Kiswahili ni lugha ya taifa, je english ni official language?

dikembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,645
1,439
Swali langu limezaliwa kutokana na matukio kadhaa wa kadhaa yanayojiri kwa sasa hapa nchini na nje ya nchi haswa tukiwa tumewakilishwa na mkuu wa nchi.

Kwa wale tuliosoma shule za kawaida za msingi (zile za serikali wakati huo ujio wa hizi saint nini ulikua bado upo kenya) , tulipata sana taabu kipindi cha presentations za vyuo na secondary kwa matumizi ya lazima ya lugha pendwa ya kiingereza. wale tuliopenda kupiga soga kwa lugha ya taifa tulivishwa bango la swahili speakers, tukazowea na kukubaliana na changamoto na kuishinda.

English ikawa lugha halali ya mawasiliano kiofisi, hata barua pepe tunaandika kwa lugha ya kiingereza, hata kwenye usahili wa kazi sekta zote binafsi na serikali lazima upasue yai.

Sasa namba moja anavyotumia kiswahili kwenye mikutano ya kikazi nje na ndani ya nchi hii imekaaje? au kuna mabadiliko yamefanyika? Kama kuna mabadiliko tafadhali tupeane taarifa wanaforum...

Thank you.....
 
Mkuu,ni kweli Tanzania tuna lugha mbili. Moja ni ya
KISWAHILI ambayo ni lugha ya Taifa.
Ya pili ni
Kiingereza na KISWAHILI ambazo ni lugha za KIOFISI. Hizi zote mbili hutumika.

UMOJA wa nchi za Afrika AU una official languages/Lugha rasmi zinazoweza kutumiwa na viongozi wa nchi hizo bila shida. Nazo ni:
KISWAHILI,
KIARABU,
KIRENO,
KIFARANSA, na
KIINGEREZA.
Rais yeyote ama kiongozi yeyote anaweza KUCHAGUA ni lugha gani ANAYOIPENDA.
Na hivyo kuitumia kuwahutubia viongozi wenzake.
Na hivyo Magufuli kutumia lugha ya KISWAHILI BADO alikuwa katika mpangilio wa AU.
 
Unafundisha usichokifanya..

Ni sawa na mchungaji anayehubiri kuacha ulevi wakati yeye anashindia kunywa bapa..

Asilimia kubwa ya sheria za Tanzania zimetungwa kingereza, halafu bwana mkubwa yupo bize kuongea kingereza kwenye mikutano ya kimataifa..

Nna uhakika hata barua ya mwaliko aliandikiwa kwa kingereza..
 
Hapa hata mimi nilipata mashaka na zile sheria za 'NO ENGLISH NO SERVICE' au tulionewa tu? au kila mfalme na zama zake?

Kama inawezekana kutumia swahili peke kwanini tugharamike kuwasomesha watoto wetu FEZA schools? Hii nchi ina sera nyingi sana zinazobishana zenyewe kwa zenyewe.
 
Mkuu,ni kweli Tanzania tuna lugha mbili. Moja ni ya
KISWAHILI ambayo ni lugha ya Taifa.
Ya pili ni
Kiingereza na KISWAHILI ambazo ni lugha za KIOFISI. Zote aweza kutumika.

UMOJA wa nchi za Afrika AU una official languages/Lugha rasmi zinazoweza kutumiwa na viongozi wa nchi hizo bila shida. Nazo ni:
KISWAHILI,
KIARABU,
KIRENO,
KIFARANSA, na
KIINGEREZA.
Rais yeyote ama kiongozi yeyote anaweza KUCHAGUA ni lugha gani ANAYOIPENDA.
Na hivyo kuitumia kuwahutubia viongozi wenzake.
Na hivyo Magufuli kutumia lugha ya KISWAHILI BADO alikuwa katika mpangilio wa AU.
Kuna kale kaujio ka yule rais wa wapi sijui naye alipigwa kiswahili, halafu mbona viongozi wengine hawamuungi mkono number moja?
 
Mkuu labda sijakupata. Viongozi wapi yaani hawamuungi mkono kwa namna gani ili nilielewe swali halafunikujibu.
Samahani lakini.
 
Hapa hata mimi nilipata mashaka na zile sheria za 'NO ENGLISH NO SERVICE' au tulionewa tu? au kila mfalme na zama zake?

Kama inawezekana kutumia swahili peke kwanini tugharamike kuwasomesha watoto wetu FEZA schools? Hii nchi ina sera nyingi sana zinazobishana zenyewe kwa zenyewe.

Kusomesha feza schools ni kupata elimu bora na si lugha.

Hatujawa serious kwenye kusimamia sera tunazoziweka.
 
Moja miongoni mwa alama za utumwa ni kuacha kielelezo cha tamaduni yako na kutumia kielelezo cha tamaduni ya bwana anae kutawala ima kimwili au kimatendo
Na ifike wakati tuone aibu kutumia lugha za wakoloni kwa sababu lugha ndio kielelezo kikuu cha tamaduni na, utambulisho wa watu fulani
JP nampa kongole kuwa juhudi ya kudhihirisha uasilia wetu, hongera, linalo chekesha na kustaajabisha utasiki baadhi ya mabaazazi waliotopewa na kasumba ya utwana wakinena ah !! Fulani hajui kingereza, au kingereza kimemtia aibu, ebo !! Kwani anaasili ipi na uzungu mpaka kingereza iwe aibu kwake. Kutojua? Na majuha wengine husifia fulani anajua kweli kingereza, ebo !!! sasa iweje atabadilika kuwa. Macdonald smith?
 
Swali langu limezaliwa kutokana na matukio kadhaa wa kadhaa yanayojiri kwa sasa hapa nchini na nje ya nchi haswa tukiwa tumewakilishwa na mkuu wa nchi.

Kwa wale tuliosoma shule za kawaida za msingi (zile za serikali wakati huo ujio wa hizi saint nini ulikua bado upo kenya) , tulipata sana taabu kipindi cha presentations za vyuo na secondary kwa matumizi ya lazima ya lugha pendwa ya kiingereza. wale tuliopenda kupiga soga kwa lugha ya taifa tulivishwa bango la swahili speakers, tukazowea na kukubaliana na changamoto na kuishinda.

English ikawa lugha halali ya mawasiliano kiofisi, hata barua pepe tunaandika kwa lugha ya kiingereza, hata kwenye usahili wa kazi sekta zote binafsi na serikali lazima upasue yai.

Sasa namba moja anavyotumia kiswahili kwenye mikutano ya kikazi nje na ndani ya nchi hii imekaaje? au kuna mabadiliko yamefanyika? Kama kuna mabadiliko tafadhali tupeane taarifa wanaforum...

Thank you.....
Hivi ni lini watu kama nyinyi mtakuja kujikomboa kifikra?
 
Back
Top Bottom