Kitabu: Technofeudalism: What killed capitalism.

Kitabu: Technofeudalism: What killed capitalism.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,884
Reaction score
18,824
Kitabu hiki kimeandikwa na mwanazuoni Yanis Varoufakis, ambaye amewahi kuwa waziri wa fedha wa Ugiriki na pia ni mwalimu wa chuo kikuu. Kwenye hiki kitabu anaelezea jinsi ambavyo ubepari umegeuka kuwa Ukabaila-Teknolojia(Technofeudalism).

Kabla ya ubepari kulikuwa na ukabaila. Kabaila ni mtu anayeishi kwa kwa kodi. Mfano kabaila anahodhi eneo kubwa la ardhi na kuwapangisha watu. Hawa ndiyo walikuwa matajiri kabla ya ubepari. Mfano ni mfumo wa Nyarubanja kwa Wahaya. Bepari yeye anatumia mtaji(Hasa Mashine) kutengeneza pesa. Anaajiri watu wa kumfanyia kazi na kumuingizia pesa. Ubepari ndiyo uliua ukabaila.

Watu wengi, kama Karl Marx waliamini kuwa baadaye wafanyakazi watawapindua mabepari wanaowanyonya na kuweka ukomunisti. Kuwa Ubepari utauliwa na ukomunisti. Yanis kwenye hiki kitabu anasema kuwa Internet imefanya mambo yaende tofauti na ilivyotarajiwa. Kwamba badala yake ubepari umekuwa replaced na Technofeudalism(Ukabaila wa kitechnolojia au wa kimtandao). Makabaila-mtandao hao ni kama Amazon, Facebook, Uber, Twitter, Alibaba nk nk. Hawa , kama walivyokuwa makabaila-wanaishi kwa kutoza kodi. Mtu anayeuza kupitia Amazon au alibaba anatozwa kodi. Mtu anayetangaza biashara kupitia Facebook anatozwa kodi. Anasema mabepari wamegeuka kuwa vibaraka wa Makabaila mtandao kwa sababu kwa sasa bila bepari kuwa Amazon au Alibaba au Twitter na facebook ni vigumu sana kufanya biashara. Anajaribu kueleza nini kifanyike na namna ya kupambana na Makabaila wa kiteknolojia.

Humo ndani pia anaeleza kwa undani mgogoro wa kibiashara kati ya China na US. Kinakupa picha nzuri juu ya bifu la Trump na China maana kimechapwa 2023.

Kitabu kizuri na Yanis Varoufakis ni mwandishi mzuri mwenye mawazo 'mageni.' Pia unaweza cheki akihojiwa Youtube.
1745756879278.jpeg
 
Back
Top Bottom