kaka kitila mkumbo nakuheshimu sana na hasa kipindi ulipokuwa pale
chuoni uliyafanya kazi nzuri sana kama rais wa Daruso. nakuomba unipitishie
maoni yangu haya kwa wateule wetu wa chadema. hatari iliyopo mbele ya chadema hivi sasa ni kwa wabunge na madiwani wao kuanza kununuliwa na ccm. sijui njia sahihi ya kuweza kukabiliana na hili kwa maana hawa ni watu wazima wana kila sababu ya kujiamulia mambo yao wenyewe. lakini chadema inachoweza kukifanya ni kuita kikao na wateule wake wote na kuwapa tahadhari hii mapema. kuwaeleza jinsi wananchi walivyo sacrifice kwa ajili yao na wajue wazi kuwa ccm inawatafuta kwa udi na uvumba kwa ajili ya kutaka kupunguza nguvu ya upinzani kwahiyo waelezwe wazi kuwa kitendo chao cha kukubali kununuliwa na ccm siyo tu ni usaliti kwa chama chako bali ni usaliti kwa waliokuchagua ambao wengine wametoa maisha yao kwa ajili yao kwahiyo usaliti wao siyo tu kwa chama bali kwa binadamu wenzao kwahiyo wana kesi ya kujibu kesho mbele ya Mungu na pia historia itawahukumu kwa kukubali kutumiwa kurudisha nyuma demokrasia ndani ya Tanzania kwahiyo huo ni usaliti dhidi ya nchi yako. kwa kuongezea kiwepo kiapo maalum cha chama cha utii kwa chama ikiwemo kutokisaliti chama na wapiga kura waliokuchagua. kwahiyo haya yote yafanywe ili wahusika wawe na information za kutosha kwa kitendo watachokifanya(God forbid). mimi binafsi ninaweza ku draft kiapo maalum cha chama kama mtaona inafaa.
hii ndio tahadhari yangu kwa chadema nitashukuru sana kama utaifikisha chamani. tume sacrifice vitu vingi sana na nisingependa kuona sacrifice hii goes on vain.
God bless Tanzania,
God Bless Chadema.