Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Maghufuli hamna kitu...ila chadema ndo pumba kabisa, yaani wale ni mazombi...yaani sijui hawajielewi
 
Mm binafsi naamini CDM wangepata wabunge zaidi na kura zaidi ya walizopata hata bila Lowassa, kiufupi Lowassa ndiye aliyefaidika zaidi na UKAWA kuliko UKAWA walivofaidika na Lowassa.
Huwa nikikaa na kuifikiria UKAWA ile kabla ya ujio wa Lowassa dhidi ya CCM vipande vipande, majibu yangu siku zote yanabaki CCM mshukuruni Lowassa na Mbowe!
Japo kwa upande mwingine huwa namuelewa Mbowe, nadhani alihofia Lowassa kwenda ACT kitu ambacho kingeharibu ushindani tuliouona!
 
Hee, tupo kwenye maombolezo ya kifo cha Samweli Sitta mkuu. Hii ungedubiri kidogo tumalize msiba. Hivi hsta kama ufisadi haupo chadema wangeendelea kupiga kelele kuhudu ufisadi? Mf km Msgu akifanikiwa kudhibiti ufissdi basi chsdema walazimike kuendelea kiimba ufisadi ufisadi! Halafu ulichokisems sio kipya, ndcho kinazungumzwa tangu Lowsss ajiunge chadema. Hivyo sioni jipya hapo.
 
Chadema ni chama kinachoongoza kwa unafiki duniani.

Usishangae Lugumi akawa mgombea wa chadema 2020
Huitaji hata cheti cha darasa la 7, kumpa ushauri lugumi, juu ya njia rahisi na nyepesi ya kujisafisha ktk jamii ya watanzania kutokana na tuhuma zinazomuangukia, bila kujali kama ni kweli, au la....
...ni kujiunga na chadema tu, kama alivyofanya lowassa!
 
Sema wewe maana tukisema sisi inaonekana tuna bifu naye. Kwa hakika CHADEMA wamenasa pabaya!
Muhimili wa kudai haki ni mahakamani,mwenye ushahidi na ufusadi wake akamfungulie shauri katika mahakama ya mafisadi
 
Dr.Slaa alishaona hii ni liability akaamua aondoke zake! Waliobaki wanakufa na tai zao huko!
 
Kiukweli, wanachadema, zaidi kwa sasa wanakuwa ndio nguzo, na kielelezo cha miujiza kwenye siasa za zama hizi ktk eneo hili la mama Afrika, ambao wenye kubabaishwa, kughilibiwa, na kulaghaiwa, wanachagua kukubali kuwa wanaojulikana kuwa ni wenye kuwababaisha, kuwaghilibu, na kuwalaghai, waendelee na ubabaishaji, ghilba na laghai zao( ndani ya chama chao)...!
Makamarade wenzetu (ukiacha wachache mno, walio huru kitafakari na ki fikra), ktk chadema wameipenda staili hii, na wengi wako tayari kufungwa, na hata kufwa, juu ya "mfumo huu" wa ktk chama....!
...today, in the party, well known klaat villain, turned to be a party hero!!!......and a well known hero of the party into wicked villain!
......down with dem!
 
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF mtoa mada amewahi kuandika hivi:"Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA". Andiko lake hilo, akiwa kama mtanzania asiye na chama chochote cha siasa (?), alilenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.

Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, kiukweli, Lowassa anaitesa CCM vibaya mno bila ya huruma au inajitesa yenyewe kuogopa kivuli chake.!
 
ni kweli sisi tuliomshabikia Magufuli hatukumshabikia kwa sababu tunaipenda ccm bali sababu kubwa ni chadema kuwasaliti watanzania na kuwaona kama watu wasio na akili, mageuzi ya ukweli yanaletwa na watu ambao hawakuwahi kuwemo kwenye mfumo wa ulaji wa ccm ndio maana magufuli amesema wazi hawezi kufukua makaburi hivyo chadema walifanya kosa kubwa kutuaminisha walewale wapiga dili,wapinga katiba ndio wanaweza kutuletea mabadiliko
 
Muulize mjinga ufisadi na asiye fisadi mtakatifu sana m/kiti wetu wa 10b.
Ukielewa maana ya ufisadi unaweza kujikuta nawe ni fisadi ktk area fulani.Kinyume cha ufisadi ni "kiasi" kwa maana nyingine ufisadi ni ulevi hata wa pombe au ngono.Tufike mahali tuwe specific mwizi aitwe mwizi na siyo "panyaroad"
 
Endeleeni kushabikia tu, hakuna anayewazuia. Na bei ya umeme inapanda huku mkishabikia. Yawezekana sababu ya kupanda kwa bei ya umeme ni ufisadi wa Escrow, lakini sina hakika kama Lowassa alihusika nao kiasi gani. Huyo mpambana na mafisadi mnayemwimbia mapambia ameshatangaza hadharani kuwa mafisadi wengine hatawagusa kwa sababu akiwagusa moto utakaowaka hataweza kuuzima.Hii ndiyo maana ya kuogopa kufukua makaburi kwa hofu ya kushindwa kuyafukia.

Magufuli ambaye mlimshabikia kwani yeye hakuwa sehemu ya mfumo huo wa kifisadi?
Mtu alikuwa ndani ya mfumo, na bado yumo humo. Si yeye na ninyi mlituaminisha kuwa ataubadili mfumo? Sasa ndio keshaanza kuugwaya mfumo sasa. Mwisho wake ni upi?
 
Lowasa ni Wakati wako sasa kutueleza uliyoyafanya ndani ya siku365za uongozi wa JPMna safari yako ya siasa kuelekea2020
 
Mkuu, pamoja na kwamba hata mimi sina chama kama wewe, lakini kitendo cha watu kuendelea kumsema Lowasa sio tu kwamba kinaendelea kumpa hadhi ambayo huenda hana, lakini kinasababisha watu wasiokuwa na mlengo wa kisiasa kama mimi na wewe tubaki kujiuliza kuwa huyu mtu ana nini hadi asakamwe hivyo, mpona kuna watu wegi sana wameondoka kwenye vyama vyao lakini kwa kuwa hawatajwi, wameiha sahaaulika ? Huyu mtu kaondoka na nini hadi afuatwe fuatwe hivyo ?
 
kuhusu umeme mwulizeni huyo richrd monduli
 
bado sijakuelewa na hayo mapenzi yako katika ukweli,hivi ajenda na kile kinachofanywa na ccm ni sawa ninia ya dhati ya ccm kupambana na huo ufisadi,how many cases ziko mahakamani zinazo husu ufisadi??sasa hawa wanao simamia ajenda ya ufisadi si ndio wenye makali kwanini wasikifute hiki chama cha mafisadi na huyo fisadi mkuu afikishwe mahakamni kujibu mashitaka yake...!! umeandika hii post kumfurahisha nani?? kwanini tusiwe na aibu hata kidogo basi..!!
 
Mpaka hapo Lowassa akipelekwa mahakamani ndipo nitaamini kwamba alikuwa fisadi la sivyo, nitaendelea kuamini ufisadi ni mfumo ndani ya CCM.
 
kuhusu umeme mwulizeni huyo richrd monduli
Wewe bado uko na Richmnd tu? Umesahau kesi ambayo TANESCO imeshindwa majuzi ni ya ESCROW na wahusika ndio hao wanaongoza Wizara ya Nishati kama zamani tu? Hilo deni ndilo linatutafuna sasa. Tunatakiwa tulilipe. Waliokula hiyo pesa tunayotakiwa kulipa wanajulikana lakini mzee wa boma amesema ni hatari sana kuwadai hao watu.
 
CHADEMA walikuwa na haki ya kupambana na ufisadi na kuupigia kerere kwa kipindi kile kwa sababu kulikuwa hakuna chama kingine cha kupambana na ufisadi kwa kipindi kile.

Sasa CCM waliokuwa wanaukumbatia ufisadi kwa kipindi kile,wameitambua kazi nzuri iliyokuwa inafanywa na CHADEMA,kazi ambayo CHADEMA walikuwa wanataka CCM wafanye kwa kuwa ndio walikuwa madarakani.

Baada ya kupata madaraka kwa mara nyingine,CCM wameupokea ushauri wa CHADEMA wameamua kupambana na ufisadi wa kwao wenyewe kwa kuwa wao ndio waasisi wa ufisadi huo.

CHADEMA wataendelea kupambana na ufisadi vipi wakati mwenye ufisadi ameamua kupambana nao mwenyewe chini ya Magufuli,wakati matatizo ya nchi siyo ufisadi tu,kuna matatizo mengi ambayo CHADEMA wamehamia kuyapigia kerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…