Kitila Mkumbo asimamishwa uongozi UDASA

Tukwazane Taratibu

Senior Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
194
Reaction score
539
Jana ilikuwa siku mbaya sana kwa Kitila Mkumbo ambaye ni mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT, ikumbukwe kuwa Kitila Mkumbo kufikia jana alikuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDASA), Kitila amekikalia kiti hicho kwa mda mfupi sana kuliko wenyeviti wote na kuandika rekodi.

Jana UDASA walikutana kwenye kikao chao cha kawaida kama ilivyo vikao vingine ila ijulikane kuwa Bwana Kitila Mkumbo alikuwa Sabbatical Leave ila cha kushangaza wasomi hao wa UDASA ni kumuona mtu aliyekuwa kwenye leave aki chair mkutano huo wa UDASA, Ndipo hapo wasomi nguli wa sheria kutokea kitivo cha sheria cha UDSM walianza kuhoji, wakipewa sapoti na Profesa Mkandala kwa nini mtu aliye kwenye likizo aje kuongoza kikao? Nini maana ya likizo? Au ndio Unkurunziza wenyewe?

Bila aibu au adabu Bwana Kitila Mkumbo alianza kujibizana na Maprofesa hao nguli na hata kumjibu shombo Prof Mkandala hali iliyopelekea Maprofesa hao kumshambulia ipasavyo pamoja na kueleza madhaifu yake yote ya Kitaaluma na Kinidhamu, walianza kumuelezea kuwa Mojawapo ya makosa anayoyafanya kama mwenyekiti wa UDASA ni kulitumia jukwaa hilo la wasomi kujijengea umaarufu wake binafsi pamoja na kuliigeuza kuwa jopo la kisiasa badala ya kuwa jopo la Kitaaluma, walimsema kuwa amekuwa akilitumia jukwaa hilo la wasomi kueneza propaganda za chama chake cha ACT hali iliyopelekea ukumbi mzima kuzizima kwa kelele na kumtaka Ang'oke haraka sana kabla hajang'olewa kitini hapo maana hakimfai tena.

Kitila Mkumbo kwa aibu kubwa huku akiwa anatiririkwa na machozi kwa jinsi alivyoanikwa hadharani atemeshwa mzigo. Hivyo basi nawaomba mjue kuwa kufikai mda huu Ndugu Kitila Mkumbo siyo Kiongozi wa UDASA tena.

Ameingia kwenye historia ya kuwa kiongozi alietimuliwa kila sehemu anayokimbilia, alianza CHADEMA, wakamtimua, akaenda ACT akatimuliwa akarudishwa na genge lake, sasa katimuliwa tena UDASA.

Pole sana ACT, Pole sana Kitila Mkumbo.

 
Weka picha yake
Hili jina si geni
Labda sababu tuko mbali na hii sanaa ya siasa
 
Kwani Kitila Mkumbo bila UDSM hamna maisha mbona Prof Baregu alifukuzwa UDSM na maisha yanaendelea.

uko sahihi Ritz, tatizo la vijana wengi ni utegemezi wa fikra za ili uishi sharti uajiriwe tena kwenye secta ya umma.
 
Acha upotoshaji pr, Kitila Mkumbo hajatimuliwa kama unavyotaka kuaminisha umma,acheni siasa za majitaka kuleta kweny taaluma huku hatuendeshwi na miemko.
 
sijaona mahala ameandika kuwa 'hamna maisha'. ni habari tu, kama habari nyingine.


Huyu jamaa ameandika kishabiki km si kimipasho. Anaonekana anachuki binafsi na Kitila !
 
Si yumo humu JF aje mwenyewe athibitishe.

BTW kutokana na mambo ya likizo hili ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania, wezi wote serikalini na kwenye mashirika hawataki kuchukua likizo.

Sheria zipitishwe kiongozi au yeyote kwenye ngazi ya juu kama hataki kwenda likizo afukuzwe au alazimishwe.

These people had been stealing with impunity.
 
Reactions: BAK
Duh kweli tunatofautiana uelewa. Hapa Kitila aliamliwa asiwe mwenyekiti wa kikao kwani yupo rikizo. hajaondolewa uenyekiti wa UDASA wala hajafukuzwa chuo.
 
"... madhaifu yake yote ya kitaaluma ..." - sasa walimpaje u-professor kama nao sio dhahifu?
 
Kwani Kitila Mkumbo bila UDSM hamna maisha mbona Prof Baregu alifukuzwa UDSM na maisha yanaendelea.

HAHAHAHAHAHAH....Unajifanya huelewi tu....

Hajafukuzwa ajira ya ualimu

Amefukuzwa uongozi wa chama cha wanataaluma wa UDSM

Ana damu ya kunguni yeye na wenzake...kila anapoenda anafukuzwa...hahahaha
 

Uko sahihi...wezi huwa hawataki kwenda likizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…