Wakuu sitaki kuwachosha nawaletea habari kamili, kuna siku nilienda katika mazishi sasa nilifuatana na rafiki yangu wa kike, tumefika pale tukakutana na ndugu zake katika kubadilishana mawazo zikaingia story za usafi wa mwanamke.
Ndugu mmoja wapo akawa anaelezea jinsi ya kusafisha uke, akasema namnukuu "mwanamke ili awe msafi wakati wa kujisafisha achukue kitambaa cha kotoni au pamba aingize ukeni asubuhi alafu jioni ndio akitoe then akutane na mume wake.
Mimi nililiacha palepale maana niliona zito kwangu, sasa rafiki yangu ambae ni ndugu zake kalibeba na tangia siku ile uzi ndio huo, sasahivi mjamzito nabado anaweka jamani haiwezi kumletea madhara kweli?
Nawaasa wasichana wenzangu pia msije mkatumia njia hii kwakweli naona ya ki local sana na nafikiri inaweza ikaleta balaa baadae, maana unashindisha nguo ndani kutwa mzima wakati sio mahala pake kwa uelewa wangu mdogo nadhani inaweza ata kusababisha cancer au tatizo lolote zito.