Nilidhani serikali hii itakuwa smart kwenye kushughulika na Gwajima (Mchungaji) lakini kitendo cha waziri wa afya kuagiza mchungaji huyo akamatwe badala ya kujibu hoja zake kinaendelea kuthibitisha kuwa tuko kwenye mwendelezo wa utawala usiokubali mawazo na hoja mbadala...
Niliposikia tangazo la Waziri Gwajma kwenye tiivi,nikiwa migombani moivo,nikashtuka nikajiuliza mmm,kumbe hata balozi wa nyumba 10 anaweza kuwaambia jeshi la polisi,takukuru,tiss,magereza nakuamuru wanitafute wanikamate niende kuandika maelezo,nikajiuliza kirahisi hivyo tu.
Nikasema hapa tayari madaraka yameshalevya mtu.Nchi hii inakuwa kama haina taratibu na miiko ya uongozi,hata elimu ya siasa ya darasa la pili imetushinda.Hakuna mkuu wa Nchi,tupotupo tu.
Baadaye kumbe wapo wengi sana waliofikiri kama mimi badala ya utekelezaji,wakarekebisha na kushauri.Iweje leo hii kwenye majukwaa wala huna mamlaka hayo, unadhalilisha uongozi mzima na uonekane kwa wananchi kuwa hawajui wanachokifanya.Mimi nikafikiri hivi.Ingekuwa busara itumike.
Kuna Waziri wa Mambo ya ndani,Waziri wa Ulinzi na usalama wangeshirikishwa jambo hili,tena kimya kimya bila sisi wananchi wa kawaida kujua.Ona sasa mnavyolikoroga na kujibizana kwenye majukwaa.
UONGOZI NI DHAMANA.Leo umekalia kiti,kesho mwingine.Tuheshimu nafasi za wengine,nao wanaweza ndiyo maana wakapewa hizo nafasi.