Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,896
- 2,925
Habari hii inasikitisha sana na nadhani kuna haja Bunge letu lifanye marekebisho ya sheria ya kujamihiana kwani imekuwa ni kawaida kwa akina mama kusingizia kubakwa wakati si kweli: Kwa habari za kina soma hapa chini.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5278
Mwanamke asakwa kwa kuidanganya mahakama kuwa amebakwa
Na Awila Silla , Singida
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida, inamsaka mwanamke mwenye umri wa miaka 38 aliyefungua kesi ya uongo akidai kubakwa na wanaume wawili.
Uchunguzi wa mahakama hiyo umebaini mwanamke huyo alidanganya kwa nia ya kutaka kujipatia kiasi cha Sh1.5 milioni 1.5 kutoka kwa ndugu wa washitakiwa waliyemtuma afanye hivyo.
Mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Majengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida baada ya kugundua mahakama imebaini kuwa ni muongo, anadaiwa kutorokea kusikojulikana.
Agosti 16 mwaka juzi, mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Tatu alifungua kesi ya madai ya kubakwa kwa zamu na wanaume na kupatwa maumivu makali sehemu zake za siri.
Kesi hiyo alifungua dhidi ya Ramadhani Lisu (42), mkazi wa Manga na Mohamed Majengo (45), wa Misinko- Singida Vijijini.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Agatta Chigullu alisisitiza kuwa, mwanamke huyo hakubakwa bali alifanya hivyo ili kutimiza ahadi aliyoahidiwa ya kupatiwa Sh1.5 milioni na ndugu wa washitakiwa waliotaka wanaume hao wafungwe jela ili wamiliki mashamba yao.
Baada ya makubaliano na ndugu wa washitakiwa hao, Tatu alitumia maarifa mengine ya kujitongozesha kwa Yusuf Msaghaa (68) kwa kumweleza kila kitu na kumtaka afanye naye mapenzi bila kinga ili apate uchafu au mbegu za kiuume ambazo zingetumika kama ushahidi kwa ahadi ya malipo ya Sh300,000.
Alisema baada ya tendo hilo, mwanamke huyo, alitoka mbio hadi jirani na nyumba za washitakiwa hao kisha kuanza kulia na kupiga yowe kuomba msaada huku akigaragara kwa madai kuwa amebakwa kwa zamu.
Alisema mayowe hayo, yalimaidia kupata msaada wa jirani akiwemo mmoja wa washtakiwa hao na kudai kuwa amebakwa.
Hakimu aliongeza kuwa, washtakiwa hao, walikamatwa na kupelekwa polisi na Tatu hospitali kwa uchunguzi zaidi na kukutwa akiwa na mbegu za kiume sehemu za siri.
Alisema wakati mahakama hiyo ikiwa katika harakati za kutoa hukumu dhidi ya washitakiwa hao , siri ilifichuka baada ya mwanamke huyo kugundulika kushindwa kumlipa fedha zote mzee aliyefanya naye mapenzi baada ya kufika mahakamani kutoa siri na vielelezo vya maandishi.
Kutokana na hali hiyo, mahakama hiyo ilifuta kesi hiyo na kuamuru Tatu kukamatwa na kufikishwa mahakamani hapo kujibu mashtaka ya kusema uongo.