Bani Israel
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 2,144
- 4,290
Kituo cha Buza Kanisani hiki kilijengwa kwa nia nzuri ila tamaa za mapato na kukosa utu zinageuka kuwa mateso kwa abiria.
Tarehe 18/2/2026 kama ilivyo mwaka jana viongozi wa eneo hili wakitumia askari wa jiji wamenza tena kulazimisha daladala kuishia hapa kwenye hili kituo hii inatokana na kuwa kituo hiki kilichojengwa kama soko kutokuvutia Wafanyabiashara.
Kwa sasa sheria waliyokuja nayo ya dereva wa daladala wachague kuingia kituoni mara mbili ikiwa wanataka kufika buza kanisani.
Hali hii imefanya daladala zilizokuwa zinafika Kituo cha Buza Kanisani kuamua kuishia hapa kwa mama kibonge.
Kituo cha Mama Kibonge kipo nje ya njia mbali na njia kuu pia sio kituo cha mwisho wa safari hali iliyofanya daladala kusumbua kuingia kituoni humo hadi ilipokuwa kwa lazima hata kama huna abiria wakushusha ama kupakia.
Kuanza tarehe 18/2/ 2026 daladala zinaishia Kituo cha Mama Kibonge abiria wa Buza Kanisani na maeneo mengine wanalazimika kutafuta usafiri mbadala wa kufika kituoni hapo ama kutembea kwa miguu.
Tarehe 19/2 hali imekuwa mwiba tena daladala chache zinazoamua kufika Buza Kanisani kwenda Mjini zimepandisha nauli toka Sh 600 hadi 1,000.
Bajaji zilizokuwa zaenda Tandika kwa Sh 500, leo zimepandisha nauli hadi 1,000.
Tukumbuke Buza Kanisani kuna kituo rasmi maeneo ya Savoy ambacho wamekitelekeza na kuja kukazana na kwa Mama Kibonge hali hii sio sawa kwa wananchi.
Maisha ni magumu mambo ya kuongezeana tena ugumu hawa viongozi wanawaza kitu gani? Wanataka kuchangamsha kituo ili mapato ya kukodisha frame yajae bila kujali eneo la stand ilipo wapi bila kujali ugumu watakaowapa wananchi.
Inasikitisha sana.
Halmashauri imefanya mabadiliko ya Vituo vya Daladala ambayo kwa asilimia kubwa yanatuathiri sisi Wananchi wa kawaida ambao ndio watumiaji wa usafiri wa Daladala uliolengwa.
Kituo cha Daladala cha Buza Kanisani kimekuwa kikitumika kwa zaidi ya miaka 30, Wananchi wamekizoea na ndicho ambacho kipo karibu na Wakazi wengi wa Buza, magari yote yanyotoka sehemu tofauti yanafika Kituo cha Buza Kanisani lakini Halmashauri imebadili direction, na sasa magari hayo ya abiria yameelekezwa kuishia Kituo cha Njiapanda ya Kitunda.
Kutoka Buza Kanisani hadi Kituo cha Njiapanda ya Kitunda kuna umbali mrefu kiasi na imekuwa shida kwa Wananchi wanaotumia Kituo cha Buza Kanisani.
Taarifa iliyopo ni kuwa kituo ambacho mabwana wakubwa wametaka kitumike kilijengwa kwa ajili ya kuwa stendi ya Mkoa lakini Waziri Mkuu aliyepita Kassim Majaliwa alikikataa akasema ni kidogo na hakina sifa ya kuwa Stendi Kuu ya Mkoa.
Hivyo, kwa kuwa eneo hilo kuna fremu ambazo zimedoda kwa muda mrefu, wameamua kutumia nguvu ili daladala ziishie hapo na waweze kupata wateja.
Juzi Wananchi waliandamana Polisi wakawapiga mabomu.
Kinachoendelea ni kuwa gharama za usafiri zimeongezeka kwa kuwa ukiwa unatoka mjini unalazimika kuchukua usafiri mwingine kutoka Njiapanda kwenda Buza Kanisani nak ama unatokea Buza Kanisani unalazimika kutumia usafiri mwingine kufika kituo cha Njiapanda.
Pia soma:
~ Maandamano ya Wananchi wa Buza - Dar es Salaam "Tumechoka tunamhitaji mkuu wa mkoa aje tunateseka"
~ TAKUKURU: Tunafanya uchunguzi Kituo cha Buza Kanisani kuhamishwa, tunashauri kwa sasa utaratibu wa zamani urejee

=====================================