Kisiasa, mwaka 2017 CCM imeimarika sana!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
38,535
Reaction score
31,199
Namtakia salamu za heri ya krismasi na mwaka mpya 2018 mwenyekiti wa CCM Taifa.

Sio siri mwaka huu CCM imefanikiwa sana kisiasa na kiutendaji pia.

CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza ilani yake na ahadi kwa wananchi.

Yapo mengi ya kujivunia na kutembea kifua mbele kama chama dola.

Vita dhidi ya ufisadi na mafisadi ilipamba moto mwaka huu.

Utetezi wa rasilimali za nchi ni jambo kubwa sana kwa serikali chini ya CCM Kujivunia.

Vita dhidi ya rushwa ndogo na kubwa imeimarika na hatua zimechukuliwa na kuonekana kuchukuliwa.

Maendeleo kwa wananchi wa hali ya chini yameanza kuonekana vilivyo.

Tija katika masoko na bei za mazao ya kilimo hasa hasa kwenye korosho imeonekana.

Viwanda vimeanza kujengwa hasa hasa katika mkoa wa pwani.

Tumeshuhudia uzinduzi wa miradi mikubwa ya maji hasa katika maeneo korofi kama Sengerema na longido.

Fedha za kutosha katika afya hasa eneo la dawa na vifaa tiba imesaidia kubiresha huduma za afya nchini.

Ujenzi wa miuondo mbinu kama ya barabara na madaraja ni eneo lililodhihirisha umadhubuti wa serikali ya JPM.

Kufufuka kwa shirika letu la anga na ndege sio jambo la kubezwa.

Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu imeongezwa na kutolewa kwa wakati na kwa wanaostahili.

Kurejeshwa kwa ardhi zilizopokwa na mafisadi na wabinafsi imewapatia faraja wananchi waliozulumiwa.

Kuondolewa kwa vihiyo na vilaza katika sekta ya huduma za umma sio jambo dogo lakini limefanyika kwa ustadi na werevu wa hali ya juu.

Mikopo kwa vijana na wanawake imewafikia walengwa kwa mara ya kwanza.

Uwajibishwaji wa papo kwa papo kwa viongozi wazembe wa umma umeonesha nia na dhamiri safi ya Serikali ya JPM.

Ukusanyaji wa kodi halali za serikali umeumeonesha uimara wa Serikali ya JPM.

Utalii umeboreka huku ujangili dhidi ya Tembo na wanyama wengine muhimu umepungua kwa kasi.

Usimamizi wa rasilimali zetu kama nchi umeimarishwa kiusimamizi na kisheria.

CCM imeweza kuwavutia wanachama muhimu na wengi wa vyama vya upinzani hadi wakajiuzulu na kujiunga na CCM ili kuwa huru na kumsupport Magufuli katika kuleta maendeleo ya mama Tanzania.

Chini ya uwenyekiti wa Rais Magufuli CCM imeweza kuunganishwa upya na kutoa fursa kwa kila mwanaccm.

WanaCCM wote wanapaswa kuyatambua mazuri mengi yaliyotekelezwa na kikosi kazi chini ya Rais Magufuli...na hivyo wanatakiwa kuyasema na kuwaelimisha wananchi.

Yapo mengi ya kuyaelezea lakini kwa kifupi naweza kuyataja haya.

Tuingeze mengine ili tujitathmini kama nchi.

Mungu amponye na kumlinda Rais wa Jamhuri huru ya Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama dola CCM ndugu John Pombe Magufuli.

Magufuli as expected has shown the world that he is more than a politician...he is a performance oriented leader!!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
karibuni wanaccm tumpongeze na kumshangilia mwenyekiti wetu
 
Upinzani utaongelea lipi haswa zaidi ya kuzusha?
 
Kwa gharama ya demokrasia changa ya nchi, damu za wapinzani na rushwa inayochotwa hazina kwa ajili ya manunuzi ya madiwani na wabunge.
Hakuna demokrasia nzuri kama kuteua wapinzani katika nafasi za kiserikali.Hilo limefanyika mwaka huu
 
FB_IMG_1513051508549.jpg
 
Namtakia salamu za heri ya krismasi na mwaka mpya 2018 mwenyekiti wa CCM Taifa.

Sio siri mwaka huu CCM imefanikiwa sana kisiasa na kiutendaji pia.

CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza ilani yake na ahadi kwa wananchi.

Yapo mengi ya kujivunia na kutembea kifua mbele kama chama dola.

Vita dhidi ya ufisadi na mafisadi ilipamba moto mwaka huu.

Utetezi wa rasilimali za nchi ni jambo kubwa sana kwa serikali chini ya CCM Kujivunia.

Vita dhidi ya rushwa ndogo na kubwa imeimarika na hatua zimechukuliwa na kuonekana kuchukuliwa.

Maendeleo kwa wananchi wa hali ya chini yameanza kuonekana vilivyo.

Tija katika masoko na bei za mazao ya kilimo hasa hasa kwenye korosho imeonekana.

Viwanda vimeanza kujengwa hasa hasa katika mkoa wa pwani.

Tumeshuhudia uzinduzi wa miradi mikubwa ya maji hasa katika maeneo korofi kama Sengerema na longido.

Fedha za kutosha katika afya hasa eneo la dawa na vifaa tiba imesaidia kubiresha huduma za afya nchini.

Ujenzi wa miuondo mbinu kama ya barabara na madaraja ni eneo lililodhihirisha umadhubuti wa serikali ya JPM.

Kufufuka kwa shirika letu la anga na ndege sio jambo la kubezwa.

Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu imeongezwa na kutolewa kwa wakati na kwa wanaostahili.

Kurejeshwa kwa ardhi zilizopokwa na mafisadi na wabinafsi imewapatia faraja wananchi waliozulumiwa.

Kuondolewa kwa vihiyo na vilaza katika sekta ya huduma za umma sio jambo dogo lakini limefanyika kwa ustadi na werevu wa hali ya juu.

Mikopo kwa vijana na wanawake imewafikia walengwa kwa mara ya kwanza.

Uwajibishwaji wa papo kwa papo kwa viongozi wazembe wa umma umeonesha nia na dhamiri safi ya Serikali ya JPM.

Ukusanyaji wa kodi halali za serikali umeumeonesha uimara wa Serikali ya JPM.

Utalii umeboreka huku ujangili dhidi ya Tembo na wanyama wengine muhimu umepungua kwa kasi.

Usimamizi wa rasilimali zetu kama nchi umeimarishwa kiusimamizi na kisheria.

CCM imeweza kuwavutia wanachama muhimu na wengi wa vyama vya upinzani hadi wakajiuzulu na kujiunga na CCM ili kuwa huru na kumsupport Magufuli katika kuleta maendeleo ya mama Tanzania.

Chini ya uwenyekiti wa Rais Magufuli CCM imeweza kuunganishwa upya na kutoa fursa kwa kila mwanaccm.

Yapo mengi ya kuyaelezea lakini kwa kifupi naweza kuyataja haya.

Tuingeze mengine ili tujitathmini kama nchi.

Mungu amponye na kumlinda Rais wa Jamhuri huru ya Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama dola CCM ndugu John Pombe Magufuli.

Magufuli as expected has shown the world that he is more than a politician...he is a performance oriented leader!!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Hakika inapendeza.
 
Ni imeimarika sana ila ili tujiridhishe zaidi hebu fanyeni kuondoa vikwazo mikutano ya kisiasa kama enzi za JK
 
Back
Top Bottom