Kiteto: Mwananchi anusurika kifo kwa njaa

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
7,002
9,987
Ndugu wanabodi kwa hali ya kushangaza,mtu mmoja amenusurika kufa baada ya wananchi kumkuta akiwa ameanguka chini huku akiwa anakula MAJANI kama mbuzi,kufuatia kuzidiwa kwa njaa kali,ndipo wasamalia wema walipomuokoa kwa kumpakiza kwenye Bodaboda na kumpeleka kwa afisa mtendaji wa kijiji cha MWANYA kilichopo wilaya ya KITETO mkoani MANYARA.

Afisa mtendaji wa kijiji cha MWANYA aitwaye MWANAIDI MASAWE,amesema baada yakuletewa mtu huyo ambaye jina lake halijatwa kufuatia mtu huyo kuwa hajitambui,walimkologea uji na kisha kumpeleka Hospital ya wilaya ya Kiteto,na amelazwa pia hawezi kuongea.

Amesema baada ya vipimo madaktali walisema mtu huyo anasumbuliwa na njaa kwani hakupata chakula kwa muda mrefu,hivyo Mtendaji ametoa wito kwa mkuu wa wilaya kupeleka chakula cha msaada,kufuatia eneo hilo kukumbwa na baa la njaa.

Chanzo: Radio ABOOD ,kipinda mwangaza wa habali,saa mbili usiku huu.
 
Last edited by a moderator:
na bado..
hapa kazi tu !
tutampelekea viwanda karibuni asihofu au tutavunja kibanda anachoishi auze jina TBC.
 
Back
Top Bottom