Kituo cha polisi Mirerani kinanuka rushwa! Kimulikwe!

Kituo cha polisi Mirerani kinanuka rushwa! Kimulikwe!

Last emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
10,346
Reaction score
9,892
Salaam wana JF!

Kama kuna kituo kinanuka rushwa na uchafu wa kila aina, ni kituo cha polisi cha Mirerani, watu wanafanya mambo ya kuhatarisha maisha ya watu lakini bado wakifikishwa kituoni hapo na wanaachiwa baada ya kutoa rushwa.

Mfano ni tukio la hivi karibuni kurudishiwa silaha mtu mmoja anaeitwa John Waitali, huyu bwana anajulikana kwa matumizi mabaya ya silaha, amekuwa akifyatulia watu risasi ovyo, miezi michache iliyopita huyu bwana alinyang'anywa bastola yake baada ya kumpiga risasi kwa makusudi jamaa anaeitwa Daud.

Lakini cha ajabu licha ya historia mbaya ya huyu bwana Waitali ya kupiga risasi ovyo sehemu yoyote akiwa amelewa au kupishana na mtu kauli, lakini bado amerudishiwa silaha, na juzi amesikika akiwatishia watu kuwa atawamwaga utumbo wanaomzengea demu wa mdogo wake na hakuna mtu atamfanya kitu, kwasababu yupo karibu na Gody mwalusamba ambae ni mpambe mkuu wa Rizwan. Hivyo hakuna wa kumfanya kitu kwasababu anaongea na watu wanaokanyaga red carpet ya ikulu.

Hii ni fact. Wahusika wachukue hatua, huyu mtu ni hatari na ana kesi zaidi ya tano za kuwatishia kuwauwa watu hapo kituoni, lakini cha ajabu amerudishiwa silaha tena. Hatua zisipochukuliwa, nina hakika ipo siku tutakuja toa taarifa ameuwa hapa.
 
Kwanini asirogwe!!!!!,kama kama haki imeshindwa kutendeka.
 
Siku hizi machalii wa Arusha wameacha kutembea na visu, bisibisi na mapanga ndani ya suruali zao? Ingekuwa ni enzi ile ya Apolo moto huyo ungekuta hana kichwa siku mingi pamoja na kabastola kake...Ila hii ni ishara tu ya watu wanaanza kustarabika taratibu wachache kama huyo bwana tu ndo wamebaki
 
Mkuu huyu jamaa na kabastola kake anatishia watu sana. Ajabu kwanini mtu amemwaga damu juzi tu na ana historia ya kutishia kuua hadi msukuma mkokoteni anarudishiwa bastola kabla hata mtu hajapona majeraha!
 
Mambo yote hapo ni pesa wao watapata wapi mawe kama si kwenu, maisha bora kwa kila mtanzania
 
Mkuu huyu jamaa na kabastola kake anatishia watu sana. Ajabu kwanini mtu amemwaga damu juzi tu na ana historia ya kutishia kuua hadi msukuma mkokoteni anarudishiwa bastola kabla hata mtu hajapona majeraha!
Na ndiyo maana watu wanaamua kuchukua sheria mikononi tu maana ukitegemea upate haki ndan ya hii nchi...Utakaa sana
 
Back
Top Bottom