Kitabu cha Biubwa, "Mwanamke Mwanamapinduzi" ni chemsha bongo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,249
KITABU CHA BIUBWA, ''MWANAMKE MWANAMAPINDUZI'' NI CHEMSHA BONGO

Labda kwangu mimi kama si kwa Dr. Harith Ghassany kunitia katika utafiti wa kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' nisingejua mengi katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Kubwa katika kitabu cha Dr. Ghassany ni kufichua moja ya siri kubwa sana katika historia ya mapinduzi nayo ni kuwepo kambi ya mamluki wa Kimakonde wakata mkonge waliokuwa Kipumbwi, kijiji kidogo cha wavuvi maili chache kutoka Tanga na jirani ya Pangani.

Wamakonde hawa walikuwa waajiriwa wa shamba la mkonge la Sakura.

Kambi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Victor Mkello na Omari Mkwawa kwa jina lingine, ''Tindo,'' jina alilopewa na Mzee Karume wakati wa harakati za kupigania uhuru Zanzibar.

Wamakonde hawa walikuwa sehemu ya jeshi lililoshiriki katika kupindua serikali ya Zanzibar.

Mzee Mkwawa anasema wakati wa matayarisho ya jeshi hili ilikuwa marufuku kwa mtu yeyote kuonekana jirani ya kambi ile.

Hakuna kiongozi yeyote Zanzibar ambae anakubali kuwepo kwa kambi hii au kuwa Wamakonde walivushwa kuingia Zanzibar kufanya mapinduzi.

Lakini ukweli ni kuwa kambi ya Kipumbwi ilikuwapo kama alivyokuwapo Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa na Wamakonde walionekana Zanzibar asubuhi siku ya mapinduzi.

Kitabu cha Biubwa hakina lolote katika haya na mara kadhaa kinamtaja John Okello kama kiongozi wa mapinduzi.

Kitabu cha Biubwa hakina lolote katika haya na mara kadhaa kinamtaja John Okello kama kiongozi wa mapinduzi.

Dr. Ghassany kaeleza katika kitabu chake jambo lingine zito na muhimu ambalo hakuna mwandishi wa historia ya Zanzibar alilieleza nalo ni mchango wa Wayahudi katika mapinduzi.

Katika hili Biubwa kaeleza lile ambalo labda kwa kukisia ndiyo litaingia katika fikra ya mwanafunzi wa historia ya mapinduzi.

Dr. Ghassany kaeleza uhusiano uliokuwapo baina ya Myahudi Moshe Finsilber na Karume na uongozi wa ASP.

Dr. Ghassany hakugusia hata kwa mbali kuwa Moshe Finsilber alikuwa na uhusiano na Julius Nyerere.

Kitabu cha Biubwa kinasema kuwa Nyerere akifahamiana na Myahudi huyu na ndiye aliyempa amri Finsilber kuwapeleka Karume, Hanga na Babu Zanzibar siku ya pili asubuhi baada ya mapinduzi.

Kwa kuelezwa haya kitabu Biubwa kamsadikisha Dr. Ghassany kwa mengi.

Msomaji anachotakiwa kufanya ni kuunganisha yale ya Wamakonde wa Kipumbwi, Wayahudi ndani ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika chini ya Julius Nyerere ili kupata picha kamili ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Labda utajiuliza wako wapi Makomredi na nini nafasi yao katika haya yote ya kupinduliwa serikali ya Sheikh Mohamed Shamte?

Hashil Seif kaandika kitabu, ''Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar,'' (2019).

Ipo pia makala ya marehemu Salim Msoma, ''Zanzibar the Agony of its History,'' (2016).

Kitabu cha Biubwa kimefunua ukurasa mwingine ambao unahitajika kusomwa.

Screenshot_20211110-230726_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom