Kituo cha mabasi Makumbusho kinaharibiwa

Kituo cha mabasi Makumbusho kinaharibiwa

Rajabu Msechu

Member
Joined
Apr 13, 2016
Posts
35
Reaction score
18
Habari za asubuhi great thinkers wenzangu, natumaini kwa uwezo alitupatia mwenyezi Mungu hatujambo.

Nimeona ni jambo la mbolea kuleta uzi huu kwenye jukwaa hili hasa baada ya uchunguzi yakinifu nilioufanya kwenye kituo cha mabasi Makumbusho.

Wazungu wanakwambia, "No Research, No Right To Speak".

Ningependa kwenda kwenye kiini moja kwa moja, wakati kituo cha mabasi Mwenge kilipoamishwa kupisha upanuzi wa barabara na hatimaye kuhamishiwa Makumbusho, niliamini kwamba maboresho ya kituo kipya yangekuwa bora zaidi.

Hapo awali wakati kituo hiki cha Makumbusho kinaanza, uliwekwa utaratibu mzuri sana kama vile usafi, ulinzi, halikadhalika wapiga debe walipigwa marufuku. Lakini kadri muda ulipokuwa ukizidi kwenda ndipo mambo yakaanza kubadilika taratibu.

Nikianza na kero ya kwanza ya uwepo wa wapiga debe mateja, hawa watu kama wanavyojulikana kwenye jamii huwa hawana dhamana.

Hawa ndio chanzo cha uhalifu pale kituoni hasa kwa wasafiri kuibiwa mali zao kama vile, simu, mikoba na fedha.

Kama hiyo haitoshi hawa wapiga debe huwaleta wenzao ambao wao kazi yao ni kuchora ramani za kuwaibia watu ndani ya stand.

Ndio maana sasa hivi hali ya kiusalama kwa ujumla pale ndani sio ya kuridhisha ukilinganisha na hapo awali.

Kero nyingine ni ujenzi wa miundominu ya stand, tukianzia kwenye zile paving blocks walizoweka na barabara za vumbi za kuingia kituoni, ambapo ikinyesha mvua hugeuka kuwa dhahama pale hasa kwa matope kujaa.

Mwisho kabisa ningependa kutoa rai kwa wasafiri wanaotumia kituo cha Makumbusho kuwa makini sambamba na wahusika waliopewa jukumu kuhakikisha wanarekebisha dosari hizi.
 
Kero namba moja pale ni BARABARA za kuingilia pande zote...

Ngoja mvua zianze uone tope la pale, huwezi tembea kwa miguu..

Kero namba mbili pale ni DIMBWI la kuingilia mabasi ya Temeke, Buguruni, Mbagala, nk. Pale mvua zikianza magari na watembea kwa miguu hawawezi pita.

Kero namba 3 ni kujaa kwa wafanyabiashara ndogo kwenye maeneo ya kupumzikia abiria kusubiri daladala, kwa sasa hakuna nafasi hata ya kusimama.

Kero namba 4 ni uuzwaji wa chakula kwenye maeneo machafu na yasio rasmi, mfano lile geti la kutokea kuna viroba vimejaa pale vya uchafu, pembeni wanauza vyakula na juice.

Nanyi mtaendelea ......
 
Hizo njia za kuingia kituo ni mbaya sana

Unaweza kushangaa duh unapelekwa wapi huku
 
Kero kubwa kabisa ni ubovu wa kale kanjia ka kuingilia kituoni, kaboreshwe kwa kuwekwa lami. Hivi kubana kote matumizi huku tumeshindwa kabisa kupiga lami?!
 
Nimejuelewa Ndio Maana Ni Nimemjibu, Hebu Jitathmini Na Ww Labda Ndio Hujamuelewa
Sasa kama ukinunua gari yako na unamahitaji pale kituo au ndo unaishi maeneo yale.. ile kero ya barabara na wizi na msongamano unaikwepa vipi kama umeelewa mada..!???
 
Sasa kama ukinunua gari yako na unamahitaji pale kituo au ndo unaishi maeneo yale.. ile kero ya barabara na wizi na msongamano unaikwepa vipi kama umeelewa mada..!???
Kumbe Umenielewa Mkuu, Basi Tuache Hii Mada Tukajiandae Na Ukuta Tar 01
 
Nunueni Magari Yenu Mtumie, Kila Kitu Mnataka Mkosoe
Kwenye kila kitu nyie mnaona kiko sawa amtaki kukosolewa na mkishindwa kutekeleza amsemi mana kwenye kila thread unasema ivo ivo au ngozi zetu ndo tabia yetu
 
Kwenye kila kitu nyie mnaona kiko sawa amtaki kukosolewa na mkishindwa kutekeleza amsemi mana kwenye kila thread unasema ivo ivo au ngozi zetu ndo tabia yetu
Rangi ya mtu sio moyo wake.. kila kitu kwao sawa
 
Back
Top Bottom