Kiukweli ninakereka na tabia hii,.

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,885
Reaction score
29,675
Baadhi ya akina dada mnatufedhehesha sana sisi kaka zenu, wadogo zenu na hata wazazi wenu kuhusiana na hili jambo:

Jamani unamkuta mdada mrembo tena mwenye kuvutia sura lakini ujue kinywa chake chaweza kutoa neno chafu kuliko choo cha manispaa, unamkuta mdada kakorofishana na mtu kisha anapandwa na jazba anaanza kuporomosha mitusi ya nguoni, hawachagui tusi na mengine unakuta wanajitukana wenyewe pasipokujua,.. Kwa mfano anamtukana mwanaume k........ma,. Daaah!! Jamani mwenzune hapa huwa napatwa na tumbo la kuhara hata kama hamna kitu tumboni, hii inatokea mbele ya hadhara wala siyo mafichoni na hawahofii lolote, kiukweli kwa tabia hii wadada wengi mnajishusha thamani maana hata mkibahatika kuingia katika ndoa sidhani kama kuna mwanaume aliyeko tiyari kuishi na mwanamke asiyekuwa na staha!!

Dada zangu jizuieni kutoa matusi mazito kiasi hiki maana mnajishusha thamani yenu mbele ya jamii,.

Cont..........
 
Huwa wanafanya pale anapokuwa kaumia na hana jinsi ya kukuonesha maumivu!!!!!!!

Hapo angekuwa na.nguvu zaidi yako angekuoiga kabisa!!!! Unadhani kwa nini matusi hayo hayatoki kwa wanaume kwenda kwa wanawake?????
 
Katika hili siwalaum watoa matusi, bali wazazi wao na walezi wao. Kwa umri wangu sijawahi kutoa tusi la namna hiyo; ni kwa sababu nimezaliwa kijijini ambapo tusi la namna hiyo adhabu yake ni kubwa sana.
Sasa mtoto alelewe uswahilini alafu kila siku anatembelea stand ya daladala bila kazi yoyote unategemea nini? Wapo pia wazazi wanaowatukana watoto wao matusi ya namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…