Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,634
- 46,278
Nikiangalia watu wengi na picha nyingi za watu wa kuanzia mwaka wa 2000 kurudi miaka ya nyuma sana sioni kama watu wengi walikuwa na vitambi, unene uliopitiliza, kiribatumbo au kunenepeana mashavu na shingo.
Mfano ukiangalia hata viongozi wa enzi za Nyerere katika Serikali na chama utaona wengi walikuwa na siha njema na miili ya wastani, ni nadra kuona vitambi na watu walionenepeana.
Inawezekana maendeleo yanaleta matatizo mapya mabaya zaidi. Natambua changamoto za kiafya kwa wale ambao wana matatizo ya kiafya yanayosababisha miili yao kunenepea kwa kupitiliza. Ila hapa naongelea wengi wa watu ambao wamenenepeana kwa kula hovyo au uzembe mwingine.