TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Katibu Mwenezi wa Chama Cha NRA Taifa, Hamisi Kiswaga amewataka wanasiasa nchini kuacha tabia ya kupiga kelele katika majukwaa na badala yake wabadili maneno hayo kuwa vitendo katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika upataji wa huduma mbalimbali.
Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa ziara yake ya kutembelea idara mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa lengo la kujua matatizo ya Idara hizo pamoja na kutoa maoni na kero zinazowakabili wananchi wanapokuwa wanahitaji huduma kutoka katika idara hizo.
Miongoni mwa maeneo aliyotembelea ni pamoja na idara ya afya na kitengo cha jeshi la polisi katika Idara ya maji (KUWASA).