issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,795
- 5,252
WAFUGAJI zaidi ya 800 wa jamii ya kimasai wamevamia eneo la wawekezaji wa kampuni ya utalii ya Tanganyika Film and Safary lililopo kijiji cha miti Mirefu na kuharibu mali mbali mbali zikiwemo nyumba 16 na magari tisa.
Katika tukio hilo wafugaji hao wanaosadikiwa kutoka Longido mkoani Arusha na Siha na kuweka kambi katika vijiji vitano vinavyozunguka eneo la mwekezaji wilayani humo mbali na kufanya uharibifu huo pia wanadaiwa kuingiza mifugo katika mashamba nane ya Ndarakwai na kuharibu mali ikiwamo kambi za watalii.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Geofrey Kamwela aliahidi kutoa taarifa juu ya tukio hilo baada ya kufanyika vikao vya pande mbili ikiwamo ya wafugaji na serikali wilaya ya Longido na Siha.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mitimirefu, Israel Kileo tukio hilo lilitokea juzi saa 7 mchana, baada ya wafugaji kudaiwa kuingiza mifugo katika mashamba ya mwekezaji huyo kwa madai ya kukosa eneo la malisho katika maeneo ya vijijini.
Jana (juzi) mchana nilipewa taarifa ya kuwapo kwa vurugu ambazo zilisababisha wafugaji kuchoma nyumba,magari na mali nyingine za mwekezaji, pia kulikuwa na taarifa ya mtu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi, alisema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama alisema, serikali imesikitishwa na tukio hilo na kutaka jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote waliotenda tukio hilo.
Alisema kama serikali ikilifumbia macha jambo hilo,huenda likawakatisha tamaa wawekezaji, kwani mwekezaji huyo pamoja na shughuli zake lakini pia amekuwa akisaidia katika miradi ya kijamii kama Elimu na Afya.
Gama alisema chanzo cha vurugu hizo ni kitendo cha wafugaji kutafuta eneo la malisho kutokana na wingi wa mifugo waliyonayo na hali ya ukame uliopo sasa
Taarifa tulizonazo ni kwamba hadi sasa wafugaji wamepeleka mifugo zaidi ya 300 katika mashamba ya mwekezaji, Yule ametunza eneo analomiliki lina mazingira mazuri na kuna ranchi kwa ajili ya aina zaidi ya 65 za wanyama pori na ndege zaidi ya 300 wa aina mbalimbali, alisema.
Alisema eneo hilo limetoa ajira kwa wananchi zaidi ya 76 za kudumu na muda maalum huku pia kukiwa na ajira za watu 20 kila siku jambo ambalo pia linaimarisha hali za kiuchumi za wananchi wa vijiji vinavyozunguka.
Gama alisema eneo la mwekezaji linapokea zaidi ya watalii 2500 hadi 3000 kwa mwaka jambo ambalo linachangia mapato ya mkoa na taifa kwa ujumla na kwamba serikali haiwezi kukubali kupotea kwa wageni hao.
Mwekezaji wa kampuni hiyo,Peter Jones alikiri, kupata hasara ya mamilioni ya shilingi na kuongeza kuwa taarifa kamili ataitoa baada ya kufanya tathmini ya kina.
Alisema wafugaji hao walivamia eneo lake majira ya saa saba na kuathiri watalii wane ambao iliwalazimu kuwahamisha na kuwapeleka mkoani Arusha kwa ajili ya usalama wao huku kampuni ikilazimika kusitisha safari za watalii 10 kutoa nchi za Uingereza na Marekani waliopaswa kuja mwaka huu.
Naye kiongozi wa wafugaji katika kijiji cha kitendeni na Mitimirefu, Kitasho Simeli alisema, chanzo cha vurugu hizo ni kitendo cha askari kuwapiga risasi wachungaji hao na kuwatelekeza porini.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaka viongozi wa wilaya ya Kiteto na mkoa wa Manyara kuwajibishwa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya wakulima na wafugaji
Dk. Slaa alisema mauaji yanayotokea mara kwa mara wilayani Kiteto yanayosababishwa na migogoro ya ardhi yanaonyesha kushindwa kuwajibika kwa viongozi
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, jana Dk. Slaa, alisema kutwa ya jana amekuwa akipokea simu lukuki zikimtaarifu hali ni mbaya na watu wanaendelea kupoteza maisha kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji kugombea ardhi, huku serikali ikiwa kimya na Watanzania hawajui.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, hadi jana mchana alikuwa amepewa taarifa watu wanane wamepoteza maisha katika Kata ya Matui na Olporotu, ingawa amewasiliana na IGP Ernest Mangu, aliyemthibitishia kuwa Polisi wako wilayani humo.
Mgogoro huo unaondelea una sura ya ukabila na unaendekezwa na viongozi wa kisiasa ambao ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ambao wana maslahi yao binafsi, alisema
Juzi Mkuu wa Mkoa RC Erasto Mbwilo, alifika huko wakamwambia kuna Masai wamezunguka maboma, badala ya kuchukua hatua akawaambia nendeni mkawaambie watawanyikendio maana nasema wameshindwa kuwajibika na nchi haina dira hivi sasa.
Alisema kazi ya serikali ni kuwahakikishia mazingira na haki ya kuishi wananchi, jambo viongozi hao wameshindwa kulisimamia na kumtaka Rais Jakaya Kikwete awatimue.
Amani haihubiriwi ila inatengenezewa mazingiramimi nashangaa sana ninapowasikia viongozi wa serikali tena wakubwa kabisa katika chombo kimoja cha habari wakihubiri amani, amani inatengenezewa mazingira, bila hivyo haki ya kuishi haiwezi kuwepo na ndicho kinachotokea Kiteto.
Haki ya kuishi hivi sasa haipo, wakulima na wafugaji hawakuandaliwa nani akae wapi na afanyie shughuli zake wapi. Serikali inashindwa kuweka mazingira ili haki ya kuishi iwepo, alisema.
Dk. Slaa, alisema Mkuu wa Wilaya, Martha Umbulla, ameshindwa kuwajibika muda mrefu kuondoa matatizo ya ardhi katika Wilaya hiyo, lakini amekuwa akiachwa.
Yule mama Mkuu wa Wilayatena alikuwa ni Mbunge mwenzangu, tunafahamiana na ni kabila langu. Hana uwezo Rais Kikwete anambeba, amuondoe ameshindwa kulinda amani, amekuwa akibagua na kuegemea ukabila, RC naye awajibishwe, alisisitiza.
Alibainisha kuwa, matatizo yanayotokea Kiteto yanatokana na vigogo kujilimbikizia ardhi, ngombe wengi na kumiliki ranchi kubwa hivyo kuona wakulima hawatakiwi
Tanzania hatupaswi kuwa na viongozi waoga, lazima maslahi ya pande zote yaangaliweangalia kuna Wizara ya Ardhi na Makazi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na ile ya Maliasili na Utalii, lakini wanashindwa kukaa pamoja kutatua matatizo kama haya ambayo pia tunayashuhudia Mvomero, Kilosa na kwingineko, alisema na kuongeza.
Tuna taarifa na ahata vyombo vya habari kuwahi kuripoti, serikali ilichangisha Wamasai mitamba kwa madai ya kupata fedha walizowaambia ni za kuwaondoa wakulima kwenye maeneo yao ili wapate sehemu za malisho, jambo ambalo halijafanyika, hivyo wafugaji kuamua hivi sasa kujichukulia hatua mkononi.
Kazi ya serikali ni kuhakikisha inalinda haki ya watu wake kuishi, lakini imeshindwa kuwajibika, utu umewekwa pembeni, Serikali haijali, alisema.
Kutokana na hali ya hatari Kiteto, maofisa kadhaa wa juu wa Jeshi la Polisi wamepelekwa huko kuhakikisha usalama unakuwepo, huku ikiripotiwa baadhi ya watu kuzikimbia kaya zao wakihofu mauaji na kukamatwa kuhusiana na mauaji hayo