Kisutu: Kabendera aendelea kusota rumande, Hakimu wa kesi yake ateuliwa kuwa Jaji, kesi yapigwa kalenda

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Novemba 20, 2019 baada ya hakimu aliyekuwa akiisikiliza, Augustine Rwizile kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kabendera katika kesi hiyo anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji wa zaidi ya Sh173 milioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wamkyo Simon leo Alhamisi Novemba 7, 2019 amedai mbele ya Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Wankyo ameeleza kuwa Rwizile ameteuliwa kuwa jaji na kuiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo wakati wakisubiri ipangiwe hakimu mwingine wa kuisikiliza.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Hakimu Mwaikambo aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Katika shtaka la kwanza, Kabendera anadaiwa kuwa alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili anadaiwa kuwa bila sababu, alikwepa kodi ya Sh173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, Kabendera anadaiwa kutakaisha Sh173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

Chanzo: Mwananchi
 
dah rwizile namkubali sana bro wangu alikua ananisaidia sana nivokua arusha wakati akiwa hakimu bado
 
Shtaka la uraia wake ambalo ndo alikatwa nalo naona halitajwi kabisa?

Jamhuri iache kuwasumbua raia wake
 
Kabendera alitumika na Mabeberu kuharibu Amani ya Nchi

Wanasiasa wamemkimbia amebaki peke yake
Sisi Wananchi wa kawaida tuna la kujifunza hapa
Watamkimbia wote lakini naamini Zitto atakuwa naye kama alivyo onesha tangia awali hadi akawa anamsindikiza mahamani.
 
Nimemkumbuka bro Jonas Savimbi, anyway, ila karibia wanaharakati karibia wote hawakuwa na mwisho mwema, labda uwe umenunuliwa na mabeberu kama baba kaburu.
 
Kabendera alitumika na Mabeberu kuharibu Amani ya Nchi

Wanasiasa wamemkimbia amebaki peke yake
Sisi Wananchi wa kawaida tuna la kujifunza hapa

Mkuu uwe makini sana na kauli kama hizi. Maandishi huishi. Kesho unaweza kujikuta upande "wao". Hakuna mwenye haki miliki na sheria. Ni kanuni ya Maisha tuu.

Ni ushauri tuu ndugu yangu.
 
Kabendera alitumika na Mabeberu kuharibu Amani ya Nchi

Wanasiasa wamemkimbia amebaki peke yake
Sisi Wananchi wa kawaida tuna la kujifunza hapa
Hii takataka mataga ni ingizo jipya ya buku saba fc nn mbona inachafua hadhi ya jf kwa kasi ya 4G hv mode pigeni ban hii nguchiro
 
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Novemba 20, 2019 baada ya hakimu aliyekuwa akiisikiliza, Augustine Rwizile kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kabendera katika kesi hiyo anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji wa zaidi ya Sh173 milioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wamkyo Simon leo Alhamisi Novemba 7, 2019 amedai mbele ya Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Wankyo ameeleza kuwa Rwizile ameteuliwa kuwa jaji na kuiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo wakati wakisubiri ipangiwe hakimu mwingine wa kuisikiliza.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Hakimu Mwaikambo aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Katika shtaka la kwanza, Kabendera anadaiwa kuwa alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili anadaiwa kuwa bila sababu, alikwepa kodi ya Sh173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, Kabendera anadaiwa kutakaisha Sh173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

Chanzo: Mwananchi
wacha niweke akiba ya maneno
 
"Nchi ina vituko hii masikini nguvu ya magufuli ndio inatumika ili aendelee kusota jela hakuna kesi apa ni siasa tu."
 
Zitto alimchuuza na sasa kamtelekeza eti anasema Yuki busy na uchaguzi

State agent
 
Kabendera alitumika na Mabeberu kuharibu Amani ya Nchi

Wanasiasa wamemkimbia amebaki peke yake
Sisi Wananchi wa kawaida tuna la kujifunza hapa
Roho mbaya ya Magufuli kujifanya mtakatifu wakati ni fisadi papa a sadist
 
HUYU JAMAA ASIKAMATWA KWA MAKOSA YA UHAMIAJI SO WAMEMZUSHIA KESI NYINGINE KWELI HII SERIKALI NI YA KIZALIMU
 
Wanaharakati uchwara walikuwa na kitu wanaiita black pen thursday kwa ajili ya kabendera, ila sasa ivi naona wamechoka
 
Back
Top Bottom