Usedcountrynewpipo
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,636
- 2,734
Usingizi mzuri na mnono unapatikana mahali palipo na utulivu na hewa yenye jotoridi la wastani. Baadhi ya vifaa tunavyovitumia kupatia usingizi huo vinapoleta mushkeli, ni wakati mzuri wa kuvirekebisha ili kupata usingizi mwanana. Pia wale wenye majukumu ya ziada inatokea uwanja wa sita kwa sita ukawa unapiga kelele za kwichi kwichi... Je ni hatua gani za kuchukua ili kuondoa hali hiyo?
Kaza nati/Screw:
Kitu chochote kinapotumia (mechanical movement) huwa kina tabia ya kulegea. Hivyo kama kitanda chako kina nati/screw zikaze mara kwa mara.
Weka vilainishi:
Mimina oil/grease kwenye maungio ya vipande vya kitanda. Hasa kwenye maungio kama bawaba na kwenye chaga, ambayo inashikana na upande wa kitanda.
Kupata usingizi mwanana, kumbuka kulalia mashuka masafi/ mto msafi. Pia hakikisha chumba kimepuliziwa dawa ya mbu au lala kwenye chandarua hasa kile kilichowekwa dawa....