Kitovu kuvuta wakati una mimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitovu kuvuta wakati una mimba

Discussion in 'JF Doctor' started by Evarm, Oct 18, 2012.

 1. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Salaam JF Doctors,

  Nina mimba ya miezi minne, jioni ya leo ninajisikia kitovu kuvuta sana kwa ndani na hii hali inaendelea hadi sasa. Ninaombeni msaada wenu kufahamu je hii hali ni kawaida au ni tatizo kwa mama mjamzito? Samahani nipo mbali sana na hospitali ningeweza kwenda kupima na kujua tatizo ni nini. Naombeni ushauri wenu nifanyeje haya maumivu yapungue. Riwa , MziziMkavu , hippocratessocrates na wengineo naombeni ushauri.
  Nawasilisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Dada Evarm Pole, nikupongeze kwa kujali ujauzito wako(kutoa taarifa/kuulizia ushauri mapema mara tu baada ya maumivu).


  Kama ni mimba ya pili na kuendelea(tunge/ningependa kujua) tofauti ya mimba hii na ile iliyopita, lakini kama ni mimba ya kwanza ni vizuri kutambua maumivu yanaelekea upande wowote? Je, yanapungua kutokana na mkao wowote? Je, ulijigonga tumboni eneo la kiunoni?
  Pamoja na maswali hayo ningependa kusema kuwa
  Maumivu eneo linalozunguka kitovu ni kitu cha kawaida(HASA mimba unapoanza kukua), ..hii ni kutokana na msukumo/mgandamizo(pressure) ya mtoto anapokuwa anapozidi kukua kwani ni katika kitovu ndipo mishipa hii ya damu inayotumika kumpatia mtoto aliye tumboni(tumbo la uzazi) virutubisho yaani(chakula, hewa, n.k).

  Hivyo maumivu yanaweza kuhisiwa mjamzito anapoinama, mimba inapozidi kukua na wakati fulani mtoto akiwa anacheza. Hata hivyo maumivu haya hupungua(huwa yanakuja na kupotea), ni vizuri kupumzika, kupunguza kufanya kazi nzito.

  Iwapo maumivu yatazidi, kutokupungua, n.k ni vyema kufika katika Kituo cha Afya(Kwa kuwa uko mbali na hospitali) kwa uchunguzi kwani pamoja na ujauzito maumivu ya tumbo(kitovuni) yanaweza kusababishwa na mambo mengine pia.
   
 3. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Asante sana hippocratessocrates,

  Ni mimba yangu ya kwanza, haya maumivu hunitokea zaidi nikiwa nataka kusimama (ninapokuwa nimelala ile nataka kuinuka nahsi kitovu kuvuta), muda mwingine nikijaribu kubeba ndoo ya maji nahsi kitovu kinavuta ingawa baada ya muda huacha.

  Sijajigonga na kitu chochote tumboni wala kiunoni.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. s

  sepuka Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole dada wahi tu kituo cha afya wakakufanyie uchunguzi zaidi nazani utajua tatizo.
   
 5. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Asante sepuka,
  nimeenda hospitali hamna tatizo lolote!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. korino

  korino JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 492
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  pole sana dada angu...hata me hlo tatizo ninalo! mimba miezi 7 kitovu kinavuta km ivo unavyosema ww nkitaka kuamka vile nkijivuta,nkifanya kazi zangu za nyumban! sasa naogopa hata kufagia rum kwangu! jana nliandika post kuomba msaada ila cjajibiwa nw ndo naona hii ya kwako! pole Mungu atatusaidia
   
Loading...