sangu mnene
Member
- Sep 5, 2012
- 92
- 35
Waswahili husema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Maadili yamekuwa yakishuka kwa kiwango cha kutisha miongoni mwa wahitimu wa chuo kikuu bora kabisa Afrika mashariki na kati UDSM. Wahitimu wa chuo kikuu cha DSM ni wazuri sana kielimu lakini miaka ya karibuni wamakuwa na tamaa iliyokithiri ya rushwa. Sasa nimegundua sababu. Sababu ni USAB.
Chuo kikuu cha DSM hasa sehemu ya mliman, kina uhaba mkubwa wa vyumba vya kulala wanafunzi.Haieleweki sababu hasa ya chuo hicho kutojenga mabweni.Wapo wanaodai kuwa inasababishwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wa chuo kumiliki Hosteli binafsi.Ni takribani robo tu ya wanafunzi wanapata vyumba.Ili kuhakikisha ugawaji huu wa vyumba unakuwa wa haki na usawa,kilianzishwa kitengo cha ugawaji vyumba USAB.Sasa USAB imebadilika chuo cha kuwafundisha wanafunzi namna ya kutoa na kupokea rushwa.
Rushwa zinatolewa bila woga, ukifika chuoni utaambiwa hapa chumba hupati bila kutoa rushwa.Vyumba vinauzwa kama bidhaa. Hebu nitoe mfano mdogo wa Mabibo Hostel, Block F lililotengwa kwa wanafunzi wa shahada ya pili na PHD. Jumla ya vyumba vilivyotengwa kwa wanafunzi wanaosomea PHD ni 24 tu,vilivyosalia ni kwa wale wa masters. Ili upate chumba hapo lazima uandae rushwa ya Tsh laki saba. Mwanafunzi atatoa hiyo rushwa, ikiingia tu chumbani huamua kuishi bila kulipia chumba husika na kwa kuwa pesa iliyotolewa ilitafunwa na wahusika wa USAB,wanashindwa kumwondoa.Miaka inaenda miaka inarudi chuo hakipati mapato ya vyumba sababu ya ubinafsi wa USAB
Inatia shaka pale ambapo uongozi wa chuo unashindwa kuhoji kwanini malipo ya vyumba hayakamiliki.Kukosekana kwa malipo ya vyumba, kumekinyima chuo pesa ya ukarabati. Wakati UDOM angalau wakimudu kufanya ukarabati wa mabweni yao kutokana na pesa zinazolipwa na wanafunzi wapangaji, UDSM wanashindwa kabisa kufanya ukarabati kwa kuwa vyumba vyao vimekuwa shamba la bibi. Mtu anaweza kuishi bure hata kwa miaka minne.Nawashauri viongozi wa chuo wafanye yafuatayo.
Waanze uchunguzi wao Block F Mabibo, wapite chumba kwa chumba (a) Wakague waone kama wanaokaa vyumba hivyo ni wale wa masters au wa PHD (b) Waangalie kama vyumba vyote vimelipiwa benki na kama kipo ambacho hakijalipiwa waulizwe USAB kwanini hakijalipiwa. (c) Waulizwe USAB kwanini wanafunzi waliopewa vyumba vya block F hawatangazwi hadharani. (d) Waombe msaada TAKUKURU ili kuikomesha tabia hii kwani inawafundisha vijana wetu namna ya kutoa rushwa bila woga (e) Wakishagundua ukwepaji mkubwa wa kodi ya vyumba Block F,waamue kufanya uchunguzi chuo chote (f) Waanze mala moja mikakati ya ujenzi wa mabweni mapya,yaliyopo yamechakaa kupita kiasi
Kama tabia hii ya kuwafundisha vijana mapema utoaji wa rushwa haitadhibitiwa, basi tujue tunaandaa bomu.Haiwezekani katika chuo bora nchini,mambo yakawa yanafanyika kienyeji na uongozi unaona.Vyumba vya wanafunzi wa masters wakae wao na vile vya PHD wakae wanafunzi wa PHD.Kukosekana utaratibu ni namna ya kuandaa mazingira bora ya rushwa. Samaki mkunje angali mbichi, kuruhusu watoto wadogo kujifunza kutoa rushwa bila woga ni kuliangamiza taifa.Serikali mpya ya Magufuli, imulikeni UDSM hasa USAB ni chuo kinachofundisha watu kutoa na kupokea rushwa.