Da Pretty
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 3,059
- 1,153
Kwanza niwatakie heri ya mwaka mpya ujao 2013 Muda huu nipo na laptop kuna jambo limenipa utata Rafiki yangu wa miaka mingi anaishi mkoa fulani kusini amenialika kwake na nimeingia leo. Nimefika na kupokelewa vizuri ila tangu chumba nilichokaribishwa mashaka yalinijaa kimejaa bidhaa za kiume(nguo, viatu, mafuta...) nikauliza vipi nikaambiwa nitulie. Badae nikagundua best anaishi na mpenzi wake, cha ajabu muda wa kulala ananiambia tutalala watatu chumba kimoja na kitanda kimoja yani mimi yeye na mpenzi wake. Hili limenikwaza sana naona ni kitu cha tofauti na mbaya zaidi yeye ndio kanikaribisha na tiketi ya kuja huku kanitumia yeye. Hii imekaaje? mi nimeshindwa kwenda kulala kwa mtindo huo.