Kitabu cha maisha ya mwanadamu
Utangulizi
Maisha ya mwanadamu, yana sehemu kuu tatu:-
Sura 1: Kuzaliwa
Mtu anazaliwa pale panapokuwa na uhusiano wa kimapenzi, kati ya mwanaume na mwanamke.
Na uhusiano huo uleta ujauzito na baada ya miezi 9 mtoto uzaliwa.
Na tukio hili hutokea mara moja
Sura 2: Kuishi
Mtoto akishazaliwa, upitia malezi mbalimbali, pamoja na kupata elimu stahiki, itakayomuwezesha kuishi katika jamii.
Kutofautiana kwa malezi, na elimu; kutoka kwa familia moja kwenda nyingine; kunasabisha kuwa na watu wenye tabia na mitazamo tofauti.
- Mitazamo hasi:-
Ujambazi
Uhuni
Uzurumaji/utapeli
Unafiki/uongo
Ubinafsi
Uchawi
Ushoga
Chuki
Ujilimbikiziaji wa mali
Tamaa n.k
- Mitazamo chanya:-
Ni kipindi ambacho binadamu ataishi kwa furaha, pia ni kipindi ambacho ataishi kwa huzuni.
Ni kipindi ambacho, watu uishi huku wakidharauliana; na mwingine kujiona bora zaidi kuliko mwingine; ni 'full' kukanyagana.
Kutokana na viungo kuchoka, ulaji wa vyakula, umri mkubwa, magonjwa nyemelezi n.k; binadamu uanza kudhoofika.
Sura 3: Kufa
Hii ni hatua ya mwisho, inayofunga kitabu cha binadamu, na kubaki kuwa historia kwa waliobaki.
Na hii utokea mara moja tu.
Kama alitenda mema atakumbukwa kwa mema, na kama hakutenda mema atakumbukwa kwa aliyoyafanya.
Mali zote alizozitafuta, ataziacha; na mwili tu ndio utakao-ifadhiwa.
Mwisho
Nilichojifunza katika hiki kitabu, wote tulio hai leo; tupo kwenye sura 2, na wengi huwa tunajisahau kuwa hatutafika sura 3.
Ukijua sura 3 lazima ufike, itakusaidia kuishi vizuri katika sura 2; haya mambo ya kukanyagana katika sura ya 2 yatapungua.
Swali: Sura 2 kwako ikoje?