Kitu pekee kinachomfanya mwanamke asichepuke hiki hapa

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Dawa ni moja tu ndugu zangu, kua katika mahusiano na binti aliekuelewa, yanj anaekujali, sana.

haijalishi ana mapungufu kiasi gani, kama mwanamke kakuelewa huyo ndie mwanamke anaekufaa

Binafsi katika utafiti wangu nimejiridhisha kwa hili, wale mademu niliokua nikiwatongoza na kuwahonga wengi waliishia kucheat ama kuniacha ila wale ambao waliotia juhudi za kutoa ishara kwamba wananijali hawakuwahi kunichepuka nilipoitikia wito wao.

kwa bahati mbaya hawa ambao walinielewa nilikuwa nawaona hawana thamani, wengi niliwaacha nikiwaona wanajigonga kwangu na wachache waliniacha baada ya kushindwa kuvumilia navowanyanyasa.

Kuna baadhi wameolewa ila hadi Leo wananicheki sana kwenye simu, huwezi amino kuna Binti moja nilimwacha mara 3 ila alifanya jitihada zilizonishangaza kulifufua penzi kila napomwacha, nilimwacha moja kwa moja nilipogundua alikua kanifichia siri kaolewa, alikuwa ananipa hela akinidanganya kaajiriwa kumbe ni za bwana wake.

Unaweza ukawa mzibuaji mzuri sana wa sikio la chini lakini ukachepukwa, Unaweza kuwa na fedha nyingi sana ila binti akakuchepuka kwenda kupata pumziko kwa tulizo lake la moyo.

Ni hatari sana unapolazimisha penzi kwa hawa viumbe, na mbaya zaidi wana kipaji cha hali ya juu sana kukufanya udhani unapendwa kumbe unachepukwa vibaya mno.

Ni hayo tu, Penda mwanamke ambae kafa kaoza kwako.
 
SIJAONA HAPO SULUHISHO LA KUWAWEZA HAWA VIUMBE ZAIDI YA POROJO ZA SIKU ZOTE MKUU, HAWA VIUMBE HAWANA NJIA YA KUWAMUDU MAANA HAWAELEWEKI
 
Kichwa cha habari na vitu vyenye umeandika hakuna connection CORRECTION PLEASE!
 
Naona kichwa cha mada na uliyo andika ni vitu tofauti kabsa.. kijana acha mihadarati
 
Mbona sijaelewa meini pointi yani sijui niseme sijaelewa mkuu uzi wako
 
Dawa ni moja tu ndugu zangu, Hakikisha mwanamke anakuelewa kwa dhati wewe kama ulivyo, haijalishi ana mapungufu kiasi gani huyo ndie mwanamke anaekufaa, ila ndio hivyo tena watu wanapotezea hizi bahati nadra wanaenda kuhonga ma slay queen wajanja wa town na kila siku kuja humu kufungua post wamechepukwa.

Binafsi katika utafiti wangu nimejiridhisha kwa hili, wale mademu niliokua nikiwatongoza na kuwahonga wengi waliishia kucheat ama kuniacha ila wale ambao waliotia juhudi za kutoa ishara kwamba wananijali hawakuwahi kunichepuka,

kwa bahati mbaya hawa ambao walinielewa nilikuwa nawaona hawana thamani na mimi nikawa navimba kichwa kwamba hawawezi kuniacha hata nikifanya ufuska, wengi niliwaacha nikiwaona wanajigonga kwangu na wachache waliniacha baada ya kushindwa kuvumilia matukio baada ya matukio ya kuwacheat nikidhani ya kwamba naweza kuwanyanyasa navyotaka.

Ni hawa hawa ambao walifanya jitihada ya kurejesha upya mahusiano yaliyovunjika, kuna baadhi wameshaolewa ila wanapenda sana kuchat na mimi, nisingekua na msimamo wa kuheshimu ndoa za watu ingekuwa ni kitu rahisi tu kuchepuka nao kwasababu wananiependa kwa dhati.

Unaweza ukawa mzibuaji mzuri sana wa sikio la chini lakini ukachepukwa, Unaweza kuwa na fedha nyingi sana ila binti akakuchepuka kwenda kupata pumziko kwa tulizo lake la moyo.

Hawa wanawake sijui waliongeaga nini na mungu wakati tukiwa tumesinzia tunavyotolewa ubavu, hatujui waliongea nini cha ziada na shetani kabla hawajaja kutufikishia ujumbe wa shetani tulionje tunda, Ni hatari sana unapolazimisha penzi kwa mwanamke, na mbaya zaidi wana kipaji cha hali ya juu sana kukufanya udhani unapendwa kumbe unachepukwa vibaya mno.

Mwanamke ni kiumbe ambaye endapo HATAKUPENDA KWA MOYO WAKE KWA DHATI jiandae kushuhudia vimbwanga vingi sana, utasugua kama mbwa lakini atakuchepuka tu, utahonga pesa kibao lakini ataku cheat na msela aliechoka.


Hakikisha hutumii nguvu ,pesa na saundi nyingi sana kumfanya mwanamke akuelewe, kama mwanamke kakuelewa utajua tu
Umeongea points za ukweli ila ujumbe wako umeuficha; ndiyo maana watu wanashindwa kukuelewa zaidi.
Alafu mada umeifanya ndefu ila hakukuwa na ulazima.

Ke wanaotuelewa na kutupenda, sisi tunawaona hawana viwango tunavyotaka! Tunawaona ni wa kupiga na kusepa.
Na hao ndiyo wana upendo wa kweli. Na kuna bahati zingine zikikupita hazijirudii.
 
Kama mimi sababu itayonifanya nichepuke,,,,,,nipo double hila am single.....
 
Mwanamke akikuelewa- Umekwisha
Women prefer unpredictability to predictability.
 
SIJAONA HAPO SULUHISHO LA KUWAWEZA HAWA VIUMBE ZAIDI YA POROJO ZA SIKU ZOTE MKUU, HAWA VIUMBE HAWANA NJIA YA KUWAMUDU MAANA HAWAELEWEKI
Yaonekana una kichwa kizito point ya msingi ipo kwenye "kua na time wale wenye time na wewe yani penda pale unapopendwa"
 
Umechepukwa nini?! Mbona umeandika kama una mizuka sn hadi ulichoandika tofaut na kichwa cha habari!?
 
Back
Top Bottom