Kitu cha ziada(surplus) sio kwa ajili yetu,ni kwa ajili ya wahitaji

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
Surplus is not for you.

Tunapotafuta na kupata, huwa ni juhudi zetu lakini ukweli ni kuwa riziki inapangwa na Mungu.
Mungu anapotujalia ridhiki zetu za kila siku huwa anahakikisha zinakidhi mahitaji(necessaries).
Zisipokidhi mahitaji huwa kuna walakini kwa upande wa muhusika( may be unnecessaries ndio first priority).

Mungu anapotujaalia riziki huwa inakuja na ziada(surplus).
Lakini kutokana na kile nilichotafakari ni kuwa ziada huwa sio kwa ajili yetu bali ni kwa ajili ya wahitaji ( yatima, wajane,walemavu,masikini nk).
Huwa ninaamini kwenye saving(kuhifadhi) na kuhifadhi ni kwa ajili ya future na sio Kitu kibaya.
Je unaonaje pale unapohifadhi ziada(surplus) wakati jirani yako au ndugu yako ana uhitaji na hicho kitu uluchohifadhi?
Wangapi wanakufa na njaa huku sisi tukiwa tumehifadhi vyakula kwenye maghala au mafriji?
Wangapi wanakosa hela za matibabu huku sisi tukiwa tumehifadhi fedha nyingi kwenye mabenki?
Kwa nini tuhangaikie kesho wakati leo kuna watu wanauhitaji.

Na wengi wetu hutumia surplus(ziada) kwenye anasa na starehe, mfano ulevi, kuhonga,kufanya kufuru kama Zile za kipedeshee.
In fact ziada sio kwa ajili yetu kabisa,ziada ni kwa wahitaji thus why matabaka yapo kwenye jamii ili tusaidiane na hiyo ndio maana ya humanity.
Mambo ya walawi 23:22
 
Back
Top Bottom