Kiu ya Mikutano ya Hadhara yawakumba Wananchi. John Mnyika azuiliwa Tunduma akielekea Rukwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,428
Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika angali kwenye ziara ya Kusimamia usajili wa kisasa wa wanachama (CHADEMA DIGITAL) ambapo leo ni zamu ya Mkoa wa Rukwa, huko Kalambo.

Hata hivyo alipofika Tunduma (ambayo ni nchi ya Chadema), amepigwa Stop na wananchi ambao wameziba kabisa njia na Kumlazimisha Mnyika atoe neno. Nisingependa kuwachosha sana , BALI NILICHOGUNDUA NI KWAMBA WANANCHI WANA KIU YA MIKUTANO YA HADHARA .

Hata hivyo, napenda kuwatoa wasiwasi Wananchi wote wa Tanzania, wavute tu subra, Novemba siyo mbali.

Nakala : Lukas mwashambwa
 
Mama twende Naye taratibu..,atatupa kila tunachoitaji.., tatizo tunakuwa mtaka yote kwa pupa

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Sidhani kama unajua hata maana ya mtaka yote kwa pupa. Je hapa unawaongelea wale walionyimwa yote hawana kitu au wale waliojimilikisha yote na kuzihodhi hadi kuvimbiwa!

Eti wale wenye njaa waende taratibu na mlafi anayekomba kila kitu, are you serious? Halafu sijui ni kwa ujinga au ni kwa unafiki, msemo...mtaka yote kwa pupa umeingiaje hapa?

Halafu huyo mama unayemtaja ni yupi? Ni huyu huyu aliyekuwa msaidizi mkuu wa Magufuli au mwingine? Je si huyu anayewataka aliowateua wale kwa urefu wa kamba zao na kazi iendelee?

Hebu ndugu yangu niambie, mtanzania anayekamuliwa kodi na tozo bila huruma, kamba yake ina urefu gani? Kwa kweli kuna kitu hakiko sawa vichwani mwetu Watanzania!
 
..katiba inamlazimisha Maza atende haki.

..na katiba haisemi sisi hatuna haki, na Maza na chama chake ndio pekee wenye haki.
Haki kwa wote na sio chadema tu wakaifanya ni ya kwao tu na kulazimisha ionekane ni wao tu wenye haki hata CCM na vyama vingine zaidi ya 13 vina haki pia hata wasio na vyama Wana haki pia
 
Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika angali kwenye ziara ya Kusimamia usajili wa kisasa wa wanachama (CHADEMA DIGITAL) ambapo leo ni zamu ya Mkoa wa Rukwa, huko Kalambo...
Nawaonya CDM kutotumia neno NCHI ya CHADEMA (Tunduma) au Nchi ya mbeya, mnapojaribu kuonyesha umma kukubalika maeneo hayo,

Jambo hili halina AFYA ktk TAIFA.

Tumieni neno NGOME ya CDM kama mnamaanisha kukubalika maeneo hayo.

Mnapoaminiwa na Watanzania, Epukeni Makosa ya kitoto namna hii.

Nchi ni moja TANZANIA baaaas!!!

Ameeen.
 
Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika angali kwenye ziara ya Kusimamia usajili wa kisasa wa wanachama (CHADEMA DIGITAL) ambapo leo ni zamu ya Mkoa wa Rukwa, huko Kalambo...
Laa!
Unampa nakala nani huyo!

Wahimizeni wanachama wenu ndio walio na uwezo wa kuruhusu hiyo mikutano ifanyike au la.

It's as simple as that.

Wakisema wanataka mikutano, hakuna mwenye uwezo wa kuizuia hiyo mikutano isifanyike.
 
Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika angali kwenye ziara ya Kusimamia usajili wa kisasa wa wanachama (CHADEMA DIGITAL) ambapo leo ni zamu ya Mkoa wa Rukwa, huko Kalambo.

Hata hivyo alipofika Tunduma (ambayo ni nchi ya Chadema), amepigwa Stop na wananchi ambao wameziba kabisa njia na Kumlazimisha Mnyika atoe neno. Nisingependa kuwachosha sana , BALI NILICHOGUNDUA NI KWAMBA WANANCHI WANA KIU YA MIKUTANO YA HADHARA .

Hata hivyo, napenda kuwatoa wasiwasi Wananchi wote wa Tanzania, wavute tu subra, Novemba siyo mbali.

Nakala : Lukas mwashambwa

Tuoneshe video/pictures ili tukuamini.
 
Back
Top Bottom