Kituo cha sheria na haki za binaadamu Tanzania(LHRC) imesikia simulizi ya Dada alienyanyasika

Nahonyo

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
5,499
5,287
Ni wiki ya pili sasa Dada mmoja, anasimulia jinsi alivonyanyasika kutuo cha radio 5 ya jijini Arusha, cha kusikitisha wananyanyasha ni ndugu zake, hasa mjomba wake. Mjomba amefikia hatua ya kum baka tena anafanyia kinyume na maumbile,
Naomba kama kituo hiki kama kina tawi Arusha, wamfuatilie msichana huyu kupitia radio tajwa hapo juu, ili kumpata msichana huyo habari zote anazo. Maana simulizi ni ndefu ni ngumu kuandika yote hapa, kama kuna mtu amemsikia msichana huyu anaesimulia habari hizi kupitia kipindi chao chenye jina la mikasa ya maisha bila shaka ataungana nami. LHRC, mnaonekana mko kimya pindi mtu mmoja mmoja anapokosa haki yake, ni juzi juzi tu kituo cha TV ch 10, walionyesha msichana alieunguzwa vibaya kwa kuchomwa na pasi, yenye moto sehemu nyingi za mwili wake. Na kudumbukizwa kwenye karo la maji machafu na kumfunika na mfuniko wa karo, alie fanya unyama huo ni mdai wa bosi wake, maana alikua Dada wa kazi pale. Yote kwa yote sijasikia hata tamko kutoka kwa kituo hiki cha haki na sheria, hata kikilaani tukio hili, au hamfuatilii kinachoendelea kwenye vyombo vya habari?
 
LHRC hawafanyi kazi kwa shinikizo au mihemko mkuu, hold on kama hizi taarifa ni za kweli basi hatua stahiki zitachukuliwa....
 
LHRC hawafanyi kazi kwa shinikizo au mihemko mkuu, hold on kama hizi taarifa ni za kweli basi hatua stahiki zitachukuliwa....
Sitaki ni hukumu kuwa wanafanya kazi kwa shinikizo, au mihemko, ila wanapaswa kuuwasaidia hata hawa wachhache wanajitokeza mbele ya hadhara na kujieleza, watu wengi yanapotufika hatujui pa kukimbilia.
 
huwa wanatoa matamko kwenye mambo kama ya siasa ili waonekane na kupata pesa za wafadhili wangekuwa wanafanya kazi japo kwa robo inavyotakiwa watu wengi wangekuwa wanapata haki zao
 
Back
Top Bottom