Mchumia juani
Member
- Jan 28, 2008
- 27
- 13
KITENDAWILI CHA PROF. SARUNGI,IGOGO NA FEDHA ZA TACAIDS NA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA RORYA
Habarini za Asubuhi wana JF,Katika kuendeleza harakati za kupambana na ufisadi leo nataka niwangate sikio jinsi ambavyo viongozi wetu wanawatumia watu wengine kutunza fedha zao na wao kuonekana kuwa hawafanyi biashara,Hii ni taarifa ya Uchunguzi (Naweza sema katume ka Mwa Kyembe kadogo ambako hakajabarikiwa na Bunge).Taarifa hizi nimezikusanya toka Shirati,Utegi na Dar Es Salaam.
UTANGULIZI
Wana JF katika mizunguko yangu ya kawaida tu katika miaka miwili na nusu iliyopita wakati Kampeni za Ubunge na udiwani zikiwa ziepamba moto,Ndipo nilipobahatika kukutana na bwana Mmoja anaitwa Igogo akiongea na Vijana wa Rorya katika harakati za kumpamba mshikaji wake ambaye siku hizi hasikiki kabisa Bungeni,Prof Sarungi,Mojawapo ya kauli alizotoa ni jinsi alivyo Tajiri na anagyomiliki Fedha za TACAIDS za kanda ya Ziwa.Si UNAJUA wenzetu hawa wajaluo wakibarikiwa kupata mali wanavyojisifu? Hata yeye hakubaki nyuma.Kwa upande mwingine ilinipa nafasi ya kuanza kutaka kujua inakuwaje Bwana huyu ambaye anamiliki kambuni inayohusika na Clearing and Forwarding apewe fedha za kupambana na Ukimwi kanda ya Ziwa?
IGOGO NI NANI?
Igogo ambaye ni Raia wa Tanzania kutoka jimbo la Rorya ni mmiliki wa Kampuni ya UTEGI TECHNICAL ENTERPRISES L.T.D inyoshughulika na Clearing and Forwarding na Ofisi zake ziko karibu kabisa na pale Tiketi na Boti za kwenda Zanzibar zinapopatikana pale Posta.Kwa ujumla mwonekano wa ofisi hiyo kwa mtazamo wan je ni kama ofisi ya mtu yeyote wa kawaida tu kwani hata hivyo wanashare ofisi na jamaa wengine wana Rorya wao wanajiita UCHAU investment.Lakini mambo na Biashara zinazofanyika Ndani ya ofisi hiyo ni wimbo mwingine.
Ni Igogo huyu huyu ambaye alikuwa akijisifu kwa vijana wa walalahoi wana Rorya wakati wa Kampeni za Prof Sarungi ndiye huyu huyu aliye kuwa msimamizi wa Shughuli ya Prof Sarungi ya Kuongea na Wanafunzi wa Rorya wanaosoma chuo kikuu cha Dar Es Salaam pale ktk hoteli ya kifahali ya New Africa Hotel wakati uchaguzi unakaribia.Rafiki yangu mmoja ambaye alihudhuria Takrima hiyo alinihadithia jinsi ambavyo alijikuta akifungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kupata Dinner katika hotel ambayo hana hakika kama atakuja kupata nafasi ya kuwepo tena hasa ukizingatia mshahara wake baada ya kupata Digrii ya Ualimu hapo UDSM.
Ni Igogo huyo huyo aliyenunua Saa ya Rais Kikwete kwa Mamilioni mengi tu katika mnada Fulani kabla ya Uchaguzi.
Ni Igogo huyohuyo ambaye inasemekana alimfuata waziri mkuu Edward Lowasa kule Uingereza na kumkatiaa chake wakati Mgogoro wa wapi pawe makao makuu ya Wilaya mpya ya Rorya kati ya Utegi na Shirati ukiwa tete.Na mheshimiwa alivyozuru Shirati alitoa maamuzi Yenye ujasiri wa kifisadi
Ni Igogo huyu huyu ambaye tunaamini ndiye anayemtunzia Prof Sarungi fedha na Biashara zake Ndiye ninayemuongelea.
MCHAKATO WA KUWANIA UWAKALA WA FEDHA ZA TACAIDS
Baada ya World Bank kutoa mamilioni ya fedha ili kupambana na Ukimwi na Baada ya TACAIDS kuamua kutafuta wakala wa kusimamia fedha hizo katika kanda tofauti tofauti ndipo mchakato wa kuomba nafasi hizo ukaanza,Mashirika Mengi ya Kimataifa na kitaifa yakaomba kusimamia fedha ktk kanda mbalimbali ikiwemo ya Ziwa,kama vile Family Health International (FHI),ambao ni wazoefu wa masuala ya Ukimwi na Elimu ya uzazi kwa muda Mrefu,RED CROSS,African YouthAlliance (AYA) ambao wametanua huduma zao hadi vijijini hasa kandokando ya Ziwa Victoria,AMREF ambayo inasimamia vituo vya Angaza na Mashirika Mengi sana yenye uzoefu wa Kimataifa katika masuala ya Ukimwi.Japo kuw suala hilo lilikuwa wazi lakini tenda hiyo walipewa KOSHIKA WOMEN GROUP(Ilala) wakiwa na ubia na UTEGI TECHNICAL ENTERPRISES L.T.D(Ilala) NA RAO HOSPITAL(Shirati-Tarime).Utatu huu ukasaini mkataba na kuanzisha ofisi yake pale Waterfront Posta Dar Es Salaam,Hapa kuna maswali kadhaa ya Kujiuliza:
1.Je inakuwaje mashirika ya kimataifa ambayo yamekuwa yakijishughulisha na Mambo ya Ukimwi kwa Muda mrefu na wameeneza huduma zao hadi vijijini wakanyimwa tenda hiyo na Kupewa UTATU huu wa Koshika,Utegi na Rao?.Has ukizingatia kuwa Koshika Women Group wamesajiliwa katika Manispaa ya Ilala na walikuwa hawana wigo mkubwa wa Kitaifa?na UTEGI T.E L.T.D Ambayo inafanya clearing and Forwarding hapa Dar na Rao Hospital iliyo katika Bonde Fulani pale Shirati na Huduma Mbovu za Afya hadi kukosa Wateja ndiyo wapewe mamilioni haya? Hizi siyo dalili za kufanyia Forwarding fedha zetu katika mifuko na Vitambi vya watu?
2.Je Koshika,Utegi na Rao Wana Uzoefu gani wa kuwazidi FHI,AMREF,AYA katika masuala ya Ukimwi?
3.Je Koshika,Utegi na Rao ni Makampuni ya Mtummoja?
Ili kujibu Maswali haya hebu tuwaongelee kidogo Wahusika
KOSHIKA WOMEN Group
Wakati nikiwa palepale Shirati na Utegi niliona Kibao kikiwa katika kibanda cha Mafundi herehani akina mama kimeandikwa KOSHIKA WOMEN GROUP Sijui kama ndiyo hawa hawa Koshika Women Group wanaopatika na Katika ILALA MUNICIPAL COUNCIL HIV/AIDS SERVICE DIRECTORY amyo ina taarifa zifuatazo ktk ukurasa wa 14;
8. Koshika Womens Group
Physical Address: Ilala, Moshi Street
Contact Address: P. O. Box DSM,Telephone: +255 22 2211454
Contact Person: Ms. Neema Naiman
Organisation Type: Non Government
Aims: To organize and disseminate HIV/AIDS information to adolescents, youth and women in DSM
Services Provided: HBC to PLWHA, IEC materials and Research
E-Mail ;NIL
Fax;Nil
Kutokana na Taarifa hii tunatambua kuwa kupewa Jukumu la kusimamia fedha za Ukimwi kwa Kanda ya ziwa walikopew Koshika Womeni Group kama si wale washona cherehani wa shirati ilikuwa ni Zengwe tu.Huyo Ms Neema Naiman nikianza kujadili uhusiano wake na Prof Sarungi nitamuumbua mtu mzima .Hata hivyoHakukuwa na haja ya kukipa kikundi cha Wanawake ambacho kimesajiliwa kuendesha shughuli zake kwa Wanawake Mkoani Dar Es Salaam kusimamia Mamilioni ya fedha za mkoani Mwanza ambako hawakuwa na Ofisi wala kibali cha kufanya kazi huko.Na ndiyo maan ofisi zikatafutwa chapchap pale Waterfront.
UTEGI TECHNICAL ENTERPRISES L.T.D
Hii nimeshaieleza hapo juu na mmiliki wake ni mtu wa Karibu sana wa Prof.Sarungi unaweza kupata habari za kampuni hii ktk website yao ya www.ute-tech.net halafu unambie Neno UKIMWIlimetajwa wapi kama shughuli zao.Kuna maelezo kama haya:
As a Logistics Company in Tanzania, we are providing air sea freight forwarding, custom brokerage, warehousing, door to door delivery and distribution, Full Container Load, project cargo, Local Container Load Consolidation, Clearance of duty exempted goods for the NGO's, Religious, Charitable, Relief and Governmental bulky and small consignments, order follow-up and International Investors facilitation...'
SAMPLE YA MKATABA
Home > Projects > Projects Database > Contracts/Contractors > Contract Details
Contractor: KOSHIKA WOMEN GROUP IN ASSOC. WITH RAO HOSP AND UTEGI TECH ENTERPRISES (T) LTD
Contractor Country: Tanzania
Contract Description
Total US$*
Signing Date
Project Name
Proc. Group*
CONTRACT FOR CONS. SERVICES COMPLEX TIME BASED ASSIGNMENTS BTN TACAIDS & KOSHIKA WOMEN GRP IN ASS. WITH RAO HOSPITAL & UTEGI TECH. E
0.864 10-MAR-2005 Multi-Sectoral AIDS Project
CS
* Contract amount in USD$ millions. Click column header to sort, click again to reverse.
Procurement Group GW - Goods and Works , CS - Consultants
Projects Home | Advanced Projects Search | Contract/Contractors Search | Browse | Help/FAQ
Mkataba Unapatikana katika Webpage; http://web.worldbank.org/external/p...SitePK=40941&menuPK=228443&contractid=1250241
RAO HOSPITAL
Rao Hospital kama nilivyosema ipo Shirati na kutokana na ubovu wa Huduma za Afya na usanii kuanzia kwa Manesi mpaka Madaktari imekuwa ikiyumba kwa muda kama miaka mitatu hasa kutokana na Kukosa wateja.RAO hiyo hiyo ambayo inashindwa kujiendesha vizuri ndiyo walopewa kushikilia Mamilioni ya TACAIDS,Katika ka uchunguzi kangu mmiliki wake ambaye nilitajiwa kama MCHUNGAJI ambaye kwa sasa anaishi Musoma Kama msimamizi wa Fedha Za TACAIDS mkoani Mara na ambaye ni Jamaa yake Prof Sarungi,huyo ndiye MCHUNGAJI!
KOSHIKA, UTEGI NA RAO WALIPATAJE MAMILIONI YA UKIMWI?
Wakati wa kutafuta msimamizi wa Mamilioni ya TACAIDS Prof Sarungi alikuwa Waziri wa Ulinzi na kwa taarifa za ndani toka katika Taasisi ya TACAIDS inasemekana alikuwa na uhusiano wa karibu na Mkurugenzi wa TACAIDS wa wakati huo ambaye waliwahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma I mean ni Mshikaji wake wa Muda Mrefu,Yupo mfanykazi wa TACAIDS ambaye anathibitisha mawasiliano kati ya Wakubwa hao.Ni wazi kwamba Utatu huu wa Koshika,Utegi na Rao ni muunganiko ambayo ulitengenezwa na Prof. na hatimaye akapigiwa Pande.
Hii inathibitika katika Report ya TACAIDS ya mwaka 2005/2006 hasa ukiangalia NGO zinazosemekana kupata fedha kutoka katika utatu wa KOSHIKA,UTEGI n a RAO Ndugu yangu unaweza kutoa machozi kwani nyingi ni usanii tu huku wavuvi waliosongamana katika makambi ya Uvuvi na wanafanya Ngono bila kutumia kinga wakiambukizana Maginjwa ya Zinaa na hata Ukimwi halafu fedha zinapelekwa kwa Wakulima ambao hawako ktk Mazingira Hatarishi.
CONCLUSION
Kutokana na Chain iliyopo ya undugu na Urafiki kati ya Prof Sarungi,Igogo,Mchungaji,Koshika,Rao,Utegi hapa tunaona kabisa kuwa Prof Sarungi ambaye wakati huo alikuwa waziri wa Ulinzi wa Tanzania alipigiwa Pande ambalo aliwapa watu kumshikia Bendera.
Nitakuhadithia siku nyingine mchakato wa Makao Makuu ya Wilaya Ya Rorya na Harakati za Igogo,Sarungi,Lameck Aila n.k katika kuharalisha UTEGI kuwa makao makuu huku wakipuuza maoni ya Wananchi na ufisadi na Rushwa vilivyotawala katika Baraza la Madiwani wakati wa kupigia Kura makao makuu ya Wilaya mpya ya Rorya.
HII NDIYO TANZANIA NA SISI NDIYO WATANZANIA WENYEWE