Kituko/Majanga ilikuaje uliumbuka kwenye outing

Ujinga mtupu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2017
Posts
887
Reaction score
2,022
Nakumbuka mwaka jana nimetoka na Demu wangu out sasa sio mpenzi sana wa haya mambo ila nilifanya hivyo kumfurahisha.

Tukafika kahotel kamoja kako busy sana na kana wazungu wengi, kiukweli mimi hata sikuhitaji menyu nikaagiza wali na sato..na demu wangu naye akataka hivyo hivyo na juisi ya maembe. Kuja kuletewa bills imekuja Elfu 58.nilishtuka ghafla.

Yule mrembo wala ashtuki mfukoni na Elfu 24..kilichonikuta sitaki hata kukumbuka kikweli niliumbuka sana baada ya hapo.

Iliisha kistaarabu tu uzuri..nilikuja kusongesha voda kama 30 na demu wangu ikabidi nimkope hela kama elfu 10.
 
Siku nyingine inabidi ATM card hiwe imechangamka aiseeee.
 
Nahisi wazungu walikucheka sana... Vipi ulikutwa na nini kijana? Lakini kwenye vikao tulikwisha kuongelea haya mambo ya outings na wanawake bila kujihami na backup ya ku cover extra costs za nje ya budjet au ulidoji kikao?
 

Jinsi muhudumu alivyomuangalia jamaa yetu aliposikia ana 24k badala 58k anazohitaji[emoji23][emoji23][emoji23].

Hotel ukiishaikuta ina watasha,itisha juice kwanza ili upime kina cha maji,halafu jenga tabia ya kutimba peke yako sehemu kama hizo kwanza kabla upeleke mtoto wa mtu.
 
24000 watu wawili hata huku uswazi haitoshi,sijui uliwaza nini.hata ungekuwa na laki moja kanakuna wazungu bado upo kwenye risk ya kuosha vyombo
Uswazi ipi boss...

Kwa chipsi kuku za elfu 5 au kuns kingine una maanisha.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…