Kitwanga: Serikali haifichi mkataba wa Lugumi

Kitwanga: Serikali haifichi mkataba wa Lugumi

Kinachoshangaza ni kutaka kuanza kuongelea suala la Lugumi ndani ya bunge wakati kuna Kamati ndogo inafanya kazi mpaka sasa ya kuchunguza ili ilete taarifa bungeni mwishoni mwa mwezi huu na katika taarifa hiyo, bunge liweze kujadili na kutoa mapendekezo kwa serikali.

Maadam Kamati Ndogo imeundwa ili ifanye uchunguzi, lazima suala hili litajadiliwa bungeni.

Mimi ninachokiona ni siasa tu za kutafuta mass populality kwa wananchi wasiofahamu taratibu na kanuni za bunge.

Kama ni kutaka kuanza kujadili suala la Lugumi kwa sasa bungeni, basi kulikuwa hakuna maana yoyote ya kuunda kamati ndogo ili ikafanye uchunguzi kwenye vituo vyote vya polisi na kuangalia nyaraka mbali mbali.

Hoja ya Lema ingesubiri Kamati Ndogo ilete findings zake mbele ya bunge na ninaamini kwa uzoefu wake bungeni anafahamu hivyo.
Mbona wazir hajasubr kamati ndogo na kaongelea swala la lugumi bungeni bila kupingwa. So unamaanisha wapinzani hwana haki ya kuongelea hili swala mpaka wasubir kamat ila CCM 2 ndyo wanauhuru wa kuliongelea?
 
Haya ni majibu mazuri kutyoka kwa waziri makini...baadhi yetu humu tumekuwa tukisema kuwa upinzani upo kwa matukio, yaani ajenda zao ni matukio...hivi ni nani anayeweza kuficha suala la LUGUMI? watu wazima na akili zao wanazungumza kwa kufuata magazeti...magazeti yenyewe yamejaa waandishi wa habari wengi wakiwa hawana weledi kabisa, hawajui kuchambua issues...wao habari ni personalization of issues, hawajui kuchambua ndani ya habari kuna nini...waandishi wa habari na wahariri wao wamekalia kuchambua watu, mara Lema asema hivi, mara Mahiga asema vile, mara Mbowe, mara Tundu Lissu msomi wa sheria , mara kafulila, mara Mawazo na kadhalika...vyombo vyetu vya habari vimekaa kuchambua watu, vimekazania kuandika mambo ya 'bunge live' na havichambui taifa linaathirika au litanufaika vipi kwa kutokuwa na 'bunge live'...waandishi wa habari wana njaa, vyombo vyao haviwalipi mishahara mizuri , baadhi yao wanafanya kazi miaka 10 wakiwa freelancers hawana maslahi mazuri wala bima ya afya wala nssf au mifuko mingine ya jamii wanafanyishwa kazi kama watumwa lakini hawaandiki madudu ndani ya taasisi zao...wamekazania lugumi na sijui nini lakini madudu ya kutisha ndani ya vyombo vya habari hawaandiki...
Leo mmeamua kushambulia waandishi wa hbar kisa kila gazet limepost hotuba ya lema! Unafiki huu fisiem utawaua. Juzi hpa mlikuwa mnashabikia magzet yanavyosifia tumbuatumbua ya Magu. Leo hii mnayaponda. Hata hmtumii logic. Kama vip magazet yote yafungwe kama vigezo ulivyosema vyote ni kweli.
 
Hizi ndo akili za ndondocha wa Tanzania! Kwa kweli bado tuna safari ndefu, natamani mataifa yangekuwa yanaruhusiwa kupiga taifa moja na kuliteka, tungepigwa na wakenya na wakatutawala tu maana akili za wengi hapa kwetu ni za kimsukulemsule hivi! Kulikuwa na ubaya gani kuisikiliza hotuba ya Lema na mwisho kwenye majumuisho ukasema swala la kambi ya upinzani linafanyiwa kazi na kamati! Tuache ujinga, upumbav na ulofa!
Hotuba wameisoma though haikusomwa bungeni lakini chakushangaza wanatafuta kila mbinu kuijibu. wanajibuje mada ambayo haikuletwa bungeni???????? Kumbe msumar wa moto uliwaingia. Wanasema fimbo ya mbali haihui nyoka lakini hii fimbo ya mbali ya lema imewakata mikia.
 
Niulize Swali Hivi Watanzania Hatuwaamini Wabunge wetu waliyoko Mjengoni wanatimiza Wajibu wao wa kuongea na Kufuata Kanuni zao za kuendesha Vikao vyao Mpaka Tuwaone?Nina Imani Mbunge uliyomchagua anatimiza Wajibu wake.Sisi tushugulike na Kazi zetu za kujenga Nchi Na wao wako Mjengoni wanafanya kazi kwa Mujibu wa Katiba na Kanuni zao.Pindi wanaporudi Majimboni Watupe Mrejesho sio Wabaki Dar na Dodoma warudi kwetu Majimboni ambako kuna Changamoto Kibao Zinawasubiri.
Hiv wewe unajua hta kazi ya mbunge na bunge ni nini? Hau hta elimu ya uraia hauna?
 
Haya ni majibu mazuri kutyoka kwa waziri makini...baadhi yetu humu tumekuwa tukisema kuwa upinzani upo kwa matukio, yaani ajenda zao ni matukio...hivi ni nani anayeweza kuficha suala la LUGUMI? watu wazima na akili zao wanazungumza kwa kufuata magazeti...magazeti yenyewe yamejaa waandishi wa habari wengi wakiwa hawana weledi kabisa, hawajui kuchambua issues...wao habari ni personalization of issues, hawajui kuchambua ndani ya habari kuna nini...waandishi wa habari na wahariri wao wamekalia kuchambua watu, mara Lema asema hivi, mara Mahiga asema vile, mara Mbowe, mara Tundu Lissu msomi wa sheria , mara kafulila, mara Mawazo na kadhalika...vyombo vyetu vya habari vimekaa kuchambua watu, vimekazania kuandika mambo ya 'bunge live' na havichambui taifa linaathirika au litanufaika vipi kwa kutokuwa na 'bunge live'...waandishi wa habari wana njaa, vyombo vyao haviwalipi mishahara mizuri , baadhi yao wanafanya kazi miaka 10 wakiwa freelancers hawana maslahi mazuri wala bima ya afya wala nssf au mifuko mingine ya jamii wanafanyishwa kazi kama watumwa lakini hawaandiki madudu ndani ya taasisi zao...wamekazania lugumi na sijui nini lakini madudu ya kutisha ndani ya vyombo vya habari hawaandiki...
Mwenzetu unalipwa milioni ngapi huko uliko kiasi cha kuwadhalilisha hapa waandishi wa habari na kuwaambia wana njaa? Unapingana na Rais anayetaka watu walipwe mishahara kiduchu?
 
Niulize Swali Hivi Watanzania Hatuwaamini Wabunge wetu waliyoko Mjengoni wanatimiza Wajibu wao wa kuongea na Kufuata Kanuni zao za kuendesha Vikao vyao Mpaka Tuwaone?Nina Imani Mbunge uliyomchagua anatimiza Wajibu wake.Sisi tushugulike na Kazi zetu za kujenga Nchi Na wao wako Mjengoni wanafanya kazi kwa Mujibu wa Katiba na Kanuni zao.Pindi wanaporudi Majimboni Watupe Mrejesho sio Wabaki Dar na Dodoma warudi kwetu Majimboni ambako kuna Changamoto Kibao Zinawasubiri.
Uko jimbo gani?
 
Huyo anayevilaumu vyombo vya habari huenda hajui kuwa ni mhimili wa nne wa dola wenye jukumu la kuhabarisha, kuelimisha na majukumu mengine yanayofanana nayo? Ungeijuaje lugumi, epa, rscrow, meremeta na kashfa nyingine nyingi kama huyo anayeviponda vyombo vya habari hakusoma magazetini?
Kubalini tu kuwa ccm na serikali yake inatumia nguvu kubwa kuulinda uovu, wizi na udhalimu wao kwa wananchi. Hawapo kuwaongoza wananchi kwenye maendeleo. Najua wengi na puppets wao humu jf watatokwa na mapovu ya rangi kupinga hili ila ukweli unakwenda kusimama kuwa ccm ni ukoo wa panya usiohesabu machungu ya mwenye ghala.
 
Hivi huyu waziri anaijelewa kweli ...seriously?
 
lema ni kanjanja hodari wa kuzusha tafrani. upinzani wa aina ya lema hausaidii lolote. waziri kivuli gani kama sio mwenyewe ni kivuli. kila hituba yake imejaa ukakasi na kukashifu anadhani ndio upinzani.
 
Hii nchi imejaa viazi kweli, yan mtu mzima na akili yako unategemea Mwema na vikund vyake vyote vya upigaji amejiuzia tenda kweny jesh halafu hiyo taarifa source iwe ni wapi? kwenye vitabu, wizarani, au kwenye maktaba ya Taifa, lazima source ya hizo taarifa zinayepenyea kwenye social networks, magazet na kuendelea. karibu mambo yote yalioangusha wabadhirifu yalianzia huko.

Yan kwel, kuna kiongoz aliwahi kumwambia kiongozi mwenzake kuwa kuwa anaongoza maiti, naona inaweza kuwa kweli, yan skendo karibu zote watu walizowahi kupiga, ukiingia kwenye social networks watu wa ccm ni kuwatetea, tena kwa nguvu kabisa. Hii ni laana.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema serikali haifichi mkataba wowote ukiwamo wa Lugumi Enterprises, isipokuwa wabunge wanapaswa kufuata taratibu ili kuona mikataba hiyo kama kanuni zinavyowaelekeza.

Kitwanga alisema hayo juzi usiku bungeni wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa hotuba yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17. Kuliibuka mjadala mzito kuhusu masuala ya mikataba ukiwamo wa Lugumi na Jeshi la Polisi, kiasi cha kuwa moja ya sababu za wabunge wa upinzani kukataa kusoma maoni yao kuhusu hotuba hiyo ya Waziri Kitwanga.

Kitwanga alipojibu hoja za wabunge, alisema hakuna anayeficha mikataba yoyote katika wizara hiyo kwani hata hiyo mikataba inayozungumzwa aliiwasilisha katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alipotakiwa kufanya hivyo.

“Hata huu mkataba wa Lugumi unaweza kuonwa na mbunge yeyote ila kuna taratibu zake. Pia wabunge msisahau haya ni masuala ya usalama, yanaiweka nchi katika hali ya utata,” alisema Kitwanga. Aliendelea, “Mkataba upo na uko wazi, lakini hizi kelele za magazeti zinaiweka nchi katika hatari.

Hakuna anayeficha kitu, lakini tufuate taratibu zilizowekwa. Tunapiga kelele sana. Tunalo (wabunge) jukumu la kulinda usalama. Tufuate taratibu zilizo sahihi kuomba taarifa tunazohitaji.” Kitwanga alisema amesikitishwa na maneno yaliyowekwa katika maoni ya Kambi ya Upinzani ambayo yalitakiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya kusomwa bungeni juzi asubuhi.

“Baada ya kusoma bajeti mbadala nimesikitika sana. Bila CCM nchi hii haina serikali mbadala. Yaani hotuba nzima imejaa rejea ya magazeti. Kambi ya Upinzani iliyopo ni kambi ya upingaji,” alisema Waziri Kitwanga.

Alisema badala ya wapinzani kujikita katika rejea ya magazeti na maneno ya kusikia, alitarajia waseme kile wanachowaza wao. “Niko serikalini kwa miaka 35 sasa. Natambulika kama Mr STK, Mzee wa STK – Sheria, Taratibu na Kanuni.

Nimewasilisha fomu yangu Sekretarieti ya Maadili kwa mara ya kwanza mwaka 1998. “Hivyo vinatosha kuwapa taarifa mimi ni mtu wa aina gani, sipendi kusema, napenda kutenda,” alisema Kitwanga ambaye ni Mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza.

Akijibu hoja nyingine, alisema uhakiki wa madeni ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) unaendelea. Alisema zipo taasisi tatu za umma; Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) zinafanyia kazi masuala mbalimbali ndani ya Nida.

Alisema Sh bilioni 50 zipo Hazina na ziko tayari kulipa wafanyakazi ambao waliamuriwa kuachishwa kazi. Hata hivyo alisema, hilo litafanyika kwa uhakiki ili kutolipa wafanyakazi hewa.

Alikiri kuwa askari hawana makazi mazuri na bado maslahi yao ni ya kiwango cha chini. Alisema serikali inayafanyia kazi ikiwamo ujenzi wa nyumba za kuishi pamoja na kuongeza mishahara yao.

Akijibu hoja za wabunge kuhusu kuongezwa fedha kwa Nida ili ikamilishe kazi zake mwishoni mwa mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, alisema fedha zilizotengwa kwa mamlaka hiyo katika bajeti zinatolewa ili kazi zifanyike.
Conflict of interest
 
Sukari iliyopo kwenye maghala makuuuuubwa tumeambiwa imefichwa, lakini mkataba wa Lugumi ambao hata wawakilishi wetu kupitia kamati ya bunge hawajaonyeshwa tunaambiwa haujafichwa!!! Only in Tanzania.

Ifike wakati Magufuli aanze kutumbua hata aliowaweka yeye na wasukuma wenzie haya mambo ya ukabila yatamgharimu huko mbeleni

Namalizia kwa maneno ya Saidi Lugumi kuwa sio kila jipu ni la kutumbuliwa na watanzania tuachane na hii habari ya Lugumi kama tulivyoachana na Kagoda, Richmond, Dowans, Escrow, Meremeta, Kivuko cha Bagamoyo nk. Sasa Kazi Tu

Sasa wewe unatutafuta uchokozi tukijua sehemu ulipo tunakuletea gari la washa washa mambo ya mkataba wa Ligumi haukuhusu mambo ya kutuchokonoa chokonoa wakati tumepumzika tunakula mema ya nchi hatutaki.
 
Kinachoshangaza ni kutaka kuanza kuongelea suala la Lugumi ndani ya bunge wakati kuna Kamati ndogo inafanya kazi mpaka sasa ya kuchunguza ili ilete taarifa bungeni mwishoni mwa mwezi huu na katika taarifa hiyo, bunge liweze kujadili na kutoa mapendekezo kwa serikali.

Maadam Kamati Ndogo imeundwa ili ifanye uchunguzi, lazima suala hili litajadiliwa bungeni.

Mimi ninachokiona ni siasa tu za kutafuta mass populality kwa wananchi wasiofahamu taratibu na kanuni za bunge.

Kama ni kutaka kuanza kujadili suala la Lugumi kwa sasa bungeni, basi kulikuwa hakuna maana yoyote ya kuunda kamati ndogo ili ikafanye uchunguzi kwenye vituo vyote vya polisi na kuangalia nyaraka mbali mbali.

Hoja ya Lema ingesubiri Kamati Ndogo ilete findings zake mbele ya bunge na ninaamini kwa uzoefu wake bungeni anafahamu hivyo.
Hivyo conflict of interest naiona peke yangu?
 
Niulize Swali Hivi Watanzania Hatuwaamini Wabunge wetu waliyoko Mjengoni wanatimiza Wajibu wao wa kuongea na Kufuata Kanuni zao za kuendesha Vikao vyao Mpaka Tuwaone?Nina Imani Mbunge uliyomchagua anatimiza Wajibu wake.Sisi tushugulike na Kazi zetu za kujenga Nchi Na wao wako Mjengoni wanafanya kazi kwa Mujibu wa Katiba na Kanuni zao.Pindi wanaporudi Majimboni Watupe Mrejesho sio Wabaki Dar na Dodoma warudi kwetu Majimboni ambako kuna Changamoto Kibao Zinawasubiri.
Well said Mkuu
 
Kinachoshangaza ni kutaka kuanza kuongelea suala la Lugumi ndani ya bunge wakati kuna Kamati ndogo inafanya kazi mpaka sasa ya kuchunguza ili ilete taarifa bungeni mwishoni mwa mwezi huu na katika taarifa hiyo, bunge liweze kujadili na kutoa mapendekezo kwa serikali.

Maadam Kamati Ndogo imeundwa ili ifanye uchunguzi, lazima suala hili litajadiliwa bungeni.

Mimi ninachokiona ni siasa tu za kutafuta mass populality kwa wananchi wasiofahamu taratibu na kanuni za bunge.

Kama ni kutaka kuanza kujadili suala la Lugumi kwa sasa bungeni, basi kulikuwa hakuna maana yoyote ya kuunda kamati ndogo ili ikafanye uchunguzi kwenye vituo vyote vya polisi na kuangalia nyaraka mbali mbali.

Kwa nini wamekubali kuunda Kamati ndogo inayotumia pesa za walipa kodi kama posho za safari wakati suala zima wanalifahamu!

Hoja ya Lema ingesubiri Kamati Ndogo ilete findings zake mbele ya bunge na ninaamini kwa uzoefu wake bungeni anafahamu hivyo.
Kamati za bunge hili zilivyosukwa ni tofauti na bunge la awamu iliopita, usitegemee kitu hapo. Walioko kule mjengoni wameshaliona hilo.
 
Hawa wanaotetea lugumi leo ndio wale wale waliotetea swala la Richmond. Ila baada ya mkashifiwa mkuu wa scandal ya Richmond kuhamia CDM mada ikabadlika kuwa Lowasa fisadi lakini mkataba wa Richmond upo sawa kisheria.
 
Kwani yeye kitwanga huwa anayajua mambo yanayohusiana na nchi kutoka wapi kama sio radio, tv na magazeti!?
wanaofuatilia Panama papers si zilianzia magazetini au magazeti ya ulaya ni tofauti na ya kwetu!
 
DO NOT EXPECT TOO MUCH FROM THEM...CCM HAS NEVER BETRAYED THERE NEW IDEOLOGY AFTER NYERERE'S DEATH...THEY EMBRACE EMBEZZLEMENT OF PUBLIC RESOURCES IS THERE CALIBRATE...
 
Back
Top Bottom