Amanikwenu
Senior Member
- Dec 1, 2009
- 187
- 0
- Thread starter
-
- #21
siungi mkono hoja kwa nini kupoteza muda na hela hizo bilioni ulizotaja itakuwa dowans nyingine kama sio kagoda kengine,kama ulifuatilia mjadala wa jmosi pale nkrumah kuna mchangiaji mmoja alisema serikali sio sikivu tutaandaa semina, warsha ,kongamano ,kigoda,mikutano,mbongi nk lakini hiyo yote haitasaidia ,cha msingi tunajua tunataka nini basi serikali ikileta ujanja ni kuandamana tu wacha wafyatue risasi tufe kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu,kilichotokea nkruma juzi kimeshasahulika zamani lakini kilichotokea arusha tarehe 5 january hakitasahulika kamwe kimeishaingia wenye kumbukumbu za dunia so solution na peples power,
nawasilisha
Naunga mkono hoja,ila vyombo binafsi vya habari ndio vipewe malipo ila TBC walirushe matangazo BURE!
Naunga mkono hoja vilevile iangaliwe njia ya kuproduce CD na DVD za kongamano hilo ili ziweze kusambazwa kwa wananchi wengi.Kwa njia hii wengi watapata uelewa na kushiriki kwenye mchakato kwa umakini zaidi.
ni hoja nzuri. na pia kwa jambo hili kama udasa mkiwa approach donors ni rahisi kupata fedha za kutosha kueneza elimu kwa watz
kila la kheri, mtakapo kuwa mnawazika watoto wa masikini ambao ndio huwa chambo mnapoandamana kama ilivyokuwa arusha, mimi nitakuwa home na watoto wangu tunaangalia cartoon ya wacky races, mkipata hicho mnachokitafuta kama kinafaida na mimi nitakuwa mstari wa mbele katika kufaidi.
siungi mkono, serikali itenge na kutumia rasilimali zetu, hakuna haja ya kuwabebesha mzigo wa tz wachache au labda serikali iwalipe hawa walimu kama konsaltants.
Naunga mkono hoja ila donors wawe watanzania mimi nikiwa mmoja wao. Donors wazungu hapana maana wao ni sehemu ya misiba inayotupata kila siku.
mambo matatu waliyosema wana jf wengine ni ya msingi sana! Moja kuwaepuka wahisani ni mkakati mzuri wa kuondokana na fikra tegemezi hasa kwenye jambo la utaifa wetu! Pili wananchi washirikishwe iwezekanavyo mana katiba ni yao! Tatu, matumizi ya viyombo vya habari ni muhimu sana hasa redio maana zinawafikia watu wengi zaidi nchini, ikichanganywa na tv, magazeti, nk tutafanya jambo zuri kwa TAIFA
LETU!