wa kufikiria kutumia vipaji vya ubongo wao.

  Sasa tunaambiwa huyu magufuli eti ndo ana nafuu
   
 5. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ni wazo zuri japo limekuja ktk wakati mbaya
  Kumbuka ni serikali ya chama chake inayokopa watumishi mpaka sasa, uchumi upo ktk lala salama
  Ila wazo zuri sana
   
 6. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  maneno matupu hayavunji mfupa. Tuone kivuko kwanza ndio tuanze kuchangia mada
   
 7. k

  kindafu JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo yaliyopo ni kwamba kivuko cha sasa Kigamboni kinalipiwa gharama kwa kiasi kikubwa na serikali, hii ina maana hela za kodi za Watanzania wote zinatumika hapo! Kwa namna yako ya kufikiri - je, kwa nini kodi ya mtu wa Mtwara au Loliondo nk imlipie nauli mtu wa Kigamboni?
   
 8. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Dr Magufuli Anawadanganya wajinga ili kuhalalisha ubabe wake. Iweje watu wa Kigamboani na kwingineko vilipo ovuko watozwe fedha zaidi ili kuchangia fedha za kununua pantoni za Dar-Bagamoyo badala ya Serikali kuwekeza raslimali zake kununua vivuko hivyo? Hiki ni kielelzo cha kushindwa kwa Serikali iliyoko madarakani anayoitumikia Dr Magufuli kupanga prioroties zake na hivyo kuwaachaia watendaji wake kutumia ubabe katika nyadhifa zao kufanikisha malengo yao. Vitendo hivi vya Magufuli havina tofauti kabisa na wale askari wa DRC ambao huwa tunaambiwa hawalipwi mishahra ya kutosha hivyo hutumia bunduki zao kufanikisha matakwa ya kukidhi mahitaji yao binafsi.


  Je kivuko cha cha Dar-Bagamaoyo kitapunguza vilpi foleno na kwa kiwano gani ilihali hakuna mkakati wowote ulioanishwa wa kuwekeza katika miundo mbinu inayohotajika ili Pantoni hiyo iweze kuchukua abiria katika ameneo mbali mbali kama vile Ununio, Bunju, Kunduchi, White Sands< Mbezi Beach n.k.

  Kwa maoni yangu hata Dr Magufuli awachangishe vipi abiria wanaotuia kivuko cha Kigamboni na kwingineko hawezi kuata rasmlimali za kutosha kuwekeza katika miundo mbinu kama Serikali anayoitumikia haipo tayari na haioni umuhimu wa kuwelkeza katika miundo mbinu hiyo.

  Anachofanya Dr Magufuli ni kufunika udhaifu wa Serikali anayoitumikia katika matumizi ya fedha zinzokusanywa na misaada kwa kutumia ubabe kuwatoza wananchi fedha nyingi zaidi kwa huduma wanazopata chini ya wizara yake. Kwani ni chombo gani kinachopaswa kutazama na kuongeza mishahara ya wafanyakazi na vipatao vya wananchi kutokana na kuongeza kwa gharama za maisha? Si ni Serikali hii hii anayoitumikia Dr Magufuli. Hivyo Dr Magufuli angekuwa ni kiongozi bora kwanza angetumia baraza la mawaziri kuhakisha Serikali inatzama mihsahara ya wananchi na mfumuko wa bei kabala hajafiakiria kupandisha bei za huduma zinzotolewa na wizara yake.

  Pendekezo la Kutumia usafiri wa maji kati ya Dar na Bagamoyo siyo geni au ubunifu wa Dr Magufuli. Hili ni moja ya mapendekeoz yaliyotolea mapema miaka ya 90 kuepusha Jiji la Dar kukumbwa na msongamano wa watu na magari Mapendekeoz mengine yalikuwa ni kutumia usafiri wa treni katika Wazo hili-Ubungo Buguruni hadi stensheni; kuhamisha soko la Kariakoo, kuhamisha stendi ya mabasi ya mikoani toka Kisutu kwenda Ubungo na kujenga wa masoko pembezoni mwa Jiji la Dar kama vile Temeke Stereo, Kijitonyama n.k. Lakini Serikali ilyo chni ya CCM chama anachokitumiaka Dr Magufuli na serikali yake vilipuuza mapendekeo hayo hadi sasa anapoona amebanwa kwa kuwatukana na kuwadhalilisha wananchi ndipo anapotumia mapendekeoz hayo kujinasua.

  i
   
 9. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kimantiki kabla ya bei za bidha kupandishwa kwanza hufanyika utafiti wa hali za mapato na matumizi ya wananchi, ndio maana kuna idara ya National Bureau of Statistics (NBS) ikibainika mapato ya wananchi yako chini na mwajiri kuu yaani Serikali haina uwezo wa kupandisha mishahara basi mbinu zingine hutumika ili kupta fedha za kunua vitu vya muhimu kama vivuko. Serikali tuliyo nayo ni kubwa sana na gharama za kuendedshaji ni kubwa sana, achai mbali ubadhirifu wa mabilioni ya fedha unaoripotiwa katika taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali; kilamwisho wa wili mkuu wa nchi hutumia magari kati ya 20 hadi 40 toka Dar hadi Msoga Bagamoyo kuzuru miradi yake binafsi. Magari haya hutum ia mafuta, vipuri na watumishi waote wanaohudumia misafara hii hulipwa posho.

  Kama Raisi wa nchi yetu anahudumiwa hadi kufa kwake kuna haja gani ya Rais wetu aliingize taiafa garama kubwa kiasi hiki kuzuru miradi binafsi. Je ni hakia katia amazingira haya wakazi wa Kigamboni kushurutishwa kiubabe kubeba jukuma la Serikali la kuwanunulia wakazi wa Bagamaoyo kivuko?
   
Loading...