Kituo cha mwendokasi Kimara, ni jehanamu ya abiria

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
654
Maelefu ya abiria wanaorundikana kituo cha mabasi ya mwendokasi Kimara mateso yake yanafanana moto wa jehanamu. Hakuna sababu yeyote ya maana ya kuwarundika abiria wote hapo zaidi ya kupigania nauli ya sh. 400 tu.

Abiria wote wanaochukuliwa Mbezi Luisi kwenda mjini hakuna hata mmoja ambae hua anahitaji kushuka Kimara lakini wote hushushushwa Kimara na baadae huanza kusombwa upya kwenda mjini. Na abiria wote wanaotoka mjini asilimia 90 mwisho wao hua Mbezi Luis lakini wote hushushwa Kimara na baada kufururika hapo kama nyuki ndo huanza kusombwa kwa mbinde kubwa kuwapeleka Mbezi Luis.

Lakini inawezekana kwa jinsi yeyote ile kuondoa msongongamano wa abiria kwa kuwasafirisha moja kwa moja kwenda mjini au moja kwa moja kwenda Mbezi Luis kwa kuchagua baadhi ya mabasi yanayokidhi vigezo vya njia hizo.Viongozi wote akiwemo Makonda hakuna hata mmoja ambae amepata UFUNUO WA TATIZO LA MSONGAMANO WA ABIRIA KIMARA MWISHO.

Lakini wahusika wanajua dawa yake ila hawawezi kuitoa kwa sababu wanapata faida kubwa ya sh 400 kwa ruti fupi tu. Sasa labda tusubiri Rais Magufuli aje kutegua kitendawili hiki cha mrundikano wa abiria usio wa kawaida hapo Kimara.
 
Abiria wote wanaochukuliwa Mbezi Luisi kwenda mjini hakuna hata mmoja ambae hua anahitaji kushuka Kimara lakini wote hushushushwa Kimara na baadae huanza kusombwa upya kwenda mjini. Na abiria wote wanaotoka mjini asilimia 90 mwisho wao hua Mbezi Luis lakini wote hushushwa Kimara na baada kufururika hapo kama nyuki ndo huanza kusombwa kwa mbinde kubwa kuwapeleka Mbezi Luis.

Kinachotuangamiza ni utengenezaji wa fursa kwa kulazimisha, hapakuwa na sababu ya msingi ya kushusha abiria wa Mbezi mwisho pale Kimara, kilichotakiwa ni kuwa na mabasi yanayotumia njia ya mwendokasi na njia ya kawaida kama yale ya Muhimbili ili yaanzie safari Mbezi mwisho mpaka mjini badala ya kuwatesa watu panda shuka ili kumaximize faida, ukitazama kwa makini kilichofanyika hapo ilikuwa kumnufaisha mtoa huduma wa Udart na siyo kuwasaidia wananchi, vinginevyo zingefunguliwa njia za ndani kama ile ya Mbezi mwisho kupitia Kingerezi hadi Tabata kwenda mjini zikawekewa miundombinu mizuri na mabasi mazuri shida ingepungua sana.
 
Kama unaona unaibiwa panda daladala ambako hauibiwi kila kitu kina mipango na mikakati
 
Back
Top Bottom