Kitila Mkumbo amshukuru Rais Magufuli kumteua kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
92,382
111,998

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Kitila Mkumbo amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo akichukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.

Prof. Mkumbo ambaye pia ni kada na mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema Rais amempa heshima kubwa kwa nafasi hiyo, na yeye kama mtumishi wa umma hawezi kuikataa kwa kuwa ni kazi aliyotumwa na mkuu wa nchi.

"Ukishapewa kazi na mkuu wa nchi, unaipokea na unaifanya kwa bidii kama yalivyo matarajio, kwahiyo nimepokea uteuzi, nimekubali, mkuu wa nchi akikupa kazi utaikataa vipi, mkuu wa nchi akikupa kazi unaifanya, kumbuka mimi ni mtumishi wa umma" Amesema Prof Kitila

Chanzo: Malunde blogs
 
Piga kazi Kitila hao hao wanaokubeza wanaitamani hiyo nafasi adimu kuipata.
 
Jambo moja lipo wazi. NI NJAA NDUGU ZANGU, BASI. CCM imewajulia wapinzani, ni kuwapa vyeo, kwa hiyo it may take hundreds of years kuitoa CCM madarakani. Maana ya hili ni kwamba, sasa hivi Mkumbo karudi CCM na kwenda kutangaza sera zake. Hata Zitto anatafutiwa nafasi UN au IMF. Hivi kati ya mdomo na tumbo yupi mpinzani wa kweli? Ni mdomo, lakini tumbo upinzani wake hufuata pale linaposhibia. Sasa hivi Mrema hajui hata TLP ni nini na hajatamka TLP tangu ateuliwe askari jela mkuu. TUMEKWISHA!!!!
 
Du!!,wasomi wetu kwa kusahau mambo,Leo kasema hivi kesho anafanya hivi,shikamoo wasomi
 
Jambo moja lipo wazi. NI NJAA NDUGU ZANGU, BASI. CCM imewajulia wapinzani, ni kuwapa vyeo, kwa hiyo it may take hundreds of years kuitoa CCM madarakani. Maana ya hili ni kwamba, sasa hivi Mkumbo karudi CCM na kwenda kutangaza sera zake. Hata Zitto anatafutiwa nafasi UN au IMF. Hivi kati ya mdomo na tumbo yupi mpinzani wa kweli? Ni mdomo, lakini tumbo upinzani wake hufuata pale linaposhibia. Sasa hivi Mrema hajui hata TLP ni nini na hajatamka TLP tangu ateuliwe askari jela mkuu. TUMEKWISHA!!!!
Mkuu umeongea point, ndugu yangu Mrema alishasahau kabisa kama kuna TLP, soon Lipumba atakuwa Gavana wa BOT.
 
Jambo moja lipo wazi. NI NJAA NDUGU ZANGU, BASI. CCM imewajulia wapinzani, ni kuwapa vyeo, kwa hiyo it may take hundreds of years kuitoa CCM madarakani. Maana ya hili ni kwamba, sasa hivi Mkumbo karudi CCM na kwenda kutangaza sera zake. Hata Zitto anatafutiwa nafasi UN au IMF. Hivi kati ya mdomo na tumbo yupi mpinzani wa kweli? Ni mdomo, lakini tumbo upinzani wake hufuata pale linaposhibia. Sasa hivi Mrema hajui hata TLP ni nini na hajatamka TLP tangu ateuliwe askari jela mkuu. TUMEKWISHA!!!!
Ccm ni mabingwa wa kucheza na saikolojia za watu.
 
Sasa kwanini hakuyasema haya kwenye teuzi zilizotangulia badala yake akasema wahadhiri waache wafanye kazi ya kufundisha... hapana chezea njaa ... kwani wahadhiri wengine walioteuliwa hawakua watumishi wa umma au ni yeye peke yake???
 
Zitto na Kitila si watu wa kuwaamini hata siku moja.
 
Wasomi wetu sio watu wanaoweza kusimamia maneno yao. Wengi wao wanaongozwa na tumbo kama huyu Profesa. Ni rahisi sana kujikana pindi wanapopewa ulaji
 
Siasa mtihani...mchezo unaohitaji utulivu sana wa akili. Imagine wale walioamini katika Kitila wana hali gani
 
Na wale wahadhiri wengine aliosema Rais anamaliza watu kwenye vyuo vikuu, walipewa na Mwenyekiti wa kijiji?

Wabongo tumezidi unafiki na uongo. Mtu likifika kwake, principles zinayeyuka !
 
Watanzania tu watu wa ajabu sana, yaani mtu umesoma mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni Uprofesa lakini huiamini wala kuipenda fani na kazi yake bali yuko anazuga! Anaamini uteuzi wa rais kwenye field ambayo hakuisomea ndio sahihi na heshima!!
 
Ni mnafiki wa hali ya juu. Hajui kipi anasimamia hujigeuza geuza kama kinyonga kwa kuweka mbele maslahi ya tumbo lake.

Sasa kwanini hakuyasema haya kwenye teuzi zilizotangulia badala yake akasema wahadhiri waache wafanye kazi ya kufundisha... hapana chezea njaa ... kwani wahadhiri wengine walioteuliwa hawakua watumishi wa umma au ni yeye peke yake???
 
Wasomi vigeu geu.
Ni rahisi kusema wasomi vigeu geu lakini ni vigumu kama mtumishi wa umma Kitila kukataa ile nafasi kwani asingeachwa huru labda angekuwa na sababu inayoeleweka (e.g. afya), vyuo vetu vikuu ni sehemu ya serikali na viongozi wake wanachaguliwa na serikali hiyo hiyo. Lakini pia kuna faida kwa pande zote-ACT inazidi kusogea karibu na serikali hata kama amejiuzulu nafasi yake ya ushauri wa ACT. Tatu anapata nafasi ya kuwatumikia watanzania wengi zaidi kwa wizara hiyo na hii kisiasa inamuweka mahali pazuri akifanya vizuri. Inaweza kuwa nafasi yake ya kujipanga pia kugombea ubunge (ACT/CCM) wakati ukifika 2020 au2025. Ukichukua yote hayo hakuna la ajabu yeye kumshukuru raisi. Tumuombee tu akafanye kazi nzuri ingawa hatakuwa Kitila yule kwani kazi yake mpya itamfunga na haina uhuru kama alipokuwa chuo. Mwishowe Katibu Mkuu ana marupu rupu si haba, huwezi kumlinganisha na Professa wa kawaida.
 
Sasa kwanini hakuyasema haya kwenye teuzi zilizotangulia badala yake akasema wahadhiri waache wafanye kazi ya kufundisha... hapana chezea njaa ... kwani wahadhiri wengine walioteuliwa hawakua watumishi wa umma au ni yeye peke yake???
Kasema waache au waachwe? Bahati mbaya utaratibu wetu hakuna atakae kuuliza kama unapenda hiyo post kabla hujachaguliwa. Ukichaguliwa hasa kama ni mfanya kazi wa umma ni vigumu kukataa. Raisi ana mkono utakao kufikia kazini kwako kama ataona umedharau uchaguzi wake. Wengine ni kweli wanaishi na kuota siku moja raisi atawaona lakini wengine inakua ndio hivyo.
 
Back
Top Bottom