Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,135
- 48,824
Marehemu Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Paul Kihwelo anayeisikiliza kesi hiyo, amesema atatoa uamuzi wake endapo mtuhumiwa ana kesi ya kujibu au la Saa sita mchana.
Iringa. Kesi ya mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Iringa, Pasificus Simon, inaendelea leo baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi kumaliza kutoa ushaidi wao jana.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Paul Kihwelo anayeisikiliza kesi hiyo, amesema atatoa uamuzi wake endapo mtuhumiwa ana kesi ya kujibu au la Saa sita mchana.
Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Wakili wa utetezi, Rwezaula Kaijage alidai mahakamani hapo kuwa katika mashahidi wake wanne hakuna hata mmoja aliyetoa ushahidi wa moja kwa moja unaomuhusisha mtuhumiwa na mauaji.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Ladislaus Komanya na Sunday Hyera, ulidai kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wao wanne, Mwangosi aliuawa eneo la tukio, na kifo chake si cha kawaida.
Chanzo: Mwananchi.