Kitila Mkumbo amenena kwa makini na walakini

Rutaca

Member
Nov 13, 2014
94
236
Nimesoma maoni ya Mwalimu wangu Prof.Kitila Mkumbo juu ya umuhimu wa vyama vyenye mashiko makubwa kwenye uchaguzi wa marudio, yaani CUF, CHADEMA na ACT (kwa mtizamo wake), kukutana haraka na kuona namna ya kuachiana kata ikiwa imebaki wiki moja. Kwa mujibu wa Brother Kitila, jambo hilo likifanywa upinzani utashinda kata muhimu kwa kiwango cha kuridhisha. Maoni ya Mwalimu Kitila ni mazuri sana, kwa bahati mbaya hayatekelezeki na yamekuja kukiwa KUMESHAKUCHA. Mimi nina maoni yafuatayo;

1. Kwa uzoefu wa UKAWA (2014 - 2015), vyama vya Tanzania vinahitaji PLATFORM ya kuuendea uchaguzi walau MIEZI 18 kabla ya uchaguzi wenyewe. Yaani miezi Sita ya Majadiliano na kukubaliana na miezi 12 ya kutekeleza yale yaliyoafikiwa ikiwemo viongozi wa juu kufanya ziara PHYSICALLY katika ngazi za chini za vyama na kutoa msimamo wa umoja/makubaliano.

2. Kuna MASLAHI HASI mengi katika uchaguzi huu wa marudio. Uchaguzi ulipotangazwa tuliitisha vikao vya UKAWA na kukamilisha makubaliano ya namna ya kuachiana kata. Siku moja kabla ya kuyatangaza na kusaini MEMORANDAM mbele ya Watanzania, Bi. Magdalena Sakaya alizungumza na MEDIA na kuweka msimamo kuwa hakuna UKAWA, na kwamba CUF (Ya Msajili wa Vyama na Bwana Yule) itaweka wagombea kwenye kata zote. Pia, Bwana Yule alinukuliwa na redio moja akisisitiza hakuna UKAWA na kwamba CUF itakwenda yenyewe. Tulipofanya FIELD ANALYSIS na SITUATIONAL analysis tukaona kuwa katika mkanganyiko huu hakutakuwa na ushirikiano thabiti. Wakati tunatafakari hayo tayari mawakala wa Bwana Yule walianza kuzunguka kila kata kutafuta na kuweka wagombea. Tukaamua kuzika makubaliano tuliyofikia ili kuacha DUNIA ifanye kazi yake ya asili.

3. Tulipochunguza lengo la Bwana Yule na kundi lake tukagundua mkakati wao ni kuikomoa UKAWA bila kujali kuwa kuikomoa UKAWA hasara yake kubwa ni kuipa CUF kata "sifuri" kwenye uchaguzi huu mdogo wa marudio aw kata 20. Yaani, mkakati wa Lipumba wa kuja kupambana na UKAWA ni wa kuiua CUF kuliko kuiokoa. Huko nyuma, ni mkakati wa namna hiyo ndiyo umeiponza CUF, ni mkakati wa namna hiyo ndiyo Bwana Yule alijaribu kuufanya mwaka jana, akataka CUF ijitoe UKAWA kwa maslahi yake, tukawa na msimamo, tukamuacha akaenda ake ndipo CUF ikavuna ushindi mkubwa wa kihistoria. Katika uchaguzi huu wa marudio wa kata 20 CUF ina nguvu kwenye kata nne tu, kama ingeliungwa mkono na vyama vingine ingelipata madiwani "watatu hadi wanne", lakini mkakati wa CUF kuweka wagombea kwenye kata zote ili kuukomoa UKAWA una maana ya CUF kupata "SIFURI" jumapili hii. Maoni ya Mwalimu Kitila, kwamba vyama vishirikiane leo hayatekelezeki kwa sababu tayari BWANA YULE ameshaweka wagombea kila mahali ili kudumisha "SIFURI" alizoziasisi CUF kwa miaka 20.

4. Chama cha Pekee ambacho kinaweza kuvuka vikwazo vya mparaganyiko wa upinzani uliopo, ni CHADEMA, walau pamoja na vurugu za Bwana Yule na nguvu ya ACT kwenye kampeni hizi, bado CHADEMA wanaweza kushinda kata kadhaa (chache). Hii ina maana kuwa kata nyingi zitachukuliwa na CCM kwa sababu kimkakati CCM tayari inao mawakala miongoni mwetu. Nimefuatilia kampeni ya kikundi cha Bwana Yule katika kata kadhaa na nilichokisikia ni "kejeli na dharau" dhidi ya UKAWA, CHADEMA n.k. CUF inapojirudisha kwenye enzi za kuzunguka nchi kuishambulia CHADEMA kwa kuiunganisha na CCM inajirudisha kule kule kwenye siasa za SIFURI. Wiki moja iliyobaki haitoshi kurekebisha makosa haya ambayo kimkakati yanasimamiwa na CCM.

5. ACT imejikita katika masuala ya sera na kujiuhuisha zaidi kwa watanzania, jambo ambalo vyama vingine hulifanya kwa kusuasua. Tatizo kubwa la ACT ni kwamba mara kadhaa inayumba kujenga mashaka kwa vyama vingine. Mathalani, mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, viongozi wa ACT waliingia kwenye DENSI ya "JPM ndiye masihi alokuwa anasubiriwa". Sisi wengine tuliushtukia uongozi wa JPM mapema sana, ACT walichelewa mno na leo (kiukweli) wako kwenye boti moja na sisi, kuwa JPM siye "aliyekuwa anasubiriwa", "Masihi Msubiriwaji" bado hajaingia Ikulu na si rahisi akatokea ndani ya CCM directly. Sijawasikia viongozi wakuu wa ACT wakiishambulia CUF au CHADEMA katika kampeni hizi, nimeona wakimwaga sera tu, hiyo ni FAIDA kubwa sana katika kuanza kujenga kuwaamini na hata kuwa washirika wazuri wa UKAWA ya mbele ya safari.

6. Kitila amezungumzia suala la vyama kuachiana kata wiki moja kabla ya uchaguzi bila kuzingatia kuwa CUF imo kwenye mgogoro ambao yeye Kitila amekuwa na upande kwa muda mrefu tu (Siwezi kuweka details za role yake). Napata shida sana kumuamini Mwalimu wangu kwenye jambo hili. Mwalimu Kitila anafahamu kuwa mtu mmojawapo watakayezungumza naye ili kuachiana kata (Bwana Yule) alishafukuzwa uanachama na Baraza Kuu la CUF, na kwamba hivi sasa UHAI WAKE KISIASA umeegemea zaidi kwenye DOLA na CCM. Sielewi ni kwa namna gani Kitila anataka vyama vifanye mazungumzo. UKAWA ilishaweka msimamo kuwa inafuata maamuzi halali ya vikao halali vya CUF, Msajili wa Vyama anasema vikao hivyo ni halali lakini maamuzi yake ni haramu.

7. Kwa wiki moja iliyobakia naona ni rahisi zaidi kwa ACT na Bwana Yule kukutana na kukubaliana kuachiana baadhi ya kata. Bahati nzuri, ACT iko karibu sana kimahusiano na kimashauriano naye, nadhani ingezungumza naye haraka ili walau kama ushirikiano wa vyama vyote vya UKAWA hauwezekani basi walau ule vyama viwili ufanyike. Hii ingeweza kuwa PILOT PROJECT kwa ACT, kujua inahitaji washirika wa namna gani na wenye nguvu gani siku za mbele. Honestly, this is not a joke, naongelea a serious POSSIBLE PILOT PROJECT ambayo ingeisaidia sana ACT kujitafakari upya kwa sababu huko mbele tuendako vyama vitakavyo SURVIVE ni vile vyenye nguvu tu.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Kitila ni rafiki yangu, tofauti zetu ni za kiitikadi na kimitizamo tu, msitoane macho kwenye mjadala huu, jengeni hoja.

Wasalaam,

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J. S
 
ACT ndiyo wanatakiwa kuwa waelewa maana sisi wananchi wote bara tutaipigia kura chadema
 
Prof. Kitila is right na Mtatiro is wrong!.

Kwa sasa upinzani uko in between the two devils, the only way for survival is to choose the lesser, akimaanisha hata kama CUF haintambui bwana yule kwa sababu he is a devil, na CCM pía is a devil, then choose the devil you know!.

Kwa sababu huku bara bwana yule ndie anayetambulika, then lazima CUF wamkubali watake wasitake! . Kama amesimamisha wagombea kote, then vyama vingine vyote viwaunge wagombea wanne wa bwana yule. Na wagombea wa bwana yule wajitoe kwenye strong hold ya Chadema na ACT.

Forget kuhusu Ukawa ile, vyama viunde the emeegence winning coalition, wagombea weak wajitoe, upinzani wote wawachague strong holds za kila mmoja wao ili game ibaki ni CCM vs opposition.

Vinginevyo the opposition wata split kura kwenye vita vya panzi, ni furaha ya kunguru, CCM inakomba kata zote 20 kwa ulaini kama kumsukuma mlevi.

Paskali
 
Ibra the learned and Experienced one ...pamoja na mapungufu Yake mtatiro his no match to him lazma tu wakubaliane nae his think 5 mile awaY from there strategY mtatiro and Group wamkubali tu
 
Back
Top Bottom