kitovu kuwa kikubwa nini chanzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kitovu kuwa kikubwa nini chanzo

Discussion in 'JF Doctor' started by Mkwanga, Jan 19, 2012.

 1. Mkwanga

  Mkwanga Senior Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wanajamii naomba mwenye ufahamu juu ya hili mtoto kuzaliwa kitovu kikubwa inasababishwa na nini?je kuna utaalamu wa kuweza kkufanya kikapungua natumaini mtanisaidia.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mtoto hazaliwi na kitovu kikubwa, tatizo linakuwepo kwenye ukataji.

  Ila pia inategemea na umri, kama ni chini ya mwaka mmoja au hata miwili kinaweza kurudi ndani chenyewe taratibu, kisiporudi chenyewe anaweza akafanyiwa operation kidogo kurekebisha.
   
 3. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiyo inaitwa umbilical hernia, inasababishwa na misuli ya tumbo kulegea.
   
 4. n

  ngwana ongwa doi Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama alivyosema d.ya sikio huitwa umblical hernia,hernia hutokea wakati utumbo,maji,mafuta yanaposukuma na kuingia eneo lililo na tundu(hole) au sehemu ambayo kuna weakness ya muscles.Kwa watoto mara nyingi huzaliwa nayo hata hivyo haina maumivu kwa mtoto.

  Husababishwa na nini kwa watoto.

  Kwa kawaida kwenye kitovu huwa kuna umblical ring ambayo kawaida hufunga kwenye kitovu kabla ya mtoto kuzaliwa,kama ikitokea haikufunga tissue zinasukuma kuingia kwenye hilo tundu la kitovu na kufanya hernia.

  Kwa watoto wengine huanza kuonekana pindi kitovu kikikatika,lakini wengine huwa haionyeshi mpaka akiwa amekua.
  mara nyingi unaigundua hasa mtoto akichuchumaa,akisimama wima amenyooka,wakati akilia,kukohoa, sehemu ya kidovu inatuna(bulge).

  Matibabu yake.
  1.Hupona yenyewe bila matibabu katka kipindi cha mwaka 1.
  2.Kama mtoto akifikisha miaka 5 haijafunga tu njia ni kufanyiwa upasuaji mdogo kurekebisha hernia hiyo.
   
 5. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu kwa maelezo yako mazuri.
   
 6. d

  drberno Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa maelezo yako yaonesha hiyo yawezakuwa ni umbilical hernia(kama ambavyo wengine wametangulia kusema)!
  matibabu:
  1. kama tundu lake ni dogo chini ya sentimeta 4 linauwezekano wa kujifunga by the age of 4yrs!
  2. otherwise to the above statement..upasuaji unaweza kuhitajika
  3. ni bora ukaonane na dr ili aweze kumpima huyo mtoto na akupe ushauri sahihi zaidi baada ya hapo!
   
 7. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ahsante Mkuu,umetoa full class. Nimejifunza something new ( sababu+ mnx ya uh)
  ILA HAPO CHINI EDIT KIDOGO...
  NI MGANGA WA JADI SIO MIMI

  ...
   
 8. mudushi

  mudushi Senior Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Mwanangu alikuwa na tatizo hilo. alifanyiwa operation sasa fresh. Nenda hospital bana.

  Mudushi
   
 9. n

  ngwana ongwa doi Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  samahani mkuu ulikuwa akilini mwangu nilijua naandika mganga wa jadi kumbe nikaandika DAWA YA SIKIO tehe tehe,nashukuru sana.
   
 10. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  teh teh teh... Lol !
   
Loading...