Kama ni UGONJWA basi BARA la AMERIKA na ULAYA wanaongoza kwa kuwa na WAGONJWA wengi.....Pamoja na kuwa ni ugonjwa unaotokana na kuzidisha kula lakini jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikiutafuta kwa hali na mali ili kuweza kupata heshima kwenye jamii.Mtu mwenye ugonjwa huo hupewa kipaumbele na kuonekana bora kuliko wengine katika jamii.Wakati mwingine kitambi hutumika kama kipimo cha mafanikio ya mtu.Watu wanaweza kukuona wa ajabu kama una mali lakini hauna ugonjwa huu ambao wakati mwingine huitwa utapiamlo au obesity.Unaweza kukosa hata mke na mambo ya muhimu kama haujabahatika kuwa na hilo gonjwa la kujaa mwili na tumbo.Je watu hawajui kuwa kiambi ni ugonjwa au wanajitoa ufahamu?
Kula vizr yan namaanisha usiruke ata mlo mmja na hakikisha unashibaMkuu kinapatikana vipi kitambi
Kula vizr yan namaanisha usiruke ata mlo mmja na hakikisha unashiba
Kwamba hata njaa ikija tuna akiba sio?Ila kama ni UGONJWA unao sababishwa na ziada ya CHAKULA.
Naona ni Ugonjwa wa KUJIVUNIA.
Uwe na uhakika wa KULA milo mitatu HEAVY (ya Nguvu kabisa)...Mkuu kinapatikana vipi kitambi
Kabisa mkuuKuna baadhi ya nchi Duniani hapa ukiwa na kitambi sahau kupata mchuchu. Ukiwa na kitambi unaonekana mjinga mbele ya jamii, mpenda kubukanya (kula hovyo) na usiejali afya yako.
Tena afadhali Kitambi hicho uwe nacho mgeni walau wataogopa au watakunyooshea vidole kwa siri, ukiwa mwananchi ndio una kitambi utaishi kwa tabu sana, ukiumwa hata kidonda cha mguuni ukienda hospital tegemea kuchanwa ukimkuta doctor aliyepinda, kuwa kwanini umeuachia mwili mpaka uwe hivyo.
Kuna baadhi ya nchi watu wanene hasa uliotokana na kula kula wanaishi kwa shida sana mbele ya jamii zao.
Wanaposema tupo nyuma tupo nyuma kweli, kwetu jambo la kawaida kumkuta Daktari na kitambi, huku ughaibuni unaweza kutembea hospital zote mpaka miguu kutokea mabegani usimkute daktari wa namna hiyo.
Zamani kabla sijaja kuelimika huku nilikuwa naona kitambi mswano tu, nilipokuja huku na kuelimishwa madhara yake, nikajiona mjinga, hivi sasa hata iweje siwezi kukiruhusu kwenye mwili wangu.