Kishindo cha Oparesheni 255 Katiba Mpya Okoa Bandari kuanzia Kagera, Freeman Mbowe kuongoza Mashambulizi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,775
218,396
Awamu ya Pili ya mpango kabambe wa kuwaamsha wananchi wa Tanzania kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, ambao sasa umeongezewa kipengele cha "Okoa Bandari Zetu," unaanza rasmi 28/07/2023 Mkoani Kagera.

Taarifa iliyosambazwa na Chadema kote duniani inaonyesha kwamba mkutano mkubwa wa hadhara wa kuzindua kampeni hiyo utafanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa, Manispaa ya Bukoba na utaongozwa na Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe akiwa pamoja na Tundu Lissu.

Nimebahatika kuwemo kwenye Timu ya Wataalam Wasomi, waliokagua Chopa itakayotumika kwa mashambulizi ya angani. Kiukweli, chama kimejipanga na sasa kimekomaa hasa, mipango yake ni ya kisasa mno hadi inashangaza! Watu wa Kagera wana bahati sana kwa kampeni hii, kuanzia kwao, maana kila kitu ni kipya kabisa, hadi mic ni mpya!

Kama kawaida, mimi mtumishi wenu Erythrocyte nitawaletea kila kitakachojili.

Mungu ibariki Chadema.
 
Aiseeh Chopa ina maandishi ya Kiukombozi yaani hata ikiwa km 50 angani YANASOMEKA

Mashambulizi ya angani na nchi kavu yakianza ndani ya nusu saa wataomba poo.....

Ikumbukwe ni Kanda ya Ziwa....gete gete
Moto wa kifuu
 
Back
Top Bottom